Mkataba wa Richmond wafutwa
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,July 01, 2008 @00:01
Ni baada ya ushauri wa kisheria
Tanesco yasema haukuwa halali
SERIKALI imefuta mkataba kati yake na kampuni ya kutoa huduma ya umeme ya Dowans Tanzania Ltd kuanzia Agosti mosi mwaka huu. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupata ushauri wa kisheria kwamba mkataba kati ya shirika hilo na Kampuni ya Richmond ambayo mkataba wake ulihamishiwa Dowans, haukuwa halali wala haukuwa na nguvu kisheria.
Dk. Rashid alisema kutokana na mkataba kati ya Richmond na Tanesco kuwa na utata, shirika hilo liliajiri kampuni ya sheria kutoa ushauri wa uhalali wa utaratibu mzima wa mkataba huo. Hakuitaja kampuni gani. Alisema kampuni hiyo ilibaini kuwa utaratibu mzima wa ununuzi wa huduma hiyo ya umeme na kuingia mkataba na Richmond Development Company LLC, ulikiuka sheria ya ununuzi namba 21 ya 2004.
Kutokana na mapendekezo ya ripoti hiyo, serikali iliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo, na juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliahidi kuwa yuko tayari kutoa taarifa ya serikali kuhusu ilivyofanyia kazi mapendekezo ya Bunge.
Mkataba unaisha 30 july 08 ...je wataendelea kulipwa mpaka tarehe hio?....kwa nini wasivunje mkataba palepale kama imejulikana ni batili?...je fedha walizochukua wanazirudisha?...isiwe tunazugwa hapa...
huu sasa wizi.... yaani wameajiri kampuni ya sheria kuwashauri kwa mambo ambayo tumeyaandika magazetini? Nadhani it is about time watugawie hiyo fee waliyowalipa hao jamaa.
Tangu siku ya kwanza tuliwaambia mkataba wa Dowans hauna msingi wa sheria na tukasema ni kwanini kweli wanaenda kuajiri mtu mwingine kuwaambia kitu ambacho kiko dhahiri?
Hii inaudhi kweli!!
Hatua nzuri sana, lakini vipi sasa, je pesa walizokwisha chukua zitarudishwa?
Kama mkataba haukuwa halali kwa nini isiwe immediate contract termination...kwa nini mpaka agosti mosi?
je wanaendelea kulipwa mapaka siku hiyo?
Unajua nini, angalau safari hii wameajiri law firm ya Kibongo. Huwa nachukia sana ma contract wakipewa wageni.
Originally Posted by Bubu ataka kusema
Dk. Rashid alisema kutokana na mkataba kati ya Richmond na Tanesco kuwa na utata, shirika hilo liliajiri kampuni ya sheria kutoa ushauri wa uhalali wa utaratibu mzima wa mkataba huo. Hakuitaja kampuni gani. Alisema kampuni hiyo ilibaini kuwa utaratibu mzima wa ununuzi wa huduma hiyo ya umeme na kuingia mkataba na Richmond Development Company LLC, ulikiuka sheria ya ununuzi namba 21 ya 2004.
But then again ndio unakuta ma law firm hayo hayo ya Wabunge wa CCM.
Yale yale!
...hivi hakuna media TZ kumbana huyu Idrissa Rashid ili kumwaibisha maana wanaona sisi ni wajiiinga sana ...wamwambie wazi wazi mkataba unaisha 30 July kwa hiyo story za kuvunjwa 1st Agost ni mkataba gani anaongelea hapo...kazi kweli kweli yaani mafisadi yamejisahau mpaka hawajui wanaongea nini? lingine kule limekurupuka na kusema EPA sio pesa za serikali,tuna wendawazimu watupu pale,dawa ni kuwaonyesha njia 2010
Mkuu I feel you!huu sasa wizi.... yaani wameajiri kampuni ya sheria kuwashauri kwa mambo ambayo tumeyaandika magazetini? Nadhani it is about time watugawie hiyo fee waliyowalipa hao jamaa.
Tangu siku ya kwanza tuliwaambia mkataba wa Dowans hauna msingi wa sheria na tukasema ni kwanini kweli wanaenda kuajiri mtu mwingine kuwaambia kitu ambacho kiko dhahiri?
Hii inaudhi kweli!!
Who are these shameless, merciless bloodthirst criminals behind these bogus Companies? I will cast the first stone....
...hii yote ni kwa sababu tuna Raisi ambaye ni mtupu kichwani,huyu jamaa ametucost sana na huu upuuzi wao tutaulipia for the next 50 yrs!
huu sasa wizi.... yaani wameajiri kampuni ya sheria kuwashauri kwa mambo ambayo tumeyaandika magazetini? Nadhani it is about time watugawie hiyo fee waliyowalipa hao jamaa.
Tangu siku ya kwanza tuliwaambia mkataba wa Dowans hauna msingi wa sheria na tukasema ni kwanini kweli wanaenda kuajiri mtu mwingine kuwaambia kitu ambacho kiko dhahiri?
Hii inaudhi kweli!!
na waziri Ngeleja kadhibitisha ulikuwa ni mkataba batili na wanatakiwa waondoe mitambo yao ifikapo agust mosi.Hongera kamati ya Mwakyembe
Hivi jamani huyu Ngeleja si alikuwa wizara hii hii (wakati wa kusaini mkataba)!! sasa nini tena leo anasema "wamegundua" mkataba ulikuwa "fake", jamani huyu Ngeleja si ni yule mtaalamu wa masuala ya sheria!? Jamani hii imekaaje!
Mi binafsi sikubaliani na maelezo mepesi namna hii, ninachotaka bunge litengue kile kipengele cha sheria kisha mjadala ya Richmond urudiwe tena kujadiliwa!! Mpaka mchawi apatikane!!