Dotto Biteko: Tusiruhusu viongozi wa nchi yetu kutwezwa utu wao

Mwacheni kijana afanye kazi, he is very royal heshima kwa wakubwa inambeba,
 
Siku za hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakitumia uhuru waliopewa kutukana na kudhalilisha Viongozi badala ya kujadili hoja hususani kwenye uwekezaji wa Bandari.
simple, tungeni sheria mfute vyama vya siasa ili mtawale mnavyotaka, maana Bunge ni lenu, Jeshi lenu, mahakama na pilato mkuu mnamlipa ninyi - sisi ni kina nani tubishe.
 
Huyu mwl wa praimari naye anasemaje? Tutetee nchi kwanza isitwezwe viongozi wajitetee wenyewe Kwa utendaji mahiri!!!
Katiba mpya na time huru ya uchaguzi kwanza!!
 
CHADEMA ambao mda wote wanatukana na kudhalilisha Viongozi wameendelea kuonywa na Viongozi mbalimbali ambapo Dotto Biteko amekemea Vikali upuuzi huo.

Siku za hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakitumia uhuru waliopewa kutukana na kudhalilisha Viongozi badala ya kujadili hoja hususani kwenye uwekezaji wa Bandari.

Ukiacha kudhalilisha utu wa Viongozi, CHADEMA wamekuwa wanahubiri migawanyiko ya Kitaifa Kwa msingi wa maeneo na ukabila kinyume na tunu za Taifa hili..

My Take
Nitoe wito Kwa Wananchi kuwakataa na kuwalaani pia Serikali isiwachekee

======
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Doto Mashaka Biteko (Mb) ambaye pia ni Waziri wa Madini amekemea vikali kejeli, kutweza utu wa viongozi na kauli za kuudhi ikiwemo matusi.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan aliruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa lakini baadhi ya wanasiasa wanatumia vibaya uhuru huo na kuanza kashfa dhidi ya viongozi.

Mhe Biteko ameyasema hayo mjini Katoro katika Jimbo la Busanda wakati wa mkutano wa hadhara wa wananchi ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndg Nicolas Kasendamila kwa ajili ya kueleza mafanikio ya serikali na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo itafanyika katika majimbo yote ya mkoa huo.

"Ukweli tufanyeni siasa maana siasa ni pamoja na kuwa na mawazo kinzani, wacha tuyafanye lakini tusichukue muda mwingi tukaruhusu kutukanana, kudhalilishana, tukaruhusu viongozi wa nchi yetu wakatwezwa utu wao" Amekaririwa Dkt Biteko

Mhe Biteko amesema kuwa wote wanaotoa kejeli na matusi kwa viongozi wanapaswa wapuuzwe kwa sababu hawana hoja wala ajenda ya maendeleo.

Mhe Biteko amesisitiza ulazima wa wana CCM kujibu hoja bila kujibu kejeli ama matusi, waushinde ubaya kwa wema huku akisema kuwa wananchi wa vyama vyote ni ndugu na sio maadui. Na amewataka wa vyama vingine kuheshimiana miongoni mwao na kuwaheshimu wana CCM maana wote ni ndugu.

"Hakuna muujiza wa kuwatambua watu wanaosema uongo ama wanaosema ukweli zIdi sana watatambuliwa kwa matendo yao, kadhalika Rais wetu Mhe Samia atatambuliwa kwa matendo yake na sio maneno, kazi zake zinamtambulisha kama Rais aliyeamua kuwaletea maendeleo ya haraka Watanzania”. Amesisitiza Mhe Biteko

Kuhusu maendeleo Mhe Biteko amesema kuwa Maendeleo ni mchakato wa ukuaji unaoweza kuhusisha: Matumizi ya ardhi, sayansi na teknolojia, sayansi ya jamii, biashara na ueledi hivyo Mhe. Rais anaweza kufanya kila kinachotakiwa kufanywa lakini bado kukahitajika jambo jingine kufanyika kutokana na uhitaji wa wakati huo.
Wewe mbona ulikuwa umtukana Magufuli?nyie machawa ni ovyo sana.
 
Hovyo ni wewe hapo,msingi wa Mimi kumtukana Mwendazake ni uendeshaji mbaya wa uchumi Kila kitu kilihatibika Ajira hakuna uwekezaji hakuna , biashara kufa ,kupora pesa,mazao ya wakulima kuanguka bei,kujenga mamiradi ya hovyo tuu yasiyo na Tija ila Yana sifa na upuuzi kama huo.
 
Sasa Watu wanatukana sasa hivi kwa sababu serikali imekuwa ovyo kwenye kila kitu.
 
Tunahitaji kujenga taifa lenye wananchi wanaoheshimiana kuanzia mdogo hadi mkubwa, mwenye madaraka au cheo na asiye nacho.
Kila mmoja atimize wajibu wake kwa weledi na heshima.
Katika jamii au nchi isiyo na maadili;
Bunduki yaweza kutumika kulinda mali yako na hiyo hiyo yaweza kutumika kuiba mali yako, Mahakama kuhukumu wasio na kosa, gereza kufunga wasio na makosa, polisi kulinda/kutetea wezi, bunge kuwakilisha Serikali badala ya wananchi,.......
Kazi kubwa ya viongozi kwa sasa ni kurudisha na kuisimamia uadilifu.
Changamoto kubwa ni kuwapata ambao ni waadilifu.
Kila mtu atimize wajibu wake? Kuuza bandari ni kutimiza wajibu?
 
Lugha za matusi sio sehemu ya ustaarabu
Si Bora wao wanatukana kama ni kweli,wao kupigwa Risasi,Kuvunjwa miguu,kufungulia Makesi ya ajabu ajabu,kuharibiwa Mali zao halali,kufungiwa account zao benk,kuanzishwa account fake nk,hatua zipi huchukulia?
 
CHADEMA ambao mda wote wanatukana na kudhalilisha Viongozi wameendelea kuonywa na Viongozi mbalimbali ambapo Dotto Biteko amekemea Vikali upuuzi huo.

Siku za hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakitumia uhuru waliopewa kutukana na kudhalilisha Viongozi badala ya kujadili hoja hususani kwenye uwekezaji wa Bandari.

Ukiacha kudhalilisha utu wa Viongozi, CHADEMA wamekuwa wanahubiri migawanyiko ya Kitaifa Kwa msingi wa maeneo na ukabila kinyume na tunu za Taifa hili..

My Take
Nitoe wito Kwa Wananchi kuwakataa na kuwalaani pia Serikali isiwachekee

======
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Doto Mashaka Biteko (Mb) ambaye pia ni Waziri wa Madini amekemea vikali kejeli, kutweza utu wa viongozi na kauli za kuudhi ikiwemo matusi.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan aliruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa lakini baadhi ya wanasiasa wanatumia vibaya uhuru huo na kuanza kashfa dhidi ya viongozi.

Mhe Biteko ameyasema hayo mjini Katoro katika Jimbo la Busanda wakati wa mkutano wa hadhara wa wananchi ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndg Nicolas Kasendamila kwa ajili ya kueleza mafanikio ya serikali na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo itafanyika katika majimbo yote ya mkoa huo.

"Ukweli tufanyeni siasa maana siasa ni pamoja na kuwa na mawazo kinzani, wacha tuyafanye lakini tusichukue muda mwingi tukaruhusu kutukanana, kudhalilishana, tukaruhusu viongozi wa nchi yetu wakatwezwa utu wao" Amekaririwa Dkt Biteko

Mhe Biteko amesema kuwa wote wanaotoa kejeli na matusi kwa viongozi wanapaswa wapuuzwe kwa sababu hawana hoja wala ajenda ya maendeleo.

Mhe Biteko amesisitiza ulazima wa wana CCM kujibu hoja bila kujibu kejeli ama matusi, waushinde ubaya kwa wema huku akisema kuwa wananchi wa vyama vyote ni ndugu na sio maadui. Na amewataka wa vyama vingine kuheshimiana miongoni mwao na kuwaheshimu wana CCM maana wote ni ndugu.

"Hakuna muujiza wa kuwatambua watu wanaosema uongo ama wanaosema ukweli zIdi sana watatambuliwa kwa matendo yao, kadhalika Rais wetu Mhe Samia atatambuliwa kwa matendo yake na sio maneno, kazi zake zinamtambulisha kama Rais aliyeamua kuwaletea maendeleo ya haraka Watanzania”. Amesisitiza Mhe Biteko

Kuhusu maendeleo Mhe Biteko amesema kuwa Maendeleo ni mchakato wa ukuaji unaoweza kuhusisha: Matumizi ya ardhi, sayansi na teknolojia, sayansi ya jamii, biashara na ueledi hivyo Mhe. Rais anaweza kufanya kila kinachotakiwa kufanywa lakini bado kukahitajika jambo jingine kufanyika kutokana na uhitaji wa wakati huo.
Anaanza kulipa fadhila ya uteuzi mapema sana
 
Naibu waziri mkuu wa Wasukuma.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom