Dotto Biteko: Tusiruhusu viongozi wa nchi yetu kutwezwa utu wao

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,110
49,822
CHADEMA ambao mda wote wanatukana na kudhalilisha Viongozi wameendelea kuonywa na Viongozi mbalimbali ambapo Dotto Biteko amekemea Vikali upuuzi huo.

Siku za hivi karibuni CHADEMA wamekuwa wakitumia uhuru waliopewa kutukana na kudhalilisha Viongozi badala ya kujadili hoja hususani kwenye uwekezaji wa Bandari.

Ukiacha kudhalilisha utu wa Viongozi, CHADEMA wamekuwa wanahubiri migawanyiko ya Kitaifa Kwa msingi wa maeneo na ukabila kinyume na tunu za Taifa hili..

My Take
Nitoe wito Kwa Wananchi kuwakataa na kuwalaani pia Serikali isiwachekee

======
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Doto Mashaka Biteko (Mb) ambaye pia ni Waziri wa Madini amekemea vikali kejeli, kutweza utu wa viongozi na kauli za kuudhi ikiwemo matusi.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan aliruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa lakini baadhi ya wanasiasa wanatumia vibaya uhuru huo na kuanza kashfa dhidi ya viongozi.

Mhe Biteko ameyasema hayo mjini Katoro katika Jimbo la Busanda wakati wa mkutano wa hadhara wa wananchi ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndg Nicolas Kasendamila kwa ajili ya kueleza mafanikio ya serikali na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo itafanyika katika majimbo yote ya mkoa huo.

"Ukweli tufanyeni siasa maana siasa ni pamoja na kuwa na mawazo kinzani, wacha tuyafanye lakini tusichukue muda mwingi tukaruhusu kutukanana, kudhalilishana, tukaruhusu viongozi wa nchi yetu wakatwezwa utu wao" Amekaririwa Dkt Biteko

Mhe Biteko amesema kuwa wote wanaotoa kejeli na matusi kwa viongozi wanapaswa wapuuzwe kwa sababu hawana hoja wala ajenda ya maendeleo.

Mhe Biteko amesisitiza ulazima wa wana CCM kujibu hoja bila kujibu kejeli ama matusi, waushinde ubaya kwa wema huku akisema kuwa wananchi wa vyama vyote ni ndugu na sio maadui. Na amewataka wa vyama vingine kuheshimiana miongoni mwao na kuwaheshimu wana CCM maana wote ni ndugu.

"Hakuna muujiza wa kuwatambua watu wanaosema uongo ama wanaosema ukweli zIdi sana watatambuliwa kwa matendo yao, kadhalika Rais wetu Mhe Samia atatambuliwa kwa matendo yake na sio maneno, kazi zake zinamtambulisha kama Rais aliyeamua kuwaletea maendeleo ya haraka Watanzania”. Amesisitiza Mhe Biteko

Kuhusu maendeleo Mhe Biteko amesema kuwa Maendeleo ni mchakato wa ukuaji unaoweza kuhusisha: Matumizi ya ardhi, sayansi na teknolojia, sayansi ya jamii, biashara na ueledi hivyo Mhe. Rais anaweza kufanya kila kinachotakiwa kufanywa lakini bado kukahitajika jambo jingine kufanyika kutokana na uhitaji wa wakati huo.
 
..Viongozi ktk nchi hii sio Ccm tu.

..hata viongozi wa vyama vya upinzani nao wanastahili heshima.

..Biteko awaase vijana wa Ccm waache kutukana na kuwatweza viongozi wa vyama vya upinzani.
Ccm Huwa haidhalilishi utu wa viongozi wa upinzani
 
makuwadi na vibaraka ya dpworld lazima yarudishe hela yalizohongwa na warabu koko wa dubai ili kutoa bandar za tanganyika bure na bila ukomo kwa hao warabu koko, naridia tena makuwadi ya warabu koko lazima hela za hongo mzitapike.
Hapo ndipo wanapochanganyikiwa
 
Tajiri, Bilionea Dotto Biteko.. na PhD fake yako,

Kwahiyo kutoruhusu ni kufanyaje?

Tabia za nchi jirani,Burundi na Rwanda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom