Dotto Biteko: Tumezima mtambo wa bwawa la Mwl Nyerere

Verrazanno

JF-Expert Member
Sep 15, 2021
384
783
AFRIKA tuna shida jamani. Sasa inabidi tumwombe Mungu apunguze mvua.

Mitambo inazama majini. Serikali imeshtuka baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kutangaza mvua inanyesha kali viunga hivyo. Wakati wana dizaini bwawa hawakujua kuna siku mvua zitapiga, hakuna provision ya kuchepusha maji yanapozidi....

MWANANCHI ONLINE
APRIL 1st 2024

Mashine yazimwa Julius Nyerere

biteko 2.jpg

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dr. Dotto Biteko, akikagua mitambo ya kufua umeme

Biteko amesema kutokana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kutangaza uwepo wa mvua kubwa kwenye maeneo mengi, wizara hiyo itaendelea kuchukua kila hatua ya tahadhari

“Mfano Kituo cha Julius Nyerere ipo mashine moja ya kuzalisha umeme, lakini maji yanayozalishwa pale ni mengi sana kinyume kabisa na mipango tuliyokuwa nayo"

Maana tulikuwa tunajua kwamba Julius nyerere ingeweza kujaa bwawa lile mwezi wa 12 mwaka 2026, lakini yamejaa ndani ya msimu huu tu mmoja na yale maji yanavyojaa yanakuja mengi kwa wakati mmoja,” amesema.

Amesema baada ya kuona wingi walitoa tahadhari Machi kwa watu wote walioko upande wa chini wa bwawa, kwamba wangeachia maji maana uwezo wa kuendelea kuyashikilia haupo.

“Ukianza kufungulia yale maji, Julius Nyerere lazima uizime, maana yanayotoka juu ni mengi zaidi kuliko yanayotoka kwenye teresi, hivyo ninavyozungumza mtambo wa Julius Nyerere tumeuzima, tunapunguza maji ili tupate umeme," amesema Dk Biteko
 
Nadhani concept ni moja.

Kuna mashine 9, inayofanya kazi ni moja. Bwawa linatakiwa kuhifadhi maji ya mashine 9.

Sasa kama mashine moja kati ya 9 ndio inafanya kazi, maji mengine hayana sababu ya kuwepo pale, lazima yafunguliwe yaondoke.

Iwapo mashine zote 9 zingekua zinafanya kazi basi hayo maji bado yasingetosha.

Ni serikali kuhakikisha mashine zote zinawashwa kwa wakati mmoja tu ama vinginevyo yale maji yote yatapotea bure.
 
Hayo yote hawakuwa wameyaona awali?

Hakukuwepo na contingency plans zozote zile kuhusu maji kuwa mengi?
 
kama sikosei, Model ya bwawa inaonyesha kuwa kuna michepuko nadhani miwili kulia na kushoto kwa ajili kuruhusu maji yapungue pale bwawa linapokuwa na maji ya ziada. Kulikoni?
Hakuna cha kulikoni, kuna ujinga tu:

Sasa wakishayapunguza maji kipindi cha kiangazi watasema maji ni machache mno. Shenzi taipu zao hao wawashe mashine zote watengeneze storage facility za umeme ili utumike kipindi maji yakiwa machache kipindi cha kiangazi ndio wazime baadhi ya mashine.
 
Makadirio yao yalikuwa bwawa lijae 2026 lakini limejaa ndani ya msimu mmoja tu 2023/24.... Hivi haya yalikuwa makadirio ya aina gani?

Hapo waseme tu walikuwa wanataka kuwapiga watanzania dana dana hadi 2026 lakini walivyoona kelele zimezidi ndo wakawasha kamtambo kamoja.

Hako kamtambo kamoja kati ya 9 iliyopo ndo kanawapa shida hivi, je zikiwashwa zote 9 wataweza kuzimanage kweli?

Majii yakijaa shida, yakipungua shida. Sitashangaa wakitangaza mgao wa umeme sababu maji yamejaa na yakipungua tena watatangaza mgao na kutuhimiza tuombee mvua zinyeshe bwawa lijae.... Hii nchi ni kama wote tupo chekechea.
 
AFRIKA tuna shida jamani. Sasa inabidi tumwombe Mungu apunguze mvua.

Mitambo inazama majini. Serikali imeshtuka baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kutangaza mvua itanyesha kali. Wakati wana dizaini bwawa hawakujua kuna siku mvua zitapiga kali. Hakuna provision ya kuchepusha maji yanapozidi....

MWANANCHI ONLINE
APRIL 1st 2024

Mashine yazimwa Julius Nyerere

View attachment 2951205
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dr. Dotto Biteko, akikagua mitambo ya kufua umeme

Biteko amesema kutokana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kutangaza uwepo wa mvua kubwa kwenye maeneo mengi, wizara hiyo itaendelea kuchukua kila hatua ya tahadhari

“Mfano Kituo cha Julius Nyerere ipo mashine moja ya kuzalisha umeme, lakini maji yanayozalishwa pale ni mengi sana kinyume kabisa na mipango tuliyokuwa nayo"

Maana tulikuwa tunajua kwamba Julius nyerere ingeweza kujaa bwawa lile mwezi wa 12 mwaka 2026, lakini yamejaa ndani ya msimu huu tu mmoja na yale maji yanavyojaa yanakuja mengi kwa wakati mmoja,” amesema.

Amesema baada ya kuona wingi walitoa tahadhari Machi kwa watu wote walioko upande wa chini wa bwawa, kwamba wangeachia maji maana uwezo wa kuendelea kuyashikilia haupo.

“Ukianza kufungulia yale maji, Julius Nyerere lazima uizime, maana yanayotoka juu ni mengi zaidi kuliko yanayotoka kwenye teresi, hivyo ninavyozungumza mtambo wa Julius Nyerere tumeuzima, tunapunguza maji ili tupate umeme," amesema Dk Biteko
Watu wa ajabu tu hawa; hakuna bwawa duniani linalojengwa bila kuwa na spillway. Ni kama kujenga nyumba ya ghorofa bila kuwa na ngazi. Kazi spillway ni kuruhusu maji ya zaida kupita
 
Y

Yaani hakuna overflow?
Nchi ngumu hii

Watanzania walienda shule kusomea ujinga.

Hakuna cha kulikoni, kuna ujinga tu:

Najiuliza shina ni nini? hatuna weledi, hatuna teknolojia, poor decision making au poor political will au Bwegez wamejaa kwenye hiyo Taasisi? Inasikitisha sana! kujenga bwawa tabu!! hata uratibu wa bwawa nao tabu. sijui kipi tunaweza sasa. Au tunahitaji tuletewe tena SAP part II
 
Back
Top Bottom