Dotto Biteko aagiza wadaiwa sugu wa TANESCO wakatiwe umeme

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Screenshot 2023-11-26 165516.png

Botto Biteko mesema TANESCO ina wadaiwa sugu ambao wanadaiwa takribani Bilioni 224 za matumizi ya umeme na hawajalipa.

Naunga mkono hoja, ila hapo utakuta 99% ni Taasisi za Serikali kama Hospital, Mamlaka za Maji na Ofisi za Umma.

Swali je, agizo lake litatekelwzeka? Maana TANESCO sio shirika la kibiashara, ni la huduma.

====

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameiagiza TANESCO kukata umeme kwa wadaiwa wote wasiolipa gharama za kutumia umeme ambapo Shirika hilo linadai jumla ya Shilingi Bilioni 224 kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Binafsi na waliohama na madeni.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amekemea vikali watu wote wanaohujumu miundombinu ya umeme akitolea mfano wizi wa shaba na mafuta ambapo kati ya tarehe 25 Novemba, 2023 na 26 Novemba, 2024 kuna matukio 14 katika Ukanda wa Pwani ya kuharibu au kuhujumu miundombinu ya umeme.

Dkt. Biteko ametaka Watanzania kulinda vyanzo vya maji ambavyo vinazalisha umeme, amesema vyanzo hivyo visipolindwa vitapelekea athari mbalimbali zikiwemo kwenye uzalishaji umeme, pia ameitaka TANESCO kutokukaa nyuma katika masuala ya utunzaji wa mazingira.
 
Kateni ndio mboni sisi huku tunatumia luku prepaid ukiisha tunanunua tena kwanini hao wasifungiwe luku kubwa kwamba ukikata wanalipia wasipolipia wanalala Giza km sisi huku mtaani wanaogopa nini kuwafungia luku?

Kateni badirisheni miundombinu wafungueni luku wote ili kuondoa malalamiko ya ajabu ajabu
 
Back
Top Bottom