..ni vigumu sana kuelewa msimamo wa wa-Zanzibar.
..kwanza wanasema hawataki muungano, halafu wanageuka wanasema makubaliano ya muungano yamekiukwa.
..kama hawataki muungano, basi waachane na hoja kwamba makubaliano ya muungano yamekiukwa. badala yake wajenge hoja kwamba muungano ni hasara na usumbufu kwa wa-Zanzibar.
..pia kuna wakati hulalamika kwamba wanataka Raisi wa Zanzibar awe makamu ktk serikali ya muungano. sasa hii nadhani ni hoja ya watu wanaopenda muungano.
..kwa upande wa Tanganyika nadhani wengi, haswa wanasiasa, wanaona aibu au uwoga kutamka kwamba hawataki muungano. Watanganyika tunapaswa kujiuliza tunafaidika nini na muungano huu? je, ukiondoka tutapungukiwa na kitu gani?
Unajuwa si lazima wewe uwaelew Wazanzibari kwani wewe si mmja wao na wala huoni tabu ya kutawaliwa.
Kama ni kuungana basi ni suala la kuwepo kuthaminiana kama vitu vilivyoungana na kutowa haki kwa kila upande. Si vizuri kuona opande mmoja ukijiona kuwa una haki zaidi ya mwenziwe. Kama Muungano unakuwa katika misingi hiyo kwanini kisiwe kitu kizuri?
Inapokosekana hali hiyo na mmoja akajifanya kuwa mbora kwa mwenziwe basi ndipo inapokuja kauli ya kusema Hatutaki Muungano.
Nafikiri sasa wafahamu Wazanzibari kuwa wanatowa option mbili hizo.