Does age matters in relationships/love/marriage?

Nadhani wana JF kwa hili hamjamjibu jamaa swali! kwangu mie umri unaotakiwa kuwa tofauti baina ya mume na mke ni kuanzia miaka 0-3. Tofauti isizidi hapo. Wataalamu wanasema, tofauti ya umri unavyokuwa ndogo baina ya couples ndivyo uimara na ubora wa ndoa unavyoongezeka. Lakini pia kumbuka kuna kuzeeka, kama unamwoa unayemzidi umri wewe mwanamke au mwanaume ujue mmoja wenu atazeeka na kumwacha mwingine bado anademand kitu.. katika life sasa hapo ndo kunakuwepo na tatizo. inashauriwa kuwa bora mzeeke wote mtajua namna ya kutunzana na uzee wenu badala mmoja kuanza kuhisi kuwa mwenzie ni mzigo kwake.

Nakupa mfano wa halisi niliouona kwngu mie. mimi nilioa katika age 26 na mke wangu 27, hadi leo tunaishi bila matatizo yoyote. kunapokuwepo na tofauti ya mawazo mnaanza kuelimishana polepole hadi mnaelewana. lakini kama age difference ni kubwa, unaweza mdhania mwenzio anafanya hayo kwakuwa yeye ni mtoto na hivyo kuleta dharau na kutokuelewana katika familia au ndoa yenu.

Mfano mwingine, Babu yangu mie alioa wake 3 wenye umri tofautitofauti. Wakati akiwa bado ananguvu ya utafutaji, alikuwa na mapenzi na mke mdogo kuliko 1 na 2. Alivozeeka, mdogo wala hakumjali na ilibidi arejeshe "majeshi" kwa bi Mkubwa na wakati mwingine kwa wa 2. Alitunzwa vizuri sana na mke mkubwa hadi alipo fariki. So, you can think from the 2 examples.

But what i want to tell you which is the most important in marriage is LOVE and not AGE. age, is a variable that also plays its role in marriage but not as important as to LOVE. kama unampenda mkeo na mna umri sawa au unaolingana, huyo ndo wa kuoa provided that you both LOVE each other.

Jamii au tamaduni zinaweza kuanza kukusumbua kuwa watu watanielewaje?Kama mke wako ni wa JAMII na siyo mkeo basi usimuoe. Kama ni mke wako, oa huyo mke. Utamaduni usikufunge katika kufanya maamuzi. kumbuka tamaduni zinabadilika na siyo static na zinabadilika kulingana na wakati, teknolojia, miingiliano ya watu na mengineyo mengi. usifanye kitu kwakuwa Babu yako naye alikuwa akifanya hivyo au kwakuwa jirani yako anafanya hivyo.

Mwisho wa siku, MWENYE MAAMUZI ni wewe bi-NAFSI.

Kwaheri kwa sasa.

thanks much, but still in confusion, mada hii ilijaribu kujadiliwa na watu wengi and most of them wanasema the same age sio nzuri simply kwa sababu mwanamke huwa anachoka haraka tofauti na mwanaume, so majority wanapendaa kuoa wanawake wenye umri mdogo ili hata inapofika umri wa mwanamke kuchoka mwanaume nae awe anachoka

nakubaliana na wewe kwamba the only thing that matters is love. ila biological reasons nazo the matters
 
yes they say but on the other side age matters, huwezi ukasema binti wa miaka 25 ameolewa na zee la miaka 60, does it make sense, huyo mzee atakua na uwezo wa kumsatsfy huyo binti? probably atakua anasaidiwa na vijana ambao damu inachemka

asikwambie mtu age aint nothn bt a number.
 
naomba kujuzwa kama umri au age different ni kigezo muhimu katika maisha ya mahusiano au ndoa and if age matters ni miaka mingapi actually mwanaume na mwanamke wanatakiwa kupishana? what about the same age? others says age is just a number

age is not a number.........it defines hormonal imbalances.........................na mnapotofautiana sana ni vigumu kwenda pamoja.......................ingawaje, there are few golden exceptions to this general rule of thumb...............
 
Wife wangu kanizidi miaka kumi lakini mahaba kwa kwenda mbele, siku zinavyosonga ndio mahaba nayo yazidi kukolea. Umri na mahaba wapi na wapi! Havina uhusiano kabisa!
 
Mwanaume as a Kichwa cha Familia kama kuna kosa inabidi sometimes upige mkwara ili kuweka mambo sawa.
Sasa kama unampiga mkwara mkeo halafu ukiangalia age kama ya Maza wako inakua nishai kodogo.
Yaani hata yeye anaweza kua anakusikiliza tu unavyopiga mkwara halafu kimoyomoyo anajisemea tu "huyu Bw. Mdogo vipi huyu!""
 
Mi nadhani age sio ishu sana ila sio mtofautiane sana yani zaidi ya ten years! Mana kuna kuchoka kweli umri ukisogea hata kama
mnapendana!
 
Back
Top Bottom