Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,861
- 1,302
Nimepitia attachments zilizowasilishwa, nyingi ni communication za kawaida kiofisi juu ya jambo hilo. Inaonekana wahusika ni wengi na walijulishwa kuwa bei halisi ni euro 3,098,741.40. Lakini attachment ya 10 'to chief secretary' ndiyo inashtua. Inaonekana kuwepo kwa mikataba miwili mmoja wa official price ya euro 1,032,913.80 na real price ya euro 3,098,741.40. Maana yake kuna bei iliyoonyeshwa rasmi kule italy (official price) na bei iliyoonyeshwa huku TZ (real price); ipi ni halali?
Hapa ndipo serikali ya italy ilipostuka, inaonekana muuzaji alienda kulipa kodi ya serikali ya italy kwa kutumia official price; na baadae (hata kupitia hansard za bunge) ikajulikana kuwa jamaa aliuza kwa real price na hivyo kukwepa kodi. Serikali ya TZ iliafiki ukwepaji huo na ndipo italy walipoibana serikali ya tz kumchukulia hatua Mahalu vinginevyo wao wataichukulia hatua serikali kwa kusaidia ukwepaji kodi. Sakata lilianzia hapo.
Martin Lumbanga baada ya kupewa kimaandishi mikataba miwili tofauti alichukua hatua gani? Kumbuka huyu alikuwa katibu mkuu kiongozi yaani ofisi ya rais wakati huo Mkapa.
Mkapa anaposema mahakamani kuwa hajui kitu hicho cha mabilioni ya pesa wakati katibu wake mkuu alijulishwa, tumweleweje? Nakumbuka kulikuwa na mjadala mkali sana bungeni juu suala hili - ni kwanini Mkapa hakustuka na kumuuliza katibu mkuu wake? au waziri wa mambo ya nje? Nadhani watu wanajaribu kufichiana siri!
Pia ukijikumbusha ushahidi uliokwisha tolewa ofisa wa italy (legal counsel father Marco Papi) anasema alisaini mkataba mmoja tu wa euro 1,032,913.80, (na siyo mikataba miwili) soma hapa: ZoomInfo Cached Page