(Docs): Siri ya Kesi ya Mahalu: Ununuzi wa Jengo la Ubalozi Italia

Nackia huyu ni vice chancelor wa chuo cha bagamoyo,na vice chancelors ni wateule wa raisi,inakuwaje wakati wana bifu??
Kuuma na kupuliza ni tabia kuu ya wanafiki. Wanapenda ukonde saaana na ujifie mwenyewe, hawataki kukugusa ukafia mikononi mwao.

Kama unabisha kamuulize Babu Seya kama kuna kaukweli kokote alikofungiwa ndani maisha pamoja na wanae wote ati kwa baba na wana kusherehekea watoto wa shule kwa ushirika wa pamoja. Halafu hapa JF kumbuka sms iliyodakwa ikimtaka jaji anayesikiliza kesi ya Shamhuna (?) kugombea ubunge wa Ukonga ilisema nini.

Hana wema usimwone kucheka (binadamu) - wimbo wa Muhidin Maalim Ngurumo. Mtendee wema kamwe hatoridhika.
 
Tukubali tukatae mahalu kapiga ile pesa!hilo halina ubishi.kaporomosha jumba masaki balaa baada tu ya lile deal
 
Duh!!! Huyu mkwer.e ana mabifu mabaya sana, nilifikili ni madem tu ndo roho inaingia nyongo kumbe hata huku kwingine... I sure huyu mahalu LAZIMA aende jela, hata kama kwa mwezi mmoja... Hapo roho ya mkwe.re itakuwa nyeupeee kama theruji...
 
Hii kitu watu wamedhulumiana mgao saizi full kubanikana msalabani yetu macho tu!!!!!!!
 
Hapo kwenye RED una uhakika uhakika na hiyo currency yako (Euro)?! Mind you, Euro 1 = 2128 Tshs (kwa exchange rate ya leo), so hapo unazungumzia Trillions of money...Its not TRUE!

Pia kumbuka kuwa at the time of transaction, Exchange rate haikuwa hiyo, mfano tarehe 12/5/2001 exchange rate ilikuwa Euro 1 = 776.316 Tzs, au tarehe 5/3/2005 Exchange rate ilikuwa Euro 1 = 1360.77 Tzs. Hapa kuna time value of money, you have to discount it ten years back.
 
Mbona mnawaya waya issue ni simpo sana.

Kama jengo thamani yake Bilioni X na ubalozi ukaomba bilioni X na mwenye jengo akapewa bilioni X hapo hamna shida kabisaa!

Ila kama jengo thamani yake Billioni X ubalozi ukaomba bilioni Y halafu Mahalu na wenzake (Haijalishi wakina nani) wakalipa X halafu hii Y-X= ikabaki na hawakuirudisha serikalini. Basi Mahalu ana kesi ya kujibu na atuambie alikula hizo hela na kina nani.

Simpo
 
3: Kitendo chake cha kuwakirimu Ubalozini Maaskofu wa Kanisa la Katoliki waliotembelea Italia kilionekana kama kurasimisha UKRISTO wa Ubalozi pale Roma. Tuhuma hizi zipo sambamba na kile alichozusha Shehe na Mnajimu mmoja kwamba Balozi Mahalu ni adui wa Uislamu kwani Balozi Mahalu ndiye aliyetayarisha Memorandum of Understanding (MOU) kati ya Serikali na Kanisa ili Taasisi za Kikristo zilizokuwa chini ya Serikali zirudishwe na kuwa chini ya Kanisa kama ilivyokuwa awali.

Hapa kwakweli alichemsha maana nchi haina dini. Ikumbukwe kuwa huyu ni katika wale mabalozi watiifu wa Kanisa Katoliki hapa nchini. Yeye katika majukumu yake hutekeleza maagizo ya kanisa kwanza halafu ndio anawasikiliza mabosi wake. Waislam kamwe hawatamsahau huyu kutokana na mchango wake kwenye MOU ya kanisa na serikali. Huu ni mwanzo wa laana za wale waliodhulumiwa na watu kama Mahalu. Bado mengi yatamfika. Anastahili adhabu kali sana huyu.
 
Hakuna kesi hapo. Rais ndoo mtendaji mkuu wa serikali na akishasema amesema na JK akijifanya mjanja atajitia kitanzi maana atatakiwa mahakamani kama waziri wa mambo ya nje japo kwenye hansard kupo cristal clear. JK mwenyewe alisema mambo yalienda kama yalivyopangwa. Tatizo Prof. alikuwa anamdharau sana JK akiwa waziri, kwanza alikuwa haendi wizarani yeye ni Ikulu straight na kuna kikao kilifanyika Arusha cha mabalozi wote, Prof. Mahalu alikuwa hafuati ratiba na anachelewa mara nyingi, balozi fulani alimuuliza JK, kuwa mheshimiwa waziri inakuwaje kwa mwenzetu huyu. JK alijibu sina mamlaka nae kwani sikumteua mimi. Akawa ameliweka hilo. ndoo alipoingia Ikulu tu hiyo ikawa one of the pending issue to be delt with urgently.

Kama kweli alikuwa ana tabia hizo hata mimi ningemfunza adabu!
 
Wajameni mimi binafsi ni miongoni mwa Watanzania tunaomuombea kwa Mungu Baba Prof. Mahalu hii kesi itupiliwe mbali!.

Mtu anaweza kufanya mabaya mia na akafanya jema moja, hilo jema likayafuta mabaya yote!.

Miaka ya nyuma wakati nikiwa kijana mdogo nikiishi mitaa ya Ilala, kama kawaida ya watoto wa Ilala, kwao ulaya ilikuwa Italy na ndio mambo yote!.

Nami kwenye kuhangaika na maisha nikatia timu Italy ili na mimi niwin!. Kufika kule nikakuta mambo si mambo!. Ikanibidi kugeika mtoto wa mitaani jijini Rome!.

Siku moja (sikujua kilichonipata mpaka leo) Nilijistukia nimeamkia hospitali fulani hapo Rome ndipo nikaelezwa nililetwa 4 days ago nikiwa unconsious!. Kwa bahati niliposachiwa walinikuta na passport ya Tanzania hivyo wakaniripoti ubalozini.

Ubalozi ulikubali kutake care, uligharimia kila kitu kuhusu matibabu yangu hapo Rome, na baada ya wiki 2, niliruhusiwa kutoka hospitalini nikiwa sina hili wala lile, nikapewa hifadhi nyumbani kwa ofisa mmoja wa ubalozi Bw. Mchemwa, nikafanyiwa mipango nikarudishwa nyumbani Tanzania.

Kikubwa ambacho Mahalu alikifanya ni kuridhia ubalozi kugharimia kila kitu aendapo nisinge amka jumla kwani passport yangu ilionyesha kila kitu kuhusu mimi na katika siku hizo za kupoteza fahamu ndugu zangu walishajulishwa na kuwa tayari kwa lolote!.

Mpaka leo I'm still alive najisikia mimi ni mdeni mkubwa wa Mahalu kuokoa maisha yangu!.

Niliulizia suppose ubalozi wangegoma kusaini hospital bills ingekuwaje?. Niliambia wangeacha nature to take its course na mwili ungeishia kwenye insonereta ya hospital maana hata kupeleka kwenye creametorium ili wafanya creamation ni gharama!.

Naamini Mungu ameisikia sala yangu na labda za wengine kama mimi hivyo Prof. Costa Mahalu atakuwa free!.

Yaani umekuwa kipofu kwa kupewa huduma ya matibabu?

Nani kakwambia kuwa mahalu alitoa pesa zake mfukoni?

Tabia yenu ya kutetea mafisadi kwa kuwa nlipata share zao inaudhi sana!
 
Kwahiyo Mahalu anaonewa kwakuwa MKRISTO MKATOLIKI SAFI!!!!! mwe! Basi mwambieni Pengo akamtetee.
 
i am hitting the ground while running.
Ndugu zangu salamu zangu hizi hapa. Hebu someni attachments hizi muone nani mwongo.
Regards

na hii pia:
re: Yanayozungumzwa ministry of foreign and international affairs (mfaic) na mitaani kuhusu fitna zilizofanywa dhidi ya professor mahalu na kesi anayokabiliwa nayo mahakamani tanzania.
1: Kwamba balozi mahalu alikataa begi lile la “diplomatic bag” lisitumike katika ubebaji wa pesa toka nchi za ulaya mashariki zilizopelekwa ubalozini roma ili zisafirishwe kwenda dar es salaam kwa ajili ya kampeni ya urais ya mwaka 2005.
Inasemekana kwamba balozi mahalu alikataa utumiaji huo wa diplomatic bag kwani haukuwa sahihi. Kwa kuzingatia utaratibu na kanuni yeye alikomolewa kwa kufukuzwa kazi

2: Kwamba balozi mahalu alikataa kushiriki katika njama za kuiba pesa ya watanzania euro billioni 2.4 kwani katika tathmini iliyofanywa na wizara ya ujenzi kuhusu jengo la ubalozi, bei ya jengo hilo lingegharimu euro billioni 5.5 na siyo euro billioni 3.1 bei ambayo ndio bei ya jengo iliyokubaliwa chini ya usimamizi wa balozi katika mchakato wa ununuzi.

Wapo maofisa wa wizara ya nje walioshinikiza serikali inunue jingo lile kwa euro billioni 5.5 kwa kushirikiana na aliyekuwa honorary consul, tanzania consulate ya milano, marehemu avvocato georgio. Uadui na chuki dhidi ya balozi mahalu ulitokana na hilo pia.

3: Kitendo chake cha kuwakirimu ubalozini maaskofu wa kanisa la katoliki waliotembelea italia kilionekana kama kurasimisha ukristo wa ubalozi pale roma. Tuhuma hizi zipo sambamba na kile alichozusha shehe na mnajimu mmoja kwamba balozi mahalu ni adui wa uislamu kwani balozi mahalu ndiye aliyetayarisha memorandum of understanding (mou) kati ya serikali na kanisa ili taasisi za kikristo zilizokuwa chini ya serikali zirudishwe na kuwa chini ya kanisa kama ilivyokuwa awali.

4: Umiliki wa balozi mahalu wa shamba la hekta 500 kandokando ya barabara iendayo bagamoyo haukumfurahisha aliyekuwa bosi wake enzi zile kama waziri wa mfaic. Sasa hivi shamba lote limemegwa na kuwa sehemu ya epz ya bagamoyo.

5: Kama michezo michafu iliyochezwa kwenye majengo ya ubalozi wetu burundi, khartoum na nchi nyingine, balozi mahalu alishitulia njama za kuuzwa kwa jengo la makazi ya balozi pale roma. Njama hizi zilibuniwa na maofisa wa mfaic.

Balozi mahalu alihakikisha kwamba suala la uuzwaji huo kiholela limefikishwa kwenye vyombo vya sheria kule italia na kufanikiwa kurudisha umiliki wa hilo jengo kwa serikali ya tanzania.

Na hapo pia balozi mahalu alijiongezea maadui ambao wamedumu hadi leo.

ahsante sana mzalendo. Ndiyo maana naipenda jf hata kama niko busy kiasi gani lkn jf ni lazima. Wewe umefanya vyema kutoa docs zote, kwani kuna mwenzetu -hutaki unaacha alituletea good docs mara 2 kwa ahadi ya kurejea lkn mpaka leo bado tunasubiri na sasa yapata miezi 4.
 
I am hitting the ground while running.
Ndugu zangu salamu zangu hizi hapa. Hebu someni attachments hizi muone nani mwongo.
Regards

na hii pia:
Re: Yanayozungumzwa Ministry of Foreign and International Affairs (MFAIC) na mitaani kuhusu FITNA zilizofanywa dhidi ya Professor Mahalu na kesi anayokabiliwa nayo mahakamani Tanzania.
1: Kwamba Balozi Mahalu alikataa begi lile la “diplomatic bag” lisitumike katika ubebaji wa PESA toka nchi za Ulaya Mashariki zilizopelekwa Ubalozini Roma ili zisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni ya URAIS ya mwaka 2005.
Inasemekana kwamba Balozi Mahalu alikataa utumiaji huo wa diplomatic bag kwani haukuwa sahihi. Kwa kuzingatia utaratibu na kanuni yeye alikomolewa kwa kufukuzwa kazi

2: Kwamba Balozi Mahalu alikataa kushiriki katika njama za kuiba pesa ya Watanzania Euro billioni 2.4 kwani katika tathmini iliyofanywa na Wizara ya Ujenzi kuhusu Jengo la Ubalozi, bei ya Jengo hilo lingegharimu Euro billioni 5.5 na siyo Euro billioni 3.1 bei ambayo ndio bei ya Jengo iliyokubaliwa chini ya usimamizi wa Balozi katika mchakato wa ununuzi.

Wapo maofisa wa Wizara ya Nje walioshinikiza serikali inunue jingo lile kwa Euro billioni 5.5 kwa kushirikiana na aliyekuwa Honorary Consul, Tanzania Consulate ya Milano, marehemu Avvocato Georgio. Uadui na chuki dhidi ya Balozi Mahalu ulitokana na hilo pia.

3: Kitendo chake cha kuwakirimu Ubalozini Maaskofu wa Kanisa la Katoliki waliotembelea Italia kilionekana kama kurasimisha UKRISTO wa Ubalozi pale Roma. Tuhuma hizi zipo sambamba na kile alichozusha Shehe na Mnajimu mmoja kwamba Balozi Mahalu ni adui wa Uislamu kwani Balozi Mahalu ndiye aliyetayarisha Memorandum of Understanding (MOU) kati ya Serikali na Kanisa ili Taasisi za Kikristo zilizokuwa chini ya Serikali zirudishwe na kuwa chini ya Kanisa kama ilivyokuwa awali.

4: Umiliki wa Balozi Mahalu wa shamba la hekta 500 kandokando ya barabara iendayo Bagamoyo haukumfurahisha aliyekuwa Bosi wake enzi zile kama Waziri wa MFAIC. Sasa hivi shamba lote limemegwa na kuwa sehemu ya EPZ ya Bagamoyo.

5: Kama michezo michafu iliyochezwa kwenye majengo ya Ubalozi wetu Burundi, Khartoum na nchi nyingine, Balozi Mahalu alishitulia NJAMA za kuuzwa kwa jengo la makazi ya Balozi pale Roma. Njama hizi zilibuniwa na maofisa wa MFAIC.

Balozi Mahalu alihakikisha kwamba suala la uuzwaji huo kiholela limefikishwa kwenye vyombo vya sheria kule Italia na kufanikiwa kurudisha umiliki wa hilo jengo kwa serikali ya Tanzania.

Na hapo pia balozi Mahalu alijiongezea MAADUI ambao wamedumu hadi leo.

Mimi naamini lazima kuna walau asilimia 80 ya ukweli kwenye hizi tetesi..ingawa kati ya zote iliyomgusa zaidi mkwe`re itakuwa ni hiyo ya kugoma kuleta pesa ya uchaguzi..hii inadhihirishwa na visasi vyote alivyolipa kwa wale wote waliokuwa kinyume na yeye namna moja au nyingine kuelekea 2005
Ingawa pia mkuu,hizi pesa ni euro million na sio bilioni..asante.
 
kaaaahhh we mzee mahalu kumbe ndo ulivo hivi? yaani ulijiandaa sana..sasa serikali inangoja nini kujitoa kwenye hii kesi....JK visa havitakusaidia
 
Back
Top Bottom