Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Lakini, kutokana na maelezo huyu ndugu hakuwepo shambani, aliyekuwepo ni Mdogo wake mohamed, na aliachwa akilima shambani na treckta, sasa, haya maelezo ya njiani kuelekea hnyumbani aliyapata wapi?

Hii habari mimi nilisikia kulikua na swala la mahusiano ya kimapenzi kati ya....... na......
 
Hii habari niliisikia toka siku nyingi. Kilichonifurahisha zaidi ni kuwa kumbe kulikuwa na personal conflict kati yao. Hakika binadamu huwa tunafanya maamuzi tofauti tukiwa na wapendwa.
 
Inapatikana wapi hiyo sehemu ya pili ya kisa hiki?

Je, Kwanini Mwamwindi Alimpiga Risasi Kleruu? Nimefanya Mahojiano Na Mtoto Wa Mwamwindi (2)



Kleruu akamwuliza Mzee kwa ukali, " Mbona mnafanya kazi leo siku ya Krismasi?". Baba akamwomba Kleruu waende wakuzungumze nyumbani. Akamwambia mdogo wangu Mohammed aendelee kulima. Mzee akatangulia mbele, nyuma anamfuatia Kleruu. Kabla ya kufika kwenye nyumba yake wakayapita makaburi. Kleruu akamtamkia baba mzee Mwamwindi; " Hapa ndipo unapozika mirija yako?" Alitamka hivyo huku akimtomasa tomasa mzee na kifimbo alichoshika mkononi.

Jambo hilo lilizidi kumkasirisha marehemu mzee. Akafika nyumbani kwake. Mlangoni alisimama mke wake mdogo. Inaonekana mzee alishafanya uamuzi. Jana yake alikwenda kuwinda. Hakupata mnyama. Bunduki yake moja aia ya riffle kati ya bunduki zake mbili ilikuwa bado ina risasi. Akamwambia mke wake mdogo huku Kleruu akiwa anasikia;
" Kanichukulie bunduki yangu"…… Endelea…


" Je, aliposikia hayo Dr Kleruu alifanyaje?"

" Nadhani alipigwa na butwaa. Hakuamini kama baba angefikia hatua hiyo"

"Na ilikuwaje basi Mwamwindi alipoletewa bunduki?"

" Ilienda haraka, Mzee Mwamwindi akainua bunduki yake. Tayari ilikuwa loaded na risasa tangu jana yake alipotoka kuwinda. Kleruu aliinua mikono yote miwili kama mtu anayesalimu amri. Mwamwindi akampiga risasi ya kwapani. Kleruu akabaki hai. Akapiga risasi nyingine. Ikamwua pale pale." Anasimulia Mzee Amani Mwamwindi.

Kinafuatia kimya. Anainama, namwona usoni, kuwa huzuni imemjia. Bila shaka, ni kitendo kile cha baba yake kumpiga risasi na kumwua Dr Kleruu ndicho kilichoashiria mwanzo wa ukurasa mgumu katika familia ya Mwamwindi , Isimani na pengine Iringa kwa ujumla.

Nafikiria kumwuliza swali lifuatalo; Risasi ya pili ya Mzee Mwamwindi ilimpiga Dr Kleruu katika sehemu gani ya mwili? Nasitisha swali hilo. Litasubiri mara nyingine. Mzee Amani Mwamwindi anaendelea kunisimulia;

" Mdogo wangu Mohammed akiwa shambani alisikia mlio wa bunduki. Alidhani kuwa baba amepigwa risasi. Alikimbia kurudi nyumbani. Na pale ilipowekwa kumbukumbu ya Kleruu nyuma yake ndio ilipokuwa nyumba ya mzee. Hivyo, pale ulipowekwa mnara ni mbele ya nyumba. Kwa sasa nyumba hiyo haipo.

Alipofika nyumbani, Mohammed akamkuta baba amesimama, na Kleruu amelala chini, amekufa. Mzee alichukua kofia ya pama ya Kleruu, akaivaa. Akaingiza mkono mifukoni mwa Kleruu, akachukua funguo za gari la Kleruu. Mzee alimwambia mdogo wangu amsaidie kumwinua Dr Kleruu. Mzee alimshika miguuni na mdogo wangu Mohammed alimshika kwenye mikono. Wakamwingiza kwenye buti la gari.

Baba akaendesha mwenyewe gari lile la Mkuu wa Mkoa Kleruu, Peogeot Injection, rangi ya bluu likiwa linapepea bendera ya taifa. Aliendesha kuelekea mjini Iringa. Njiani kuna walioshangaa kumwona Mwamwindi akiendesha gari la Mkuu wa Mkoa huku akiwa kichwani amevalia pama la Kleruu.

Mzee alipoingia mjini Iringa breki ya kwanza ilikuwa hapa tulipo, nyumbani kwangu Mlandege. Kama nilivyosema, wakati huo nilikuwa kijana wa miaka 21. Nilishakuwa na mji wangu, nilijenga kibanda changu hapa tulipo. Nilifanya kazi kama karani wa Ushirika. Siku ile ya tukio nami nilikwenda kwenye shamba langu Ifunda.
Basi, Mzee alipofika hapa nyumbani akaambiwa kuwa nimekwenda shamba Ifunda. Alisikitika sana." Anasema Mzee Mwamwindi huku naye bado akionyesha huzuni machoni. Miaka 40 baada ya tukio.


Alipotoka hapa alipita nyumbani kwake pale Mshindo, na baadae akasimama kwa binamu yake. Ile nyumba ya njano nyuma ya benki ya CRDB, si unaijua?" Ananiuliza.

" Ndiyo" Namjibu.
" Pale alikuwa anakaa binamu yake na baba. Basi, alipofika pale akakutana n abinamu yake. Binamu yake yule alishangaa kumwona mzee akiwa na damu kwenye nguo zake. Akashangaa pia kumwona akiwa na gari la Kleruu lenye bendera ya taifa ikipepea. Akamwuliza nini kimetokea? Mzee hakuweza kuongea akaeleweka. Alitamka; " Nimeenda kwa Amani ( Mimi) nimeambiwa kaenda shambani kwake Ifunda". Alionekana kuchanganyikiwa.

Akaingia kwenye gari. Akaendesha moja kwa moja hadi Kituo cha polisi. Akamkuta polisi kijana. Akashuka, akamwambia; " Njoo chukua mzigo wako". Akaweka chini pia kofia ya pama ya Kleruu.

Polisi alipofungua buti ya gari akashangaa kuona mzigo wenyewe ni mwili wa Mkuu wa Mkoa, Dr Kleruu. Mzee akawa amejisalimisha.

Niliporudi nyumbani kutoka Ifunda nikazikuta habari hizo mbaya. Nikaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Mzee pale Mshindo. Nikawakuta akina mama wanalia. Ilikuwa ni kilio. Hiyo bado ilikuwa ni Jumamosi, siku ya Krismasi. Nikauliza; kuna aliyekwenda kumwona baba pale polisi? Jibu likawa hapana. Nikaenda moja kwa moja polisi ili nikamwone baba na nimsikie kauli yake.

Nilipofika polisi nikaanza kujieleza kwa askari polisi kuomba ruhusa ya kuongea na Mzee. Wakati nikifanya hivyo mzee nae alisikia sauti yangu. Akatamka; " Mwanangu huyo, mruhusu niongee nae". Nikaongea na Mzee.
 
kweli inasikitisha lakini maamuzi magumu yanaitajika asa kwa kipindi hiki cha mafisadi kujilimbikizia mali
 
"Niliweza kuongea na Mzee na kupata picha ya kilichotokea. Niliondoka kurudi nyumbani. Habari zilishasambaa. Hali haikuwa nzuri. Mji wa Iringa ulitulia sana. Halafu ukaja mtikisiko mkubwa. Wazee wengi walioishi mjini na waliokuwa wakilima na Mzee kule Isimani walisombwa na vyombo vya usalama."

Je, ni kina nani hao? Namwuliza Amani Mwamwindi.

"Mzee kama Ibrahim Khalili, Mursali na wengine. Watu kama 30 hivi walisombwa na kupelekwa sehemu mbali mbali za nchi. Kuna waliopelekwa Mwanza, Shinyanga hata Zanzibar. Kwa namna fulani walitenganishwa katika sehemu hizo."

Je, na wewe ulikumbwa na msukosuko huo?

"Ndio, hata mimi nilihojiwa ingawa niliachwa niendelee na kazi zangu. Kumbuka nilikuwa kijana wa miaka 21 tu, na siku ya tukio nilikuwa shambani kwangu Ifunda. Hapa nyumbani kwangu kulikuwa na askari wa FFU muda wote. Katika kuhojiwa kwangu maswali mengine yalikuwa hayana msingi.

Kwa mfano, niliulizwa; Mzee alipokuja hapa kwako kutoka Isimani siku ya tukio alitaka kukwambia nini? Sasa ,mimi hakunikuta nyumbani na hatukuongea, nitajuaje alichotaka kuniambia siku hiyo?! Anaongea Amani Mwamwindi akionyesha kushangaa, hata hii leo.

Je, kwa wakati huo, wewe na familia yenu mlihisi kutengwa na jamii kutokana na kitendo alichofanya Mzee Mwamwindi? Namwuliza. Namwona Amani Mwamwindi akionyesha kuguswa sana na swali hili.


" Tulikuwa na wakati mgumu sana kama familia. Kibaya zaidi kwetu ilikuwa ni kuingia kwenye uhasama na ndugu wa jamaa ambao wazee wao walisombwa na vyombo vya usalama na kwenda kusikojulikana. Kwao waliamini kama isingekuwa Mzee wetu Mwamwindi kufanya tendo lile, basi, wazee wao wangebaki salama na kuendelea na shughuli zao za kilimo. Hivyo basi tulisakamwa na wengine ambao ni ndugu zetu."

Mlifanyaje kuikabiili hali hiyo?


"Tulifikia uamuzi mimi niende Dodoma kwenye gereza alikokuwa Mzee Mwamwindi. Niende nikamjulishe baba juu ya hali iliyotokea huku nyumbani. Kwamba tuna uhasama na jamaa wa waliosombwa na vyombo vya dola.

Nilipata kibali cha DC hapa Iringa. Kibali cha kwenda kumwona Mzee kule Dodoma. Nilipofika Dodoma nikaonana nae. Tukazungumza. Nikamwambia shida ya nyumbani. Alisikitika sana. Akaniuliza; " Sasa tufanyeje?". Nikamshauri aandike barua kwenda kwa Nyerere kumwomba atusaidie. Baba aliandika barua siku hiyo hiyo. Alimwandikia Nyerere kumwambia na kumhakikishia kuwa ni yeye Said Mwamwindi na si mtu mwingine ye yote aliyehusika na tendo alilofanya; kumpiga risasi na kumwua Kleruu.
Barua ile ilifika kwa Nyerere, na haukupita muda mrefu, wazee wale wakulima wa Isimani waliachiwa huru na kurudishwa Iringa. "

Je, hali ya mahusiano na waliowachukia ilibadilika na kuwa njema baada ya wazee hao kurudi Iringa? Namwuliza Mzee Amani Mwamwindi.


" Ndio, kabisa. Hali ikawa shwari. "

Je, wazee wale wakulima wa Isimani walirudi na kuendelea na kazi zao za kilimo?


" Niseme kuwa walirudi Iringa wakiwa wameathirika kisaikolojia. Kuna ambao hawakutaka kabisa kurudi tena Isimani. Baadhi yao hawakuishi muda mrefu, walifariki. Sijui nini kiliwatokea."


Je, unafikiri Iringa ingekuwaje kama tukio lile la siku ya Krismasi mwaka 1971 lisingetokea?

" Naamini kabisa, Iringa isingekuwa kama ilivyo sasa. Ingeendelea sana. Unajua kulikuwa hakuna mahala pengine katika nchi hii ambapo kulikuwa kunazalishwa mahindi kushinda Isimani. Mzee na wenzake walilima ekari nyingi sana. Naamini wangelima zaidi. Walianza kujijenga na hata waliunda ushirika wao. Tukio lile lilisimamisha kasi ya kilimo Isimani. Ni kama laana fulani vile, maana, tangu wakati ule mvua zimekuwa za tabu Isimani." Anasema Mzee Amani Mwamwindi. Kisha namwuliza tena.

" Nilifika pale nyumbani kwenu Isimani, nikaona mnara wa kumbukumbu ya Dr Kleruu, kwanza nilifikiri ni kumbukumbu ya Mwamwindi. Je, unajisikiaje kuona nyumbani kwenu kuna mnara wa kumbukumbu ya Dr Kleruu na si ya baba yenu?" .


" Mimi naona ni sawa kabisa kwa mnara ule kuwa pale". Ananijibu Mzee Amani Mwamwindi huku akionyesha kuchangamka. Anaendelea.

"Unajua hata Nyerere alipofika Isimani wakati fulani aliuliza; " Hivi huu mnara ni wa kumbukumbu ya Dr Kleruu au Said Mwamwindi?" Nyerere alikuwa na maana yake." Ananiambia Mzee Amani Mwamwindi. Kuna kitu anataka kufafanua, anasita. Namwacha aendelee kutafakari.


Kisha ananiuliza swali gumu. Nabaini ni mara ya kwanza katika mazungumzo yetu ameamua kunirushia swali. Kwa mtazamo wangu ni swali la kifalsafa. Mzee Amani Mwamwindi ananiuliza;

" Bwana Mjengwa, mche unaochipua ardhini unahitaji kumwagiliwa maji ili uendelee kuchipua. Ukisimama vema unauacha ukue wenyewe. Na je, ukishakua na kukomaa unaufanyaje?". Mzee Amani Mwamwindi ananiuliza huku akinitazama usoni.


Naam, ni swali gumu lenye kunihitaji, sio tu kufikiri, bali kufikiri kwa bidii. Jibu lake lazima lifuatiwe na majadala.

Ewe msomaji mpendwa, kabla sijaingia kwenye nilichomjibu Mzee Amani Mwamwindi na mwendelezo wa mazungumzo yetu nakutoa nje ya nyumba ya Amani Mwamwindi pale Mlandege.
Maana, mpaka kufikia hapa tumemsikia Mzee Amani Mwamwindi, kama mwanafamilia ya marehemu Said Mwamwindi akisimulia kilichotokea.

Iringa Mjini kuna mmoja wa wazee wa siku nyingi, Mzee Omar Mselem Nzowa. Huyu ni mmoja wa wazee walionipokea nilipofika Iringa miaka sita iliyopita. Mzee Nzowa alimfahamu marehemu Said Mwamwindi, baba wa Amani Mwamwindi . Jumamosi moja ya mwezi Novemba, 2010 naamua kwenda nyumbani kwa Mzee Nzowa.


Tumekaa sebuleni, mimi na Mzee Nzowa. Tunaongea huku tukipata kikombe cha chai.

" Ndio Mzee wangu, nisimulie habari za Marehemu Said Mwamwindi, maana nimekutana na mwanae , Amani Mwamwindi, naye kuna aliyonisimulia. Je, ulipata kukutana na marehemu Said Mwamwindi wakati wa uhai wake?"

" Aah! Said Mwamwindi, nilimfahamu sana." Ananiambia huku anacheka. Kisha anaendelea kusema;

" Unajua, tulikua nae hapa mjini. Na hata siku ile ya tukio mimi na vijana wenzangu wa wakati ule tulikuwa tunacheza bao pale Miyomboni, tulishangaa sana kumwona Said amesimamisha gari la Dr Kleruu nyumbani kwa shangazi yake na huku amevalia pama la Dr Kleruu.

Nakumbuka alitunyoshea mkono akiwa anatabasamu. Tulizungumza kwa kushangaa, tukajiuliza; jamani hivi Serikali leo imempa Said Mwamwindi gari atembelee? Yakafuata yaliyofuatia. Maggid, ninayo mengi ya kukusimulia kwa yaliyotokea katika wakati ule…." Anasema Mzee Nzowa. ( Simulizi hii itaendelea.)
 
bado sijapata picha, huyu RC aliuawa kwa sababu eti alimwambia Mwamwindi anafanya kazi siku ya krismasi? Only that?
 
Sababu siyo hiyo, kulikuwa na mengine mengi ambayo hatuna uhakika kama yalikuwa ni kweli au tetesi.

Mfano, inasemekana huyu RC alikuwa anamfuatilia mke mdogo wa Kleruu na ndiyo mzee akachukia kweli kweeli.
 
Mzee Amani amesimulia vizuri hadithi ya kifo cha Dr.Wilbert Kleruu (Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa) kwa kupigwa risasi mbili na Baba yake mzazi mzee Said Mwamwindi,hadithi hii tumewahi kuisikia kwenye version nyingi tofauti,lakini mahojiano ya Bwana Mjengwa yametoa picha nzuri na kupunguza maswali mengi,Swala la msingi ambalo Mzee Amani hakulizungumzia ni kwamba Mzee Kleruu alifanya nini alimpomsikia Mzee Mwamwindi anamuagiza mkewe akalete bunduki? hakuhisi kuwa anataka kuuliwa? alikuwa na bastola kiunoni hakujaribu kujihami?Vinginevyo hadithi ni nzuri na ambayo imefungua Historia hiyo ya mauaji ya kinyama aliyofanyiwa Msomi na kiongozi yule aliyeaminiwa sana na Mwalimu Nyerere.Dr Kleruu alikuwa na PHD ya kilimo aliyosomea United States na alizikwa kwao Kilimanjaro.
 
Mzee Amani amesimulia vizuri hadithi ya kifo cha Dr.Wilbert Kleruu (Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa) kwa kupigwa risasi mbili na Baba yake mzazi mzee Said Mwamwindi,hadithi hii tumewahi kuisikia kwenye version nyingi tofauti,lakini mahojiano ya Bwana Mjengwa yametoa picha nzuri na kupunguza maswali mengi,Swala la msingi ambalo Mzee Amani hakulizungumzia ni kwamba Mzee Kleruu alifanya nini alimpomsikia Mzee Mwamwindi anamuagiza mkewe akalete bunduki? hakuhisi kuwa anataka kuuliwa? alikuwa na bastola kiunoni hakujaribu kujihami?Vinginevyo hadithi ni nzuri na ambayo imefungua Historia hiyo ya mauaji ya kinyama aliyofanyiwa Msomi na kiongozi yule aliyeaminiwa sana na Mwalimu Nyerere.Dr Kleruu alikuwa na PHD ya kilimo aliyosomea United States na alizikwa kwao Kilimanjaro.
miaka hiyo phd? huyomzee kleruu alikuwa noma sana :)
 
Huyu alitandikwa risasi na shujaa Saidi Mwamwindi, toa na sababu zilizompeleka kutandikwa risasi, alikuwa fedhuli na alilewa madaraka.

Kwa nini kusema kweli inakuwa ngumu kwako?
 
Huyu alitandikwa risasi na shujaa Saidi Mwamwindi, toa na sababu zilizompeleka kutandikwa risasi, alikuwa fedhuli na alilewa madaraka.

Kwa nini kusema kweli inakuwa ngumu kwako?

Ukweli wake ni uongo kwako na
uongo wako ni uongo kwa kila mtanzania mwenye akili timamu
 
Huyu alitandikwa risasi na shujaa Saidi Mwamwindi, toa na sababu zilizompeleka kutandikwa risasi, alikuwa fedhuli na alilewa madaraka.Kwa nini kusema kweli inakuwa ngumu kwako?
sasa kama unazijua sababu za kutandikwa risasi kwanini usiziseme!?
 
dr kleruu kiukweli mi sina shida na maandiko ya juha kama huyu, na bora aliuwawa maana alikuwa dikteta haswa, viva mwamwindi.

Nina hakika kama ningelikuwa kwenye position ya Mwamwindi, nisingemwacha Kleruu arudi salama, ningelifanya the same..., nampongeza sana Mwamwindi kwa uamuzi alioufanya, viongozi Madikteta kama Kleruu hawana moral authority ya kuzungumzia demokrasia na alistahili kufanyiwa alichofanyiwa na kuzidi...

Lala salama Mwamwindi...
 
Huyu jamaa hakua kichaa ,huyu alikua mzima kabisa na binadamu mwenye akili timamu ndivyo anavyopaswa kubehave.

Vichaa ni kizazi hiki chetu maana MAFISADI tunayasema hapa sana kwenye screen lakini ukikutana naye live TUNACHEKA kicheko kwa kuonyesha meno yote hahahahahahahahaha Mheshimiwa .
Kweli ndugu
 
Mwawado,

Pia Mwl baada ya kung'atuka mwaka 1985 alipohojiwa na BBC kwamba "katika kipindi cha uongozi wake kuna mambo mazuri na pengine mabaya aliyoyafanya" Mwl hakusita kuzungumzia kwamba anajutia kusaini adhabu ya kifo cha Mwamwindi. Hivyo bila shaka alitibu na kusamehewa na Mwenyezi Mungu. Ni mapungufu ya kibinadamu.
 
sasa kama unazijua sababu za kutandikwa risasi kwanini usiziseme!?

Aliyeanzisha ile nyuzi iliyochakachuliwa na hii post kuwekwa huku ndio hii post ilikuwa directed kwake, kama anaijuwa historia ya kleruu kwa nini hajatoa na sababu zilizofanya atandikwe risasi?

Kwa kuongezea tu, baada ya kumtandika risasi kleruu Mwamwindi akawaambia waliokuja nae "haya bebeni nguruwe wenu muondoke nae".

Mwambieni ayahadithie yote yaliyopelekea kleruu kutandikwa risasi na kisha wenzake kuambiwa "bebeni nguruwe wenu"!

Historia inapoandikwa iandikwe kwa pande zake zote kama ilivyo, kuchakachuwa haisaidii watu waisomao kujirekebisha au kuji"enhance", inapopindwa hupelekea watu kurudia makosa yale yale yaliyofanywa na yoyote awae.
 
Naomba kuweka swali lanyongeza hii inayoitwa Historia ya Tanzania imeanza lini Rasmi naoma kuelimishwa na kabla ya hapo ni kipi tunaweza kukiongelea naomba mchango utakao elimisha wengine kama mie ambao tumekuwa katika mashaka na historia yetu kwani miaka siomingi tangia kuzaliwa kwa Tanzania sasa kabla ya hapo nini kilikuwa

April 1964
 
Back
Top Bottom