Dkt. Tulia awasha moto Mbeya Mjini, awafundisha wananchi masuala ya kisheria hadharani na kusoma maamuzi ya Mahakama

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Mbeya kumenoga, kumekucha, kumependeza, kumepembazuka, kumechanua, kunavutia, kunaleta hamasa, matumaini, faraja, Tabasamu na furaha. Hii ni kutokana na ziara inayoendelea kufanywa na Dada msomi,Nguli wa sheria,mwamba wa Mbeya, chuma cha Reli,Fahari ya Mbeya Na Tumaini la wana nyanda za juu kusini mh Dkt Tulia Acksoni mwansasu.

Ameendelea kuuwasha moto na kutikisa viunga vya jiji la Mbeya na maeneo ya jirani. Ameendelea kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya wana Mbeya na yake ya kitaifa, ameendelea kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayogusa hisia za watanzania wengi.

Na kwa kipindi hiki akiwa jukwaani ,akiwa imara,mwenye bashasha,furaha, Tabasamu na mwenye kujiamini ametoa Darasa la sheria hadharani juu ya uwekezaji wa Bandarini,amefafanua masuala ya kisheria juu ya vifungu mbalimbali na kueleza hoja kwa hoja juu ya vifungu na mambo ambayo yamekuwa yakipotoshwa na watu wenye nia ovu.

Kwa utulivu, upole na unyenyekevu amewatoa hofu wana Mbeya juu ya uwekezaji huo.Na katika kuwaelimisha zaidi akafikia hatua ya kusoma maamuzi ya mahakama yaliyotupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa mkoani Mbeya ikipinga uwekezaji huo,japo waliokuwa wameifungua walionyesha uwezo mdogo wa kisheria na ujenzi wa hoja katika kuishawishi mahakama,hali iliyopelekea kutupiliwa mbali kwa kesi yao isiyo na mashiko.

Nguli huyu wa sheria huku akiendelea kushangiliwa na kupigiwa makofi kila muda alipoongea katika kata ya itigi mkoani Mbeya, alifafanua masuala mbalimbali huku akiwaasa wana Mbeya kujiepusha na kutowaunga mkono watu wanaotaka kupandikiza mbegu za ubaguzi kwa misingi ya ukabila, Dini na ukanda. Alitoa Rai kwa wana Mbeya kuendelea kumuunga mkono Mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan pamoja na serikali yake, huku akieleza mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na itakayotekelezwa na serikali yao ikiwepo ujenzi wa barabara za njia nne kutoka igawa mpaka Tunduma zenye urefu wa km zaidi ya 218.

Wana Mbeya kwa hakika wamepata zawadi ya kipekee sana kuwa na Dr Tulia ndani ya jiji la Mbeya. Hii ni Bahati, neema na baraka kwa wana Mbeya, kwani ni kupitia yeye tumeona namna yatima, wajane, wazee na vijana wakisaidiwa na kuwezeshwa, tumeona ni kupitia mikono yake ma miradi ya mabilioni yakiendelea kutekelezwa mkoani Mbeya,tumeona kupitia uwepo wake mkoani Mbeya jiji likipewa hadhi yake ya kiuwekezaji kutoka serikalini.

Sasa Mbeya ina meremeta na kumekameka, sasa wana Mbeya ni kama wote ni wana sheria wanaosubiri kutunukiwa vyeti vya mafunzo ya sheria baada ya kila mara na wakati wote kupewa darasa la sheria bure kutoka kwa mwalimu na Daktari wa sheria Dkt. Tulia Ackson mwansasu mwalimu wa walimu wa sheria ,wakili wa mawakili wasomi. Hakuna kama Tulia mkoani Mbeya kwa sasa na hakuna mwenye ubavu wa kushindana na Dr Tulia katika sanduku la kura.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Tulia! Nani huyu? Huyu ambaye degree zote za pichu! Ukimuona amefungua mdomo kama pango na huko chini kumeachama tu! Huyu asome asisome ni kilaza tu
Huna akili na naona itakuwa ni mgonjwa wa akili uliyeshika simu kwa bahati mbaya , nitashangaa usipochukuliwa hatua na moderator
 
kosa lipi? kwani hakuna ukweli hapo! au wewe ni dalali wa bandari zetu! na kuwabambikia nduguzo uhaini wakanyongwe!
Bandari ipi iliyo dalaliwa? Hao wachochezi ni lazima wafundishwe adabu na kutii sheria.lazima wafundishwe kuwa uhuru una mipaka yake na kabla ya kuongea unapaswa kupima kauli zako na siyo kujiropokea tu.
 
Bandari ipi iliyo dalaliwa? Hao wachochezi ni lazima wafundishwe adabu na kutii sheria.lazima wafundishwe kuwa uhuru una mipaka yake na kabla ya kuongea unapaswa kupima kauli zako na siyo kujiropokea tu.
Kumbe wee mtumwa mzoefu hujui hata maana ya Uhuru. Kwa hiyo kuwafuga wenzio kamba wale kwenye uzio wa nyumba yako ndiyo uhuru huo? Hivi bado unaliona lile dude linaloitwa sijui makubaliano sijui mkataba ni mkataba wa manufaa? Ule ni mkataba wa utumwa rasmi. Wote wanaoushabikia ni madalali tu! Tuna miaka millioni kutoka hapa tulipo for sure!
 
Back
Top Bottom