Dkt. Ndugulile: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, siungi Mkono kupita bila kupingwa

Makonda alipata kura nyingi kuliko Ndugulile ila Shujaa Magufuli akavuta waya na kuagiza Faustine awe namba 1 😂🔥

Hata yeye anajua hili
Kikwete ndiye akimuombea kwa Magufuli kuwa muonee huruma kafiwa mpe ubunge kufuta machozi

Hana lolote tena alishindwa vibaya sana
 
"Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, haiwezekani wagombea wa upinzani tu ndio hawakujua kujaza fomu ipasavyo halafu wagombea wa CCM wakaweza kujaza fomu ipasavyo kila mahali” Dkt. Faustine Ndugulile.

Ndugulile amesema haungi mkono suala la wagombea kupita bila kupingwa “Mtu kama unajiamini kwa nini upite pasipo ushindani..?”

Hata hivyo Ndugulile amesema alikuwa na uhakika wa kuwashinda wapinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda, ambaye kwa sasa ni katibu muenezi wa CCM Taifa.

“Mimi sijawai kuwa na uchaguzi rahisi kigamboni na uwa sipendi uchaguzi mwepesi, hata 2015 niligombea na vigogo wengi akiwemo mtoto wa Rais Mkapa lakini nilishinda” Ndugulile.

Mungu anisamehe ila HAKUNA MWANASIASA MPUUZI KULIKO UPUUZI WA CCM KAMA HUYU NDUGULILE.
Mpuuzi sana.
 
"Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, haiwezekani wagombea wa upinzani tu ndio hawakujua kujaza fomu ipasavyo halafu wagombea wa CCM wakaweza kujaza fomu ipasavyo kila mahali” Dkt. Faustine Ndugulile.

Ndugulile amesema haungi mkono suala la wagombea kupita bila kupingwa “Mtu kama unajiamini kwa nini upite pasipo ushindani..?”

Hata hivyo Ndugulile amesema alikuwa na uhakika wa kuwashinda wapinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda, ambaye kwa sasa ni katibu muenezi wa CCM Taifa.

“Mimi sijawai kuwa na uchaguzi rahisi kigamboni na uwa sipendi uchaguzi mwepesi, hata 2015 niligombea na vigogo wengi akiwemo mtoto wa Rais Mkapa lakini nilishinda” Ndugulile.

Huyu naye ni mtafuta kick tu ya kukubaliwa na waliochukua CCM sasa. Mbona hakupinga wakati huo.

Swala la wagombea kupita bila kupingwa limekuwapo tangu tupate uhuru, halikuanza majuzi tu. Amil Jamal alikuwa Mbunge wa Morogoro kwa muda mrefu sana akiwa anapita bila kupingwa. Baada ya vyama vingi na kuhitaji kila mgombea awe amesimamishwa na chama cya siasa, kuna majimbo mengi sana mwaka 1995 yalichukuliwa na CCM bila kupingwa kwa sababu vyama vya upinzani havikusimamisha wagombea.

Kilichotokea mwaka 2020 ni kwamba kuna majimbo ambayo ama vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea walioenguliwa kwa sababu yeyote ile au havikutoa mgombea kabisa. Nape na Majaliwa ni kai ya waCCM waliopita bila kupingwa kwa sabababu majimbo yao hayakuwa na wagombea wa vyama vya upinzani. Angepinga jinsi wagombea wa upinzani walivyoenguliwa siyo kupinga kitendo cha mgombea wa CCM kupita bila kupingwa wakati ndio utaratibu uliokuwapo miaka yote hiyo.

Sheria ya Uchaguzi inatakiwa marekebisho sana lakini huyu naye asitake kutafuta kukubaliwa na kundi lilipo sasa hivi kwa kukandia uchaguzi ambao yeye mwenye alishiriki na kukubali matokeo yake.
 
Sawa Magu aliagiza uchafuzi ila mbona bi. Mkubwa anapigiwa promo zile zile kwamba 2025 hamna mwengine isipokuwa yeye tu. Hilo sio dosari kweli?
 
Huyu ye mwenyew watu wa kigamboni tushamchoka..! Tangu naanza kujielewa si chini ya miaka 10+ nasikia yeye ni mbunge wa huku kigamboni! lakin kila siku kigambon ipo vilevile
Yaani huyu mbunge ni mzigo kuliko wabunge wote wa majimbo niliyoishi. Bogus MP.
 
Magu alisimamia msimamo kuwa kama kakupa nafasi kisha ukajitia tamaa kugombea nafasi nyingine haupati.

Faustine anajitia kiburi tu..ila 2025 atamkumbuka Magu..pale wajumbe watakapomuambia bila millioni 00 asijisumbue kugombea..
Hahahah kipindi cha wajumbe kupiga hela kimewadia. Bila 200M asishobokee form kabisa😂
 
Wasimamizi wanaeleezwa mshindi ni nani bila kujali idadi ya kura alizopata. Tabia hiyo ikiendelea, tunakaribisha majanga, sawa tuliyoyaona 2020 baada ya uchaguzi wa Magu.
 
Back
Top Bottom