akajasembamba
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 1,012
- 1,477
Hayo mapigo yatajibiwa wapi ITV au Chanell Ten? Labda BBC au CNN! Sijui kama watapewa nafasi ya kuonyesha the other side of the story, freedom of press bado, its flag independence
Nisichokubaliana na baadhi yenu humu ni hili la WATANZANIA kufa kwa malengo ya KISIASA kama ilivyotokea Arusha na kabla ya hapo Pemba. Hakuna kifo kinachokubalika lakini hili la vifo vya kisiasa halina TIJA wala maana yoyote kwa Mtanzania wa kawaida. Ni afadhali Mtanzania afe kwa kudai AJIRA, kulalamikia bei ya kilo ya unga, bei ya mkate, bei ya umeme, bei ya maji, karo kubwa za shule, huduma mbaya za elimu kwenye mashule ya UMMA na mambo yanayofanana na hayo.
Tusiendelee kuua watu wetu kwa malengo ya KISIASA ambayo hayawabadilishii lolote watu wetu. Wakati wa kampeni, Dr Slaa alisisitiza mara kwa mara juu ya kutomwaga damu ya Watanzania ili aende IKULU. Ni nini kinafanyika sasa?
Chama chenye nguvu ya Umma,na kinachoitesa CCM usiku na mchana,Kinachofahamika kwa jina la CHADEMA.
Kipo mbioni katika hatua za mwisho kuonyesha tukio zima la Mauaji ya Arusha lilivyo tekelezwa na Polisi wenye dhama ya kulinda amani.Mkanda huo utaonyeshwa kwenye runinga live,ikiwa ni kulaani kitendo cha TBC-1 kuchakachua ukweli wa tukio kwa kuonyesha vipande baadhi vya tukio zima,huku vipande hivyo vikiegemea kuisafisha serikali dhalimu ya JK.
Mkanda upo makao makuu ya chama,kilicho baki ni Logistics za kuuonyesha.
"Nasema uma ni lazima ujue ukweli na sio kupotoshwa na baadhi ya vyombo na watu kwa maslahi yao'
source.Tanzania Daima tar.18/1/2011.
Wa u upload on line kwenye You Tube ili dunia ione.
walete tuwaone ! hivi na wakwao wanaweza hata kudhubutu kuurusha kwenye yutubu? Wataumbuka maana hatakama wamechakachua bado wao ndo wamepiga risasi aliye ua ni polisi hatakam watsema eti walitaka kuteka kituo cha polisi! je wlikuwa na silaha ? Hata wakipambana na mwizi wanaruhusiwa kumpiga mguu siyo kuua !Wa u upload on line kwenye You Tube ili dunia ione.
Nimesuggest mara nyingi kuhusu hii issue siziuzwe wazigawe bure kama karanga