Dk. Slaa: Tutajibu mapigo

Hayo mapigo yatajibiwa wapi ITV au Chanell Ten? Labda BBC au CNN! Sijui kama watapewa nafasi ya kuonyesha the other side of the story, freedom of press bado, its flag independence
 
Naishauri Serikali ya CCM, CCM na Chadema wakae wayazungumze watafute muafaka kuhusu tukio la Arusha. Hoja inayozungumziwa inajaribu kuonyesha kuwa Chadema na Serikali wote walikuwa sahihi kwa mujibu wa sheria za nchi. Lakini mjadala huu unavyokwenda Raisi kikwete asipokuwa makini na kuamua yeye mwenyewe kuingilia kati basi wao ndo watapata hasara kubwa zaidi.

Sababu ni kuwa huwezi kuitenganisha Serikali na CCM kwa kuwa Rais ndo mwenyekiti wa chama. Serikali ikipoteza hadhi yake kwenye jamii, na chama nacho kinaanguka kwa kuwa wananchi watakosa imani nayo. Ni suala dogo tu la kujiuliza, wangeruhusu maandamano na mkutano ule wakaulinda kwa nguvu zilezile walizotumia kuyasambaratisha leo tungekuwa tumeshasahau hata yale yaliyotokea. Hata kama chadema ingekuwa haina umaarufu wowote, tukio la Arusha tayari limeshawanufaisha kisiasa
 
@ Dr. Slaa....

Nilishauri hizi DVD zitengenezwe ili mzigawe bure... sababu ni vigumu kwa vyombo vya habari kuonyesha since the are not fair... na mtu wa kawaida ni vigumu kununua sababu ya watu kutokujihusisha na siasa wapo radhi wakanywe lager kuliko kuangalia matukio haya...

Pia kuna tubes online za bure kama youtube kwanini chadema msifungue account pale na muwe mnapost habari zenu?
 
Nisichokubaliana na baadhi yenu humu ni hili la WATANZANIA kufa kwa malengo ya KISIASA kama ilivyotokea Arusha na kabla ya hapo Pemba. Hakuna kifo kinachokubalika lakini hili la vifo vya kisiasa halina TIJA wala maana yoyote kwa Mtanzania wa kawaida. Ni afadhali Mtanzania afe kwa kudai AJIRA, kulalamikia bei ya kilo ya unga, bei ya mkate, bei ya umeme, bei ya maji, karo kubwa za shule, huduma mbaya za elimu kwenye mashule ya UMMA na mambo yanayofanana na hayo.
Tusiendelee kuua watu wetu kwa malengo ya KISIASA ambayo hayawabadilishii lolote watu wetu. Wakati wa kampeni, Dr Slaa alisisitiza mara kwa mara juu ya kutomwaga damu ya Watanzania ili aende IKULU. Ni nini kinafanyika sasa?

Mara zote unapoutafuta ukweli, ukweli huja kukugongea mlangoni...na wewe ukijibu "toka hapa mimi namtafuta ukweli"! Basi ukweli huondoka zake!
Siamini kama una tatizola ufinyu wa akili kiasi hicho, ndhani ni uvivu wa kufikiri tu: au ubishi wa kuelewa! Hayo yote unayoyasema yanakuja vipi bila siasa? wapi nafasi ya demokrasia, nini wajibu wa mwananchi pindi wenye madaraka wanapobaka demokrasia? No wonder hii nchi haiendelei: kwa akili za namna hii, gademu!
 
WildCard,

Sikuwa na nia ya kuchangia, lakini unaponukuu nisingelipenda ukachakachua nukuu. Wakati naeleza uliyonukuu siku zote nilisisitiza kuwa wanaomwaga damu ni Serikali kupitia Jeshi lao la polisi.

Kwa taarifa yako mimi Dr. Slaa na Mhe. Ndessamburo tumepigwa mabomu ya machozi tukiwa katika viwanja vya NMC, tena wakati wa Dua ili tuanze mkutano. Watu wamepigwa risasi za moto mbele ya macho yangu. Wakati huo hakuna kituo cha polisi kimevamiwa, hakuna polisi amerushiwa mawe, hakuna mwananchi mwenye hata jiwe achilia mbali silaha. Hivyo nukuu yako sidhani inatoa picha kamili au ni sehemu ya uchakachuaji ambayo sasa inaelekea kuzoeleka.
 
Ni hakika kila mmoja wetu atabisha hata kama tunafikiri kuwa tupo sawa. Ikiwa IQ ya vingozi wa CHADEMA ilikuwa ndogo, nina mashaka kuwa polisi hawakuwa nayo hata hiyo ndogo. Wakati nipo JKT tuliwaambiwa kinachohitajika jeshini ni akili kijiko na nguvu gunia.

Je, ndiyo iliyotumika wakati wa kutawanya maandamano hayo. Kwa nini polisi watumie silaha za moto kwa wananchi ambao hawakufanya vurugu yoyote? Polisi wangekuwa walinzi na kuhakikisha kuwa anayefanya vurugu anadhibitiwa, kwa bahati mbaya aliyefanya vurugu ni polisi wenyewe.

Poleni wadanganyika wa Tanzania
 
kwa mtindo huu wa polisi kutumiwa na vyama vya siasa hatuwezi fika
huu ni wakati wa kubadilika na kulifanya jeshi letu kuwa si la kutumiwa na wanasiasa kwa matakwa yao na familia zao
tumechoka na wanasiasa wenye fikra mgando
ee mungu bariki jeshi hili la polisi liwe lenye kutoabudu wanasiasa na kuanza kutumikia wananchi :amen:

mapinduziii daimaaaaaaaa:
 
Kwa kauli ya Dr.(Phd) kuna mpango wa kuandaa cinema zima la Arusha, ni ukwel usiopingika tbc haiwez kurusha saga hilo na wengine watapenda kuonesha kama itv,str na ch10 lakn watauogopa kutangaziwa 'intelejensia'. Hivyo basi dvd ziuzwe mtaani ili m2 akitaka siku kupandwa hasira anaangalia cinema hilo.

Ni hayo tu
 
Chama chenye nguvu ya Umma,na kinachoitesa CCM usiku na mchana,Kinachofahamika kwa jina la CHADEMA.

Kipo mbioni katika hatua za mwisho kuonyesha tukio zima la Mauaji ya Arusha lilivyo tekelezwa na Polisi wenye dhama ya kulinda amani.Mkanda huo utaonyeshwa kwenye runinga live,ikiwa ni kulaani kitendo cha TBC-1 kuchakachua ukweli wa tukio kwa kuonyesha vipande baadhi vya tukio zima,huku vipande hivyo vikiegemea kuisafisha serikali dhalimu ya JK.

Mkanda upo makao makuu ya chama,kilicho baki ni Logistics za kuuonyesha.

"Nasema uma ni lazima ujue ukweli na sio kupotoshwa na baadhi ya vyombo na watu kwa maslahi yao'
source.Tanzania Daima tar.18/1/2011.
 
Chama chenye nguvu ya Umma,na kinachoitesa CCM usiku na mchana,Kinachofahamika kwa jina la CHADEMA.
Kipo mbioni katika hatua za mwisho kuonyesha tukio zima la Mauaji ya Arusha lilivyo tekelezwa na Polisi wenye dhama ya kulinda amani.Mkanda huo utaonyeshwa kwenye runinga live,ikiwa ni kulaani kitendo cha TBC-1 kuchakachua ukweli wa tukio kwa kuonyesha vipande baadhi vya tukio zima,huku vipande hivyo vikiegemea kuisafisha serikali dhalimu ya JK.
Mkanda upo makao makuu ya chama,kilicho baki ni Logistics za kuuonyesha.
"Nasema uma ni lazima ujue ukweli na sio kupotoshwa na baadhi ya vyombo na watu kwa maslahi yao'
source.Tanzania Daima tar.18/1/2011.

Wa u upload on line kwenye You Tube ili dunia ione.
 
Wa u upload on line kwenye You Tube ili dunia ione.

Well said Madela...

Better waulete tufanye comparison kati ya tuliokwisha kuona kupitia vyombo kadhaa vya habari pamoja na huo wa kwao then finally tutakuwa kwenye position nzuri ya ku-judge nani mkweli.

Cha muhimu nao wasijekuwa Kama TBC1 mabingwa wa kuunga unga matukio ili kupata uthibitisho wa some pre-conceived ideas kwenye vichwa vyao. Lets wait and see
 
Hawa jamaa watakimbia kabisa.. Huko maofisini na huu tuupeleke the hegue

igp mwema, apc andengenye, ocd zuberi kaeni mkao wa keko..
 
Wa u upload on line kwenye You Tube ili dunia ione.
walete tuwaone ! hivi na wakwao wanaweza hata kudhubutu kuurusha kwenye yutubu? Wataumbuka maana hatakama wamechakachua bado wao ndo wamepiga risasi aliye ua ni polisi hatakam watsema eti walitaka kuteka kituo cha polisi! je wlikuwa na silaha ? Hata wakipambana na mwizi wanaruhusiwa kumpiga mguu siyo kuua !
 
Back
Top Bottom