Elections 2010 Dk Bilal amfagilia Mkapa asema aliacha mabilioni hazina

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
bennymkapa.jpg
Rais Mstaafu Benjamin Willium Mkapa


MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal amewaambia wananchi wa Masasi kuwa, rais mstaafu wa awamu ya tatu ambaye ni mkazi wa Jimbo la Masasi, Benjamin William Mkapa alikuwa ni kiongozi mahiri ambaye aliongaza Tanzania na kwamba atakumbukwa daima kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya Tanzania.

Dk Bilal amewahi kufanya kazi na Rais Mstaafu Mkapa wakati wa awamu ya pili, wakiwa pamoja katika Wizara ya Sayansi na Elimu ya Juu.

Dk Bilal aliyepo hapa Masasi akitokea Newala mkoani Mtwara alikofanya mikutano ya kampeni alisema uongozi wa Mkapa uliingia madarakani katika kipindi cha mabadiliko ya uchumi na kusababisha Tanzania kuwa katika kipindi kigumu na kufanya kazi kubwa katika kipindi cha utawala wake na kuacha kasma ya kutosha katika hazina ya Taifa.

“Kila nikifika hapa nakumbuka majina ya viongozi mahiri waliotoka hapa. Nafahamu jambo kubwa walilolifanya kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania. Kila siku nitawakumbuka mzee Mkapa na Mama Anna Abdallah. Wote hawa wamefanya makubwa ya kuenziwa katika Tanzania.

“Wana Masasi mkipigieni kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa kinawajali na kina ilani inayotekelezeka. Tena tambueni kuwa hiki ndicho chama pekee kinachogusa maendeleo ya wanyonge,” alisema Dk Bilal.

Awali akinadi ilani ya chama cha Mapinduzi kwa mamia ya wakazi wa Wilaya ya Masasi, Mgombea Mwenza Dk Bilal alisema kila anapoitazama Tanzania na kuitazama CCM anakumbuka utumishi uliotukuka uliofanywa na liomo viongozi wa chama hicho.

“Ndani ya chama chetu kuna viongozi mahiri ambao wanafanya kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo yetu. Wanajituma kwa nguvu zao zote na wana hakikisha kuwa kila jambo linatelekezwa kwa wakati,”alisema.

Dk Bilal amekuwa katika kampeni katika mkoa wa Mtwara tangu juzi na leo anaanza kampeni katika Mkoa wa Ruvuma. Tangu aingie katika mikoa yaKusini, amegeuka kuwa kivutio kwa wanachi ambao mara kwa mara wamekuwa wakisimamisha msafara wake na kumtaka awasalimu.

Chanzo: Dk Bilal amfagilia Mkapa asema aliacha mabilioni hazina
 
Alikuwa anawadanganya tu. Anasahau jinsi Mkapa alivyortuhusu wizi wa EPA -- hujuma kubwa kabisa dhidi ya Watanzania ambao haujapata kutokea katika historia ya nchi yetu. Hawa CCM kwa nini wanapenda kusema uongo uongo tu kila wakipata jukwaa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom