Diwani wa CHADEMA ashusha bendera ya CCM na kupandisha ya Taifa

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
[h=6]Jamaaa namkubali sana kwa ujasiri huu..

"Nipo Kituo cha Polisi Moshi nikiandika maelezo kuhusu tuhuma za kushusha bendera ya CCM kwenye ofisi za serikali ya kijiji chekereni na kupandisha bendera ya Taifa! Niko tayari sana kwa hatua zitakazochukuliwa".
[/h]Alberto Msando through Facebook
Diwani wa CHADEMA Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini
 
Watatisha kwa maneno ya ukali tu, hawana mamlaka ya kuchukua hatua yoyote.
 
Kuna watu bado wanafikiri bado tuko zile enzi za chama kushika hatamu.Diwani hongera sana!
 
Hii nchi inataka viongozi kama wewe,iam real proud of you kamanda!
 
Safi, sana tu.

CCM wameifanya nchi hii kuwa shamba la bibi. Kamanda Albert ni mwanasheria makini, anajua alichokifanya na ni vizuri wasomi kuiga mfano huu badala ya kuchumia tumbo. Ni mnukuu Hon. Rev. Peter Msigwa "tusikubali akili kubwa kuongozwa na akili ndogo".
 
Mi ninavyofahamu,bendera ya taifa ndo inatakiwe iwekwe kwenye ofisi za umma.Sasa hili gamba lililo comment hapa juu lina maana gani au ndo udhaifu wenyewe?

Eti cheap popularity,ni nani mwingine aliyewahi kuufanya uzalendo kama huu. nMaslahi ya taifa lazima yawekwe mbele na ndo maana hajaweka bendera ya CHADEMA bali ya taifa.

Ndo unajiita KIBOKO YENU-kisichokuwa na fikra huru always!
 
Safi sana mtoa mada na hongera zake huyo diwani amefanya kwa vitendo!

Ofisi ya kijiji bendera inayotakiwa ni ya taifa siyo ya chama.
 
[h=6]Jamaaa namkubali sana kwa ujasiri huu..

"Nipo Kituo cha Polisi Moshi nikiandika maelezo kuhusu tuhuma za kushusha bendera ya CCM kwenye ofisi za serikali ya kijiji chekereni na kupandisha bendera ya Taifa! Niko tayari sana kwa hatua zitakazochukuliwa".
[/h]Alberto Msando through Facebook
Diwani wa CHADEMA Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini

mkuu msando uko right. ofisi ya serikali ya kijiji ni ya umma sio chama. km ingekuwa ni ofisi ya chama cha mapinduzi ya kijiji kweli lingekuwa ni kosa. polisi waliokuandikisha maelezo watakuja kujibu mbele ya wananchi very soon. hakuna mwanzo usio na mwisho.
 
anatafuta cheap popularity hana lolote huyo eti na yeye atokee kwa gazeti na tv

Jadili hoja usijadili mtu. Je, ni sawa bendera ya CCM au chama kingine cha siasa bendera yake kupepea/kupandishwa katika ofisi ya serikali? Haujui kuwa mfumo wa chama kimoja aka chama kushika hatuma ulipita? Kweli wewe ni kilaza
 
anatafuta cheap popularity hana lolote huyo eti na yeye atokee kwa gazeti na tv

Hapana!!!!!!!!. Alichokifanya ni kitendo kizuri sana. Kwani katika ofisi ya Serikali ya Kijiji inapaswa kuwekwa bendera ya Taifa.

Kumbuka tupo katika mfumo wa vyama vingi. Mambo ya Chama kusihika Hatamu yamepitwa na wakati.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Back
Top Bottom