Diwani wa Chadema akamatwa na Bunduki

Hakukamatwa na silaha bali aliikabidhi silaha kwa mkuu wa mkoa kwa kukubali mwenyewe.Kuwa na siraha kinyume na sheria ni kosa, ila kuna hili la kutangaziwa kwamba wenye siraha kinyume na sheria wazikabidhi sehemu fulani la sivyo wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria, wakikabidhi yameisha, kama wale wa epa waliambiwa wakabidhi fedha yaishe.Sijui mamlaka haya huwa yanatoka wapi,kwamba kabidhi yaishe,nafikiri sio ya kisheria, lakini imezoeleka tu.
thenk u bro,wewe ni mwanaharakati,nashukuru kama ulisikia ivo kama mimi nilivosikia,msekwa anawalipa watu waje watuchafulie jamvi bahati nzuri wote tunawajua na watatoka wenyewe,kwani wangap walikuja na wakatuacha.?
 
Sielewi ni vipi wengine wanakimbilia kufikiri inahusishwa na chama chake.

Amesikika kwenye tv akihojiwa na mkuu wa mkoa akakiri kwamba anamiliki silaha aliyopewa na "jamaa mmoja". Kisha akaongoza msafara wa mkuu wa mkoa kwenda kuifukua

Baadaye akasikika anaomba msamaha kwa wanakijiji wenzake

Swali langu ni kwa nini kazi ya upelelezi na interrogation ifanywe na mkuu wa mkoa . Kisha kwa nini tv zialikwe kuanzia kumkamata, kumhoji, kukubali kwake, na kwenda kuifukua

Kwangu mimi ilikuwa kama natazama igizo badala ya habari. Hasa RC alipokuwa ana act kama Rambo na vile alivyokuwa anasifiwa na mleta habari - Mabere Makubi

Mambo kama haya na yanayo fanana na haya ndio yanatulazimisha wengine tupaze sauti kusema, katiba mpya iharakishwe upatikanaji wake, na katika katiba hii mpya kuwe na sheria itakayo simamia vizuri utendaji wa vyombo vya ulinzi na usalma. Vitumike kwa maslahi ya umma si kupiga propoganda za viongozi, mbaya zaidi viongozi mafisadi.
 
ndugu avatar yako inanikumbusha mbali sana. wewe inawezekana ulipenda kuiweka kwa ajiri ya kuigiza. ndugu zungumza sana lakini omba usiwemo kwenye kundi la watu wa hivo. ila nazani unaweza hisi nimetoka mazingira gani!
Mkuu hiyo Avata sio maigizo ni maisha halisi ya watanzania wengi wakiwemo wazazi wangu ambayo bado wanaishi aina hii ya maisha hii ikimaanisha kuwa nami bado naishi aina hii ya maisha indirect mzee! So nimeiweka nikimaanisha kabisaa
 
Mengi mliyochangia nakubaliana nanyi bali ninatofautiana nanyi pale mnapohoji juu ya mkuu wa mkoa kukamata. Kumbukeni mkuu wa mkoa ndiye mkuu wa ulinzi na usalama katika mkoa, hivyo kushiriki kukamata ni sehemu ya majukumu yake. Huwezi kujua ni mazingira gani yalipelekea asimwamuru RPC kushughulikia suala hilo, na huwezi kujua yeye RC alipata vipi hizo taarifa (kama ni za kweli na si za kupangwa). Sitashangaa kusikia kesho kuwa mheshimiwa rais nae amekamata mtu anamiliki kifaru kwa mfano...........
 
Hivi kusema 'diwani wa chadema' ni sahihi? Nilidhani utakuwa sahihi ukisema 'diwani wa kata X'? Maana ukimwita diwani wa chadema inaonesha kachaguliwa na wananchi wa kata ya chadema.
 
Ngwendu watu wa Mara kutembea na silaha ni kawaida kama wamasai. sioni kwa nini kumiliki silaha iwe tatizo! the problem is legality here so atawajibika kisheria. Ninachojua aliyekuwa meya wa Mwanza ndiye alitajwa kutumia wa2 kuua. Propaganda hazitatusaidia kawa taifa. mwizi/jambazi/fisadi sheria zipo zifanye kazi. usil mambo ya JMK YA KUJUA WAUZA UNGA, BALALI ALIPO, WAKWEPA USHURU, WEZI WA EPA HALAFU NINI??!
Narudia tena kuandika kuwa chadema inavyoonekana wengi ni majambazi.
 
Moja ya gazeti la leo nadhani Jambo leo imeandika eti "Chadema inamiliki silaha za kivita".
Hatudanganyiki.
 
Ndo maana hivi vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya viondolewe kazi ya OCD kafanya yeye,nadhani huu ni mkakati mahsusi ikiwa ni pamoja na kuwanyima airtime CHADEMA ili wasionekane wawapoteze...wanasahu kwamba ili CHADEMA kipotee ni kutekeleza kwa vitendo maisha bora waliyoahidi..!
 
Baada ya P. Msekwa kusema JF ni tishio kwa ccm naona ameagiza vijana waje humu kwa nguvu zote ata kwa kufoji kuleta habari za kuikosoa CDM ila wamekosa mantiki kwa wanachoandika kinakosolewa.
Ila tunawakaribisha kwani aliyetumwa anajulikana mda sio mrefu wataondoka wenyewe.
 
Hivi yule Meya wa CCM Mwanza aliyekuwa rumande kwa tuhuma za mauaji ya katibu wa ccm ameshatoka??

Hivi Kesi ya Chenge ya Kuua mabinti ilikwishaje, na je kunakesi iliyofunguliwa kwa waliouawa na silaha zinazomilikiwa kihalali kule Mbagala na Gongo la Mboto!?,

Hii ni story ya kupikwa ila haitukatishi tamaa, mambo ndio kwanza yanapamba moto.
 
mbwembe za CCM hizo Polisi walishindwa ina maana RC ni Mganga wa kieneyeji au Gagula Mpaka akaweza kutabili kwa Diwani kaficha Bunduki pale alipoifukua, alfu kosa binafsi kwa nini magazeti yashupalie kama la Chama , ni marangapi madiwani wanashiriki au polisi kushiriki kwenye wizi au upolaji wakati wanamilikiwa na serikali yaCCM? hata hivyo siwashangai kwani sasa hivyi wanawaingiza kwenye system hata warundi na wakenya wakati katika serikali ndio maana vita ya kuuana hawa watu ni asili yao , kama ile ya Tegeta ukiwauliza walioua utakuta na vitambulisho vya CCM. Kujilinda ni muhimu huji kuwa mara watu wengi wanamiliki bunduki kwa ajiri ya kulinda mifugo yao
 
Ni silaha ambayo raia haruhusiwi kuimiliki...!



Kuna watanzania wengi wanaokuwa kwenye vyama mbalimbali kama binadamu wamefanya makosa na chama hakikuhusishwa Ditopile alivyomuua dereva wa daladala kwa pisto hakuna aliyesema ditopile wa CCM ametumwana CCM au hakuna aliyesema Rafiki wa KIKWETE aliyesimamia harusi ya KIKWETE NA SALMA ameua dereva kwenye makutano ya barabara ya Kawe na Lugalo watu tulimtuhumu Ditopile kwa matumizi mabaya ya pisto kama mtu binafsi
Hata alivyowekwa nje ya rumande tofauti na watuhumiwa wote wenye kesi za mauaji hakuna aliyesema Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete amemtoa kwa vile ni rafiki yake au ni mwanaCCM sisi tulisema polisi ni vipi wamefanya upelelezi wa haraka kwa Ditopile wakati kunawatu wako ndani kwa makosa
Chenge alipotumia gari lake na kuuwa wanawake wawili halafu akakimbia hatukusema Chenge mwanachama wa CCM ameua wanawake wawili alafu akatimuka alituhumiwa kama chenge
Masha alipotishia wanachi kwa pisto hatukusema Masha mwanachama wa CCM anatumia vibaya silaha,sasa huyu diwani wa Chadema atuhumiwe kama mtanzania yeyote atakayetuhumiwa anayemiliki silaha kinyume cha utaratibu
sidhani hii kampeni kama itasaidia ,endelea tuu wanachi wanajua kupembua pumba na mchele ,eneo la Bunda ,serengeti,tarime mara ngapi silaha zimekamatwa toka kwa wananchi na zikachomwa
 
Sielewi ni vipi wengine wanakimbilia kufikiri inahusishwa na chama chake.

Amesikika kwenye tv akihojiwa na mkuu wa mkoa akakiri kwamba anamiliki silaha aliyopewa na "jamaa mmoja". Kisha akaongoza msafara wa mkuu wa mkoa kwenda kuifukua

Baadaye akasikika anaomba msamaha kwa wanakijiji wenzake

Swali langu ni kwa nini kazi ya upelelezi na interrogation ifanywe na mkuu wa mkoa . Kisha kwa nini tv zialikwe kuanzia kumkamata, kumhoji, kukubali kwake, na kwenda kuifukua

Kwangu mimi ilikuwa kama natazama igizo badala ya habari. Hasa RC alipokuwa ana act kama Rambo na vile alivyokuwa anasifiwa na mleta habari - Mabere Makubi

Desparation calls for desparate measures..... wanatapatapa, wanajaribu kuipaka matope Chadema na kuipaka mafuta CCM lakini kwa mshangao wao mafuta wanayoipaka CCM yanageuka kuwa ma.vi na matope wanayoipaka Chadema yangeuka kuwa mafuta... kama yesu alivyobadirisha mawe kuwa mkate jangwani
 
Mimi naitafuta AK 47 moja wadau maana tulikofikia haya masihara hayaishi bila kuadabishana.
 
Back
Top Bottom