Diaspora: Kumbe Freeman Mbowe kumsifia Rais Samia ni baada kufunguliwa Account zake za Fedha zilizokuwa zimefungwa

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,274
Nimesikiliza haya mahojiano vizuri Diaspora wanalalamika kwamba Freeman Ekael Mbowe anamsifia mama baada ya mambo yake binafsi kushughulikiwa na Rais, ikiwemo kufunguliwa Account zake za fedha ambazo zilifungwa muda uliopita, kutoka jela pamoja na shughuli zake mbalimbali za kibiashara.

Diaspora wameenda mbali zaidi na kusema halikadhalika kwa Tundu Lissu baada ya kupata stahiki zake za Ubunge wote kwa pamoja ndio wanamsifia lakini Diaspora wanasema Rais Samia hajabadilisha chochote kwenye demokrasia ikiwemo mikutano ya kisiasa mpaka sasa bado hajaruhusu na kwamba Mama ndie aliyeanzisha tozo kuwaumiza zaidi wananchi maskini wa Tanzania.

 
Mi nilijua tu huwezi toka jela break ya kwanza ikawa ni Ikulu kumbe kujidai wana mwazungumzo na Rais ni kukunjuliwa mambo yao binafsi., tutamkumbuka hayati Maalim Seif Sharif Hamad hakuwa mbinafsi hata kidogo.
 
Kama hizo ni kauli za diasport basi itoshe kusema ni WASENGEREMA na akili zao Hazina akili kabisaa! Kwa hiyo walitaka Mbowe asilipwe fedha zake alizodhulumiwa! Au akilipwa amtukane Rais ili awe mpinzani kweli?! They should learn to give credit where it is due!
 
Back
Top Bottom