Deus Seif na Abubakari Alawi waliokuwa viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania waigaragaza Serikali Mahakamani

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Watajwa hapo juu walikuwa ni viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania ambao Juni 28 2022, walitiwa hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi na uchepushaji wa fedha za walimu kiasi cha shilingi 13,900,000 na matumizi mabaya ya madaraka. Kwa kosa hilo walifungwa miezi 6 gereza la Ukonga lakini walikaa gerezani muda usiozidi wiki moja walitamba kwa falsafa yao ya “HAKUNA MKATE MGUMU MBELE YA CHAI”.

Kabla ya hukumu hii wakati kesi inaendelea waliendelea kutamba kwamba TAKUKURU huwa haishindi kesi mahakamani na kweli kifungo cha miezi sita kilikua laini sana kulinganisha na hukumu ya Agosti 24, 2022 ambapo Jamhuri ilishinda katika Shauri Na. ECO. 90/2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Shauri hili lilimhusu, JULIUS K. MBISE, aliyeshtakiwa kwa makosa ya Ufujaji na Ubadhirifu, Matumizi Mabaya ya Madaraka pamoja na Kuisababishia Serikali Hasara, kinyume na vifungu vya 28 (1), 31 vyote vya PCCA, Cap 329 na aya ya 10 (1) ikisomwa pamoja na Jedwali la kwanza la Sheria ya EOCCA, Cap 200 [R.E 2019].

Mshtakiwa ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya KIKWE, alifuja kiasi cha sh Milioni Saba (7,000,000/=) fedha za Halmashauri ya (W) ya Meru.

Mshtakiwa alipatikana na hatia na akahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 Jela na kutakiwa kurejesha kiasi cha sh. Milioni Saba (7,000,000/=) alizofuja.

Nchi hii hii, kwa sheria hizi hizi, wafanyakazi hawa hawa, makosa yale yale lakini hukumu tofauti. Mbona ni ngumu kueleweka? Hapa tofauti ni moja, Julius Mbise hakuwa na chai ya kulowanishia mkate, chai ambayo Deus Seif na Abubakari Alawi wanayo. Ikumbukwe kuwa kabla ya hukumu ya kesi hii, mahakimu watatu wa awali walishajitoa japo chai walikunywa ila mkate haukulainika, mkate uliolainika ulikuwa wa Mheshimiwa Richard Kabate na akawaonya wasije wakakata rufaa. Naomba nirejelee kile nilichokiandika tarehe 22/02/2023.



HUKUMU YA UFISADI WA DEUS SEIF NA ABUBAKARI ALAWI TAR 10 Machi 2023, WALIMU NA WANACHAMA WA CHAMA CHA WALIMU WASUBIRI KWA HAMU

Kama inavyofahamika, watajwa hapo juu walikuwa ni viongozi wa chama cha walimu Tanzania, Deus Seif akiwa katibu mkuu na Abubakari Alawi akiwa mweka hazina wa Taifa. Walishtakiwa na Jamhuri (TAKUKURU) Mei 2021 kwa kesi ya uhujumu uchumi, wizi wa fedha za walimu na matumizi mabaya ya madaraka. Hatimaye walitiwa hatiani na hakimu Mhe. Richard Kabate na kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani Tar 28 Juni 2022. Kwa kutumia falsafa yao ya (Hakuna mkate mgumu mbele ya chai) walikaa gerezani Ukonga Siku 6 tu. Si Kamishna wa Magereza wala mahakama ya Kisutu walioeleza sababu kwa nini wafungwa hawa walikaa juma moja gerezani; kisha wakaendelea kutumikia kifungo nje ya gereza na kumaliza kifungo hicho Oktoba 2022. Kilichoshangaza watu ni kwamba inakuwaje kwa makosa makubwa kama haya kutendwa na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi eti wafungwe miezi 6 tu?

Jingine la kujiuliza, ni kwa nini Hakimu Richard Kabate kabla ya kuutafuna mfupa ambao mahakimu wenzake 3 waliushindwa na kujiuzulu kwa kesi hii hii kabla yake alithubutu kufanya hivyo? Hukumu hii iliyosomwa tarehe 28 Juni saa 1 hadi saa 3:20 Usiku kwenye hukumu hii Hakimu Kabate aliwaonya washtakiwa wasithubutu kukata rufaa kwa kuwa hawatakutana na Kabate mwingine? Hakimu aliona nini? Na kwa nini aliwapa hukumu laini kiasi hiki? Hukumu laini kama hii ina funzo gani kwa wizi wa mali na fedha za wafanyakazi kama walimu? Hapa inatia shaka kama mkate haukukutana na chai.

Wafungwa tajwa hapo juu, kabla ya kukata rufaa inasemekana walionana na mmoja ya wakili mashuhuri hapa nchini (jina tunalo) na akawashauri wakate rufaa kwa kesi hii na watashinda kwa kuwa kushinda kesi mahakamani hakutokani na kuifahamu tu sheria bali muhimu ni kuifahamu mahakama, sifa ambayo wakili huyo alijigamba anayo, jambo ambalo walilifanya na Jamhuri yenyewe haikuwa imeridhika na hukumu hivyo nayo ilikata rufaa kwa kuona kwamba hukumu waliyopewa mafisadi hawa ilikuwa ni kichekesho. Rufaa ikasikilizwa na hukumu ilikuwa itolewe tarehe 17 Februari 2023 na Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam chumba namba 4 na Jaji Ephery Kisanya. Jaji Kisanya aliamua kuahirisha hukumu hiyo kwa sababu ambazo hakuzibainisha. Cha kuvutia ni kwamba hukumu hiyo iliyokuwa isomwe saa 4 asubuhi saa moja kabla walionekana viongozi wa dini waliokuwa wakizunguka jengo la mahakama huku wakipiga dua. Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 10 Machi 2023. Umma wa walimu, wafanyakazi wa chama cha walimu, na jamii kwa ujumla wanataka kuona kwamba, au haki inatendeka au hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Na hii ni kwa sababu wahusika wameshikwa mkono na baadhi ya wanasiasa waandamizi na viongozi wa serikali kupeleka maombi ngazi za juu za mamlaka waonewe huruma kwa kigezo cha kwamba walipokuwa madarakani walisaidia sana kwenye ujenzi wa madarasa, ununuzi wa madawati na misaada mingine kwa umma. Lakini ifahamike kuwa hizo fedha walizokuwa wakitumia hazikuwa zao bali zilikua fedha za walimu na hazikutumika hivyo kwa ridhaa ya walimu. Ila walizitumia kujijengea majina na kulinda nafasi zao. Hadi leo hii, watajwa wamefanikiwa kuwaaminisha mashabiki wao wachache kwamba kwenye hukumu ya tarehe 10 Machi 2023 mafisadi hao watatoboa wakiwakumbusha wimbo wa Dar es salaam Jazz Band wa mwaka 1965 usemao “Wewe mtoto wacha kupiga mayowe, waache watu waone wenyewe”. wanatarajia kufutiwa hukumu ya awali wapate uhalali wa kurudi kwenye utumishi wa umma kisha kurudi chama cha walimu kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Jijini Tanga Machi 2023 japo tarehe bado haijabainishwa. Kwa hivi sasa viongozi hao wanaendelea kukivuruga chama cha walimu kwa kuwatumia baadhi ya makatibu na wenyeviti wachache wa ngazi za wilaya na mikoa na baadhi ya wafanyakazi wa makao makuu kwa kutoa taarifa za uongo kwa viongozi wa serikali na mamlaka zake kuhusu chama hata kunyofoa baadhi ya vielelezo ofisini na kuviweka kwenye mitandao ya kijamii.

Usiku wa Deni haukawii kucha na jogoo awike au asiwike nilazima kutakucha, Tarehe 10 Machi 2023 sio mbali, tutajua ni nini kinaendelea. “
Mwisho wa Taarifa



Yaliyosemwa kwenye taarifa hii ya tarehe 22/02/2023 ndio yamethibitika maana Jaji katika hukumu yake amebainisha kwamba Deus Seif na Abubakari Alawi walifungwa kinyume cha sheria na hawakuwa na hatia hii ina athari mbili.

  1. Serikali imeshindwa kutetea haki za walimu
  2. Ni uthibitisho wa kwamba Serikali ni Mkate na mafisani wa fedha za walimu ni Chai
  3. Kwamba Serikali si lolote mbele ya wenye fedha na hii ni kwa sababu wapo viongozi wa juu waandamizi wa serikali na wanasiasa wanazimendea fedha zitokanazo na ada za walimu na ili kuzipata ni lazima wawe Chai mbele ya Mkate ambao ni Serikali yenyewe. Kwa sababu maamuzi ya Mahakama Kuu ni yenye shinikizo. Macho na Masikio ya walimu ni kufahamu serikali itafanya nini baada ya kudhalilishwa na mafisadi hawa kiasi cha kushindwa mahakamani kwa namna isiyoeleweka.
Kinachoendelea ndani ya chama cha walimu, walimu na Jamii kwa ujumla ni taharuki na kujiuliza kwamba Serikali yetu ni thabiti? Makini? na inayothamini watu. Hili linatokeaje?

Mafisadi hawa hawa wameweka zuio la kufanyika kwa mkutano mkuu wa chama cha walimu uliopangwa kufanyika Juma linaloanzia tarehe 13 Machi JIjini Tanga, hivi zuio hili ni kwa faida ya nani? Tungependa kuiasa serikali yetu tukufu, itambue kwamba walimu na jamii sio wajinga na watu wachache wasimharibie Mheshimwa Rais ambaye amekuwa akipambana kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika nyanja zote za jamii.
 
Wanautani hao eti ubadhirifu wa shs million 13😅hiyo si ile barrier ya alawi?mtu anamiliki Kijiji chenye apartments huko kibaha,useme kaiba mil 13,alawi na boss wake deus ni mamilionea kwa wizi wa pesa za CWT, kalaghabaho 😅 Walimu pambanieni kuajiriwa CWT Kuna bonge la mzinga wa asali,ni juhudi yako tu kuirina vizuri ukipata chance.
 
Wanautani hao eti ubadhirifu wa shs million 13hiyo si ile barrier ya alawi?mtu anamiliki Kijiji chenye apartments huko kibaha,useme kaiba mil 13,alawi na boss wake deus ni mamilionea kwa wizi wa pesa za CWT, kalaghabaho Walimu pambanieni kuajiriwa CWT Kuna bonge la mzinga wa asali,ni juhudi yako tu kuirina vizuri ukipata chance.

Cc mpwayungu village
 
Naiona hila tu imejaa kwa viongozi tajwa ..kiasi hicho kilichoibiwa ndo vituko zaid...Kimsingi hakuna kesi yoyote hapo ...zaid ya Watu fulani kujaribu kuwatia Shombo baadhi ya viongozi tajwa(deus&alawi) ili washike wao msukan kwa njia Ovu..nasema hv Mwalimu Seif & Alawi shikilien hapo Hapo' ..hakika nyie n viongozi tukuka nawaona mbali sana ...
 
Mwandishi yupo kwenye kampeni Ili nae atuingize kwenye mtego huohuo, Cwt ni chombo Cha wapiga Dili tu, ukitaka na ww kachukue zako Kaa kimya!
 
Back
Top Bottom