Dereva Halima aliyekatika mkono asema 'Niliona mtu ninayemjua akivuka barabara kabla ya ajali'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,323
5,493

Siku chache baada ya tukio la kukatika mkono wa kulia, Halima Mbwana aliyepata ajali wakati akiendesha basi la Super Feo lilipokuwa likitokea Songea kwenda Dar es Salaam, ameelezea kilichotokea sikunde chache kabla ya tukio.

Kwa sasa Halima anaendelea na matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya St. Benedict iliyopo Ndanda Mtwara baada ya ajali hiyo iliyotokea Mei 22, 2022.

“Wakati natokea Songea kwenda Dar es Salaam kupitia Lindi, sehemu zote hatarishi nilikuwa nimeshazivuka, kuna sehemu ina kona ya kawaida sana, nikaona kuna mtu anavuka kutoka kulia kwenda kushoto na nina mfahamu, ilikuwa ghafla sana.

“Nilishtuka sana, nikawa namkwepa, kushtuka gari likawa limeshalalia upande mmoja, lakini baadaye nilibaini kuwa hakukuwa na huyo mtu, ni miujiza tu ya barabarani, hivyo vitu vipo.

“Wakati gari linalala mkono wangu ulikuwa nje, lilivyoanguka mkono wangu ulikatika palepale nauona, nikakumbuka kuwa gari bado linawaka na inaweza kulipuka, nikatumia mkono wangu wa kushoto kulizima kwa usalama wa kuondoa moto.

“Namshukuru Mungu, nilihudumiwa vizuri hospitali, ndoto yangu ilikuwa kuendesha gari zaidi ili baadaye nisomee urubani, lakini sijakata tamaa kuwa maisha yangu yameishia hapa,” – Halima.


Source: Azam TV

Pia soma: Basi la Super Feo Songea-Dar via Lindi limepata ajali. Dereva mwanamke avunjika mkono
 
Hilo linawezekana.

Uchovu, mawazo, mwili kuishiwa maji na safari za nenda rudi zisizoisha zinapelekea upatwe na hallucinations
Ndio maana unaambiwa ukiona uza uza lolote usikwepe..na kweli ukikilenga hukioni.
sababu ni hallucinations tuu..

Sababu kubwa kutopumzika,hapo umefika destination,badala upumzike unakula bata hadi asubuhi..mwili umeishiwa maji kwa ulevi..unaanza safari tena.lazma uone mbuzi wengi barabarani.
 
Daah kitu kama hii niliiona Sukamahela pale Singida bibi mmoja yuko katikati ya barabara na yuko umbali wa mita chini ya 5, eeee buana weeee ile kuhamaki na kutoa macho pamoja na kushika kichwa akili ikiwa imehama mtu anaonekana nyuma akikatisha barabara kulia kwenda kushoto ukitokea Dodoma.

Hapo ndio nikajua kuna mambo japo ile picha kichwani huwa haileweki (ninachoona ndicho au naota)
 
Msigwa huyo akaweka kiini macho ili dereva aangushe gari, abiria wafe yeye apate kafara, huyu baba atatuua wangoni wote khaaah.

Tutamchoka na tutamfurusha km mwenzie Ottawa. Msieeew zake.
Msigwa kama msigwa

Ninavyopenda superfeo/seloustutakufa
 
Mauzauza yapo barabarani,ilikuwa ni ghafla sana nilishutukia kitu kama Mbwa anakatiza barabara,sikutaka kumkwepa kwani umbali ulikuwa ni mdogo sana na ni usiku,nikamgonga na ngao ikapasuka nikasikia kabisa imedondoka na vipande vimepasuka kwa chini,Nikasimama kama mita 300 kuangalia nikakuta kweli imepasuka,nikasema ngoja nirudi labda naweza kuokoa baadhi ya vitu vilivyo dondoka,siku ona Mbwa,wala kilichoangauka,wala damu.Yani barabara ni nyeupe kama hakuna kilichotokea,kesho yake nikapita mchana ili niangalie vizuri sikuona chochote,ukichukulia kuwa pamenyooka kabisa.Nikaulizia wanaopafahamu wakaniambia hapa hivyo vitu vya kawaida sana.Wanaojua njia ya Babati-Arusha karibu na daraja la Kiongozi...
 
Back
Top Bottom