Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,554
Mpaka sasa taarifa zilizopo zinasema basi la Golden Deer T 618 DMG kutoka Kyela kuelekea Dar es Salaam imepata ajali.
Taarifa zaidi zitakujia baadae.
---
Morogoro. Mtu mmoja amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito wilayani Mikumi na wengine wametibiwa na kuruhusiwa baada ya basi la kampuni ya New Force walilokuwa wakisafiria kutoka Kyela kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Agosti 7, 2023 jioni eneo la Msimba kwenye mteremko na kona za Iyovi Mikumi ambapo amemtaja majeruhi kuwa ni Elinipenda Kishimbo (26) aliyeteguka mkono.
Kamanda Mkama amemtaja dereva wa basi hilo kuwa ni George Obedi (48) huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva huyo kwa kuwa alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila ya kuchukua tahadhari na hivyo kukutaka na gari jingine uso kwa uso.