Deo Fulikunjombe aomba mwongozo kukomesha tabia ya kufuja muda

Niko jimbo la Mnyika, siwezi changua Kenge yeyote hata awe na rangi gani kutoka chama cha Magwepande!
Najuwa sana madhara ya hiki chama cha Mabwepande lakini kuna wakati tuwe wakweli X Mchungaji ni heri kumchaguwa mgombea wa CCM Deo FUlikunjombe kuliko kumchaguwa mgombea wa Chadema Shibuda. Hizi ndizo aina ya siasa tunazopaswa kwenda nazo kwa sasa.
 
Hamna kitu kinakera bungeni kama hayo majina yanapotajwa! upumbavu wa hali ya juu mno
 
Dhana nzima ya kutaja majina ni sio wabunge wote wanapata nafasi ya kuchangia kwa kuongea sasa wale ambao wanachangia kwa maandishi wanataka Wananchi wao nao wasikike kua hua wanatoa michango bungeni hata kama hawataonekana wakichangia kwa kuongea
 
I saw this live while happening lakini cha ajabu waziri wa fedha ile anaanza tu kusoma hotuba yake akaanza na utaratibu ule ule usio na tija! Yaani mtu anamshukuru mkewe, familia ah!
 
Najuwa sana madhara ya hiki chama cha Mabwepande lakini kuna wakati tuwe wakweli X Mchungaji ni heri kumchaguwa mgombea wa CCM Deo FUlikunjombe kuliko kumchaguwa mgombea wa Chadema Shibuda. Hizi ndizo aina ya siasa tunazopaswa kwenda nazo kwa sasa.

aisee baba yangu nakuunga mkono asilimia zote

nipm nikutumie mbege
 
Hii Ni WIZARA YA Fedha:
===============

UTANGULIZI:
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu liweze kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na
matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

3. Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza wafuatao
kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa mawaziri kama
ifuatavyo:
Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (Mb); Mhe.
Mhandisi Christopher Kajoro Chiza (Mb); Mhe. Dkt. Harrison
George Mwakyembe (Mb); Mhe. Dkt. Fenella Ephraim
Mukangara (Mb); Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki (Mb);
.......................................

4. Mheshimiwa Spika, nawapongeza pia, Mhe. Alhaji Adam
Kimbisa (Mb.); ....................

5. Mheshimiwa Spika, maandalizi ya Bajeti hii yamehusisha
wadau na Taasisi mbalimbali. Napenda kuwashukuru walioshiriki
kwa namna moja au nyingine kufanikisha matayarisho yake
. Kwa
namna ya pekee, ninaishukuru Kamati ya Bunge ya Fedha na
Uchumi chini ya uenyekiti wa Mhe. Mtemi Andrew John Chenge
,
.............................

6. Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Mhe. Stephen
Masatu Wasira (Mb)
, ...........................

7. Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru Wakuu wa
Idara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na
wafanyakazi wote wa Wizara ya Fedha kwa ushirikiano wao
.
...................................
 
Ni upuuzi kufikiri eti kupunguza muda wa kuongea bungeni ni sawa na kuongeza ufanisi, hii ni sawa na kusema kuwa hakuna haja ya kuwa na bunge kabisa maana hata huo muda kidogo wanaotumia kuongea wangeweza kuutumia kutenda kazi zaidi jambo ambalo lingekuwa athariza moja kwa moja kwenye ufanisi. Bunge la sasa limejaa masupa staa wanaofanya kila linalowezekana kuwa kurasa za mbele kuliko kufanya majukumu yao ya msingi.
 
ufanisi wa bunge la awamu hii (4) tena chini ya huyu mama ni la hovyo kiasi kwamba inafikia hatua linatia hata kichefuchefu kuliangalia na zaidi kama unavistress vyako vinaongezeka kwa hawa waheshimiwa kutokuwa serious na mda na nafasi tulizowapa kutulindia rasilimali zetu
 
CCM wanamchukia Deo kuliko hata ya Tundu Lissu!!!! Mfano halisi wa bingwa wa kutaja watu ni yule Naibu waziri aliyeibiwa zile silaha zake za maangamizi kule morogoro pamoja ni milaptop minne na Simu zinazo jaa kiroba huwa akitaja wake zake huwa nachoka kwasababu anawataja mpaka mademu wake wa Moro waliomliza

da! We jamaa unanitesa mbavu, nipo kwa watu, nalazimika kuchekea tumboni hadi maumivu!
 
I saw this live while happening lakini cha ajabu waziri wa fedha ile anaanza tu kusoma hotuba yake akaanza na utaratibu ule ule usio na tija! Yaani mtu anamshukuru mkewe, familia ah!
Tusubili mwongozo wa speaker maana bado hajatowa mwongozo, ila utatolewa kabla hajasitisha shughuli za Bunge za asubuhi hii, nitasikitika sana kama speaker ataharalisha upumbavu huu uendelee. Leo 0mwigulu Nchemba kaleta wageni wageni wake Masheikh 69 kutoka jimboni kwake.

Zilianza kupigwa Takbir utadhani Bunge ni kikao cha shura ya Maimamu, nawaomba radhi ndugu zangu Waislamu msinielewe vibaya, mkiendelea kuruhusu hali hii kila siku mtaendelea kulalamika maana Mwigulu ambaye ni Mkristo hana gutts za kuwaghalamia na kuwalaghai mapadri au wachungaji 69 kuwaleta Bungeni, kwanza hawana muda huo.
 
nilimuona waziri Philip Mulugo akitambulisha jana mpaka nikaona kinyaa kusema kweli, anamtaja mpaka dereva na haishii tu hapa bali ni jinsi gani anaendesha gari!!! Sema waziri wake (Kawambwa) alimtaja tu Mungu na campaign manager wake tu na niliipenda.
Mimi naona hata kumshukuru Mungu bado ni makosa kwa sababu kabla kikao hakijaanza ZINASEMWA SALA lakini kinachoonekana hawa watu hawaiamini ile sala inayosemwa na ndio maana wanarudia rudia "kumshukuru Mungu"!

Alafu Mzee Cheyo mwishoni anataka kutoa taarifa Zungu ambayo labda ilikuwa muhimu lakini anakataa bila kujua kuwa mnaweza kuwa mnajadili tatizo mwezi mzima bila kukoma lakini jibu akaja kulitoa mtu mmoja tu mwishoni. Maana huyu ndiye alitoa hoja kuwa zaidi ya 70% ya pesa haziendi kwenye elimu bali ni posho za viongozi na wakaguzi.
Tatizo la hawa 'waheshimiwa' wamejikita kwenye desturi za uendeshaji na ufanyajiu wa mambo na kusahau UKWELI wa mambo yenyewe. Inasikitisha!!
 
Hii hoja ya MR DEO ni ya ukweli sana hasa yule WAZIRI NANILIU ana penda sana swaga hizi...safi sana DEO
 
1.hiyo kutaja mlolongo wa wachangiaji ni kufuja muda
2.kutoa shukrani kwa mke, mume watoto vimada, wajomba , bibi babu, shangazi ni kufuja muda
3.kutaja mlolongo wa wageni waliofika bungeni ni kupoteza muda
4. Kupigana vijembe na taarabu bungeni na kupiga meza muda mrefu ni kufuja muda

Kifupi bunge letu halina discpline ya muda hata kidogo na ni kutokana na udhaifu wa kiti cha speaker ambacho nachelea kusema kipo wazi tangu alipoondolewa mzee wa speed na viwango

Unatarajia nini kutoka kwa mbunge anayeshindwa kuweka tick sehemu sahihi na kura yake ikaharibika kama ilivyo tokea juzi? Kuna vihiyo wengi bungeni,ndiyo sababu ujinga,mizaha na utani wa kitoto ni mambo ya kawaida huko.
 
Ina maana huyu spika hakuliona hili mpaka akumbushwe na Deo Fili, mbona sisi (Watazamaji) tumeanza kuhoji ujinga huu toka kitambo tu.
 
Unatarajia nini kutoka kwa mbunge anayeshindwa kuweka tick sehemu sahihi na kura yake ikaharibika kama ilivyo tokea juzi? Kuna vihiyo wengi bungeni,ndiyo sababu ujinga,mizaha na utani wa kitoto ni mambo ya kawaida huko.
Ndio mliwachagua wenyewe
 
Ni upuuzi kufikiri eti kupunguza muda wa kuongea bungeni ni sawa na kuongeza ufanisi, hii ni sawa na kusema kuwa hakuna haja ya kuwa na bunge kabisa maana hata huo muda kidogo wanaotumia kuongea wangeweza kuutumia kutenda kazi zaidi jambo ambalo lingekuwa athariza moja kwa moja kwenye ufanisi. Bunge la sasa limejaa masupa staa wanaofanya kila linalowezekana kuwa kurasa za mbele kuliko kufanya majukumu yao ya msingi.
Ndio sababu yenu kuu ya kutaka Bunge lisioneshwe Live ili mpate muda hadi wa kupeana asante za muheshiwa fulani kuhudhuli kitchen party ya binti yako?
 
Back
Top Bottom