Deni la Taifa: Kutoka trilioni 10.5 hadi trilioni 14.4 kwa mwaka?

Hahaaaaa eti watakuja kutuwowa???? Msinifanye nilale njaa mie kwenye haka kamshahara kangu ka KCC nijikwamue nilipe hilo deni.
 
nielekezwe nchi wanayotunadai na nitawalipa hela yao moja kwa moja.
siwezi wapa pesa yangu hawa wezi ccm tena!
 
Utakutana na wapumbavuu wa chama wakishabikia deni likue, lipeni sasa nyinyiemu; faizyfox uko wapi na hili deni wakati hatujui wanakopa kufanya nini??? kila siku kodi tunalipa deni la nini au kuna mwaka tulisamehewa kulipa kodi nchi nzima???
 
Kiu kwel den la taifa linaskitishaaaa sana watanzania tunabebeshwa mzigo ambao hatu ujui. Watu wana kufaa na njaa kumbe tunadaiwa mapesa ambayo hatuyajui hayo mapesa tunadauwa vp.
 
Kiu kwel den la taifa linaskitishaaaa sana watanzania tunabebeshwa mzigo ambao hatu ujui. Watu wana kufaa na njaa kumbe tunadaiwa mapesa ambayo hatuyajui hayo mapesa tunadauwa vp.

Ukizingatia pato la watanzania ni sh laki 6 kwa mwaka .tena sio kwa hard cash ni kwa kuhesabiwa mahindi na maharage na uvunaji wa kuni za kupikia kande.
 
Hii ndio kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania. Kila tukiwaambia msiichague ccm hamsikii. Wanawahonga:
1. WALI-Kwenu hamuli?
2. MASHATI/SKAF/FULANA-Kwenu hamvai?
nasikia sasa wanaandaa na vy-pi ili mfaidi zaidi
 
Habari zenu wana jukwaa,natumai wote mnaendelea poa na ujenzi wa taifa letu,
Leo nimeamka nikiwa nafikiria mshahara wangu ni ugawe gawe vipi angalau unifikishe kati kati ya mwezi ujao,wakati nawaza haya nikachoshwa na taarifa za vyomba vya habari, "KILA MTANZANIA ANADAIWA SI CHINI YA LAKI SITA KATIKA DENI LA TAIFA LINADAIWA KUFIKA TRILION 27"
Japo sijawahi kujua lini nilishawahi kwenda kukopa serekalini,wakat ukienda hospital nalipia ili nitibiwe,wanangu huko shule ya msingi bado kuna vimichango vya hapa na pale,Nashindwa kuelewa hamna siku niliyovuka pale kigamboni na pantoni bila kuchangia,hamna cku niliyopata maji ya bure kwangu,au ofa kutoka tanesco kutumia nishati yao bila kulipia.
WADAU MIMI HILI DENI LINANIUZUNISHA SABABU SIPENDI KUDAIWA

Related story NIONYENI ZILIPO OFC WANAZOKUSANYIA DENI LA TAIFA NKAPUNGUZE DENI john ze don facebook

attachment.php


...kukopa wa kope wao, na kulipa' tulipe sisi...!
 
huwez kubisha kulipa wakat unakatwa kodi kila siku...kwa bidhaa unazonunua na bado direct tax kwenye mshahara kama ni muajiriwa
 
baadhi ya viongozi ni mizigo, na hata mfumo wa serikali pia ni mbovu. nnchi yangu sijui inapelekwa wapi na hao mabwana. si ajabu hadi mimba nayo inadaiwa
 
Mbona hiyo chamtoto.soma hapa chini.
Outstanding public debt of USA as of 30january 2014 at 07:45 am GMT IS.
Usd 17,275,429,380,978.01.

The US population is 317,541,193 so each citizen's share of this debt is USD 54,403.74.
The national debt has continued to grow on average of USD 2.49 billion per day since september 30,2012.

Kwamaana ingine kila mmarekani anadaiwa kama shiling za kitanzania milioni 90.
Na deni linakua kwa siku kwa shilingi kama trilion 4...huh!!

Marekani deni hilo wanadaiwa na nchi gani? Ninachofahamu deni hilo ni la ndani ya nchi, hivyo hata riba ambayo italipwa inaingia ndani ya mzunguko wa ndani ya nchi na kuendelea kuimarisha uchumi wao.

Tanzania kila tunachochuma tunachumia nchi zinazotukopesha, plus riba, umeona tofauti ya deni la Tanzania na Marekani?
 
Hilo deni watanzania mpende msipende mtalipa tu! Dr Slaa anapowaambia kuwa mabomba ya gesi yanaelekea Ulaya ni watanzania wachache sana (tena wenye mang'amuzi mapana) ndio watakaoweza kumwelewa!
 
Inadaaiwa jamhuri bana wasituvuruge na takwimu. Biashara na mwenyebiashara ni vitu viwili tofauti.
 
Back
Top Bottom