Deni la Taifa: Kutoka trilioni 10.5 hadi trilioni 14.4 kwa mwaka?

tatizo bado kuna utata wapinzani tunaotarajia kuwapa nchi 2015 mbona wamejipitishia mafao mil 160?
kama pesa zinagawanywa namna hiyo unategemea deni la taifa lisiongezeke?
 
Sasa deni la Tanzania limefika Trilioni 22 sasa tunaambiwa tunadaiwa sasa kwani ile misaada Jk anayopitisha bakuli ndo madeni haya au kuna kwingine wanakokopa? Kwa matumizi ya nani?

Source: Star tv habari

============

Jan 2014:

Kila raia Tanzania anadaiwa 600,000/-. Deni la Taifa lafikia trillion 27.04
e

JK alisema wafadhili lazima uwafuate kwenye nchi zao. Serikali inashindwa kukusanya kodi , inashindwa kubana matumizi, wizi umekidhiri , bajeti za ubabaishaji , hii deni ndio matokeo yake
 
Hapa nina wasiwas yawezekana kabisa
wizara ya Fedha wanataka kucheza mchezo ili watafute hela ya uchaguz maana naskia ccm wapo taaban kifedha
 
Tunakopa pesa kutoka ulaya kisha zinaingia mifukoni kwa majamaa flani then zinapelekwa Uswisi bila kufanya kazi iliyokusudiwa mwisho wa siku tunajikuta tuna deni ambalo ni = (Interest rate+Pesa ambayo wanajifanya hawajui iliko). Now that is Fcuked up!
 
Rais JK ameamua kuwa Promota wa muziki wa Bongofleva baada ya kuona hili deni halilipiki na nchi imerudi katika kundi la HIPC,,, Mkapa alijitahiti kututoa katika Hilo kundi, Promota katurudisha.
 
Nahisi kuhama. duniani nani anapokea deni nalodaiwa maana yawezekana nikaondoka hapa TZ kabla sijalipa deni langu.
 
Au tuzaane sana ili deni lipungue? Mungu usitucgukue waja wako deni litaongezeka!
 
nimekuwa nikimsikiliza mwigulu mchemba (mbunge wa ndagu, singida) Leo asubuhi kupitia clouds fm, akitoa ufafanuzi wa kila mwananchi kudaiwa laki 6 na deni la taifa kuwa kubwa.
kiukweli amezungumza kisiasa Sana kana kwamba wananchi watanzania wote Ni wajinga kwa kuwa kwa ufafanuzi huo kila mmoja ataridhika. Amesema wakati anaondoka mkapa deni la taifa aliloliacha lilikuwa dola bilioni 5 (5B US$) na mpaka sasa limefikia dola bilioni 20s, kwa maana hiyo limekuwa Mara nne ya lile,

ameeleza kuwa watanzania wao ndio wenye uamuzi WA kukopa au kuacha kukopa, kwa maana ya kwamba, kipindi cha nyerere deni la taifa lilikuwa dogo Sana na pia maendeleo yalikuwa kidogo, hasa kwenye miundombinu kama kilomita za barabara yenye lami zilikuwa chache, hali kadhalika kwenye awamu ya mkapa.

Hii awamu ya kikwete deni la taifa limekuwa kubwa, kwa sababu maendeleo yameongezeka, akatoa mfano WA barabara pia, kuwa kilomita zenye lami zimeongezeka maradufu sambamba na kukuwa kwa deni la taifa.

sasa swali la kujiuliza, Je, maendeleo ya Tanzania yanategemea na yatategemea mikopo Tu?, hii nchi haina vyanzo vingine vya kipato mpaka wakakope?, Je, hizo kodi tunazolipa zinafanyiwa nini?, na zaidi hilo deni tunalodaiwa linafanana na hatua ya maendeleo tuliyonayo?.

na kama Ni hivyo basi, tusiendelee kulipa kodi, Bali tuendelee kukopa, na rasilimali zote nchini zikabidhiwe wananchi ili wazalishe walipe deni, maana serikali imeshindwa kuzitumia, na imebaki kukopa Tu.
nawasilisha.
 
Si ajabu haujawahi kutoka nje ya Dar Es Salaam ndiyo maana unabwabwaja tu hapa jukwaani.

Tembea uone maendeleo yanayoletwa na serikali ya CCM.
 
Serikali ya United States of America inakopa ndiyo ushangae serikali ya Tanzania kukopa?

Jitahidi kusoma vitabu vya maana ili urutubishe ubongo wako.
 
Sumu, nimewasilisha kile alichokisema mwigulu, na nikahoji reason ya yy kusema kuwa maendeleo ya nchi Ni lazima yategemee ukopaji, binafsi sijapinga kukopa lakini sio kwa kiwango hicho. Alaf ndugu siyo kila kinachofanywa na USA Ni sahihi, na nikiwa kama mwananchi WA tz Nina haki ya kuhoji, kama wewe umenufaishwa na hayo madeni basi Mimi nimenyonywa.

kitu kingine maendeleo unayoyaona sasa yalitakiwa yawe yamekwisha fikiwa tokea miaka ya 90 siyo Leo.
...vitabu unavyoniambia nisome havinijengi kwa sababu uhalisia ninauona, so why nikasome kitabu wakati halo halisi ninaiona, PIA usidhani Mimi Ni mtu WA kukurupuka kama ulivyo wewe kwenye mlengo WA kisiasa.

badilika.
 
Last edited by a moderator:
...ni mikoa minne Tu tz ndo sijafika, ninaijua tz kuliko ulivyo wewe, dsm mi Ni wakuja Tu Sumu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom