Deni la Taifa: Kutoka trilioni 10.5 hadi trilioni 14.4 kwa mwaka?

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Nilikuwa nasoma ripoti za CAG zinaonyesha kuwa deni la taifa limeongezeka kutoka trilioni 10.5 mwaka 2009/10 hadi trilioni 14.4 mwaka 2010/11. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 38 kwa mwaka. Nashangaa deni la taifa kuendelea kukua tena kwa kasi kubwa sana wakati miradi mingi nchini haina fedha. Hivi huwa tunakopa kwa matumizi gani? Wakati tunakopa huwa tunafikiria vizazi vinavyo?

Ama kweli deni la taifa litatupa matatizo makubwa sisi wote na vizazi vijavyo maana tunakopa tuu lakini miradi ya maendeleo haina pesa. Wakati huo huo, Waziri Mkuu Pinda anatuambia, kutokana na ukata, serikali imeagiza kusimamishwa kwa matumizi yasiyo ya lazima. Kwamba, tubane matumizi kweli kweli ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida. Sijui kuhusu shughuli za miradi ya maendeleo.

Kuna umuhimu wa kuwa na kikomo cha kukopa. Hatuwezi kuendelea kukopa tuu bila kufikiria vizazi vijavyo watalipaje. Kuna mdau humu alishashau kuweka deni la taifa kwenye Katiba kwa kutumia GDP kupiga hesabu ni kiasi gani kiwe cha mwisho kukopa kwa mwaka kutokana na uwezo wetu kama nchi (debt ceiling).

Whether or not ni wazo zuri kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na kikomo cha kukopa. Vingenevyo vizazi vijavyo vitaishia kuwa watumwa wa kulipia madeni yetu ambayo mengi tumekopa kwa sjili ya kujikidhi sisi wenyewe bila kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo kwa faida ya vizazi vijavyo.

---------------------

June, 21.

Tanzania: Deni la taifa lafikia Sh. Trilioni 20!


Deni la taifa limefikia zaidi ya Sh. Trilioni 20 mwishoni mwa mwaka huu, lakini Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa amesema hakuna sababu ya kupaniki kwa kuwa sehemu kubwa ya deni hilo limewekezwa kwenye miradi ya nishati na maji.

Dkt. Mgimwa amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Tanzania ilipata mkopo wa karibu sh. trilioni moja kutoka China kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar Es Salaam.

Amesema kuwa mradi huo ukikamilika utazalisha nishati zaidi na kwa gharama nafuu. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 ijayo.

Pia amesema Tanzania imepokea dola za Kimarekani milioni 178.2 kwa ajili ya mradi wa maji Ruvu, kwa hiyo hakuna haja kuogopa kuongezeka kwa deni la taifa.

Some reflections

[video=youtube_share;T3wgDb2PRAI]http://youtu.be/T3wgDb2PRAI[/video]


------------------------

Jan, 2014.


Kila Mtanzania bila kujali kama ni mtoto, mzee au mfanyakazi anadaiwa Sh. 600,000 miongoni mwa watu milioni 45 raia wote wa Tanzania.

Hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa deni la Taifa kufikia Dola za Marekani bilioni 17.10 (Sh. trilioni 27.04 hadi kufikia Desemba mwaka jana.

Kwa mtumishi wa serikali anayelipwa kima cha chini cha Sh. 150,000 kwa mwezi atatakiwa kulipa deni kwa miezi minne mfululizo bila kubaki na chochote.

Deni hilo ni bajeti ya serikali ya mwaka mmoja na nusu kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2013/14 ya Sh. trilioni 17.7.

Kati fedha hizo, Dola bilioni 12.79 (Sh. trilioni 20.23) ni deni la nje na la ndani ni Sh. trilioni 6.81.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo.

Hata hivyo, alisema pamoja na kuongezeka kwa deni hilo, serikali itaendelea kukopa kwa sababu bado ina sifa za kukopa kwa kuwa kiwango cha deni ni asilimia 28 wakati ukomo wa kukopa ni asilimia 50.

Aliongeza kuwa itakopa fedha kwa masharti nafuu ambazo zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya miundombinu ambayo aliitaja kuwa ni barabara, reli, bandari, mkongo wa Taifa, bomba la gesi, viwanja vya ndege Zanzibar na Songwe.

Waziri Mkuya alifafanua kuwa sababu za kuongezeka kwa deni ni mikopo iliyopokelewa na serikali ambayo muda wake wa kulipa haujafika kutoka vyanzo vya masharti nafuu na ya kibiashara na malimbikizo ya deni la nje kiasi cha dola za Marekani milioni 801.7 kwenye nchi zisizo wanachama wa jumuiya ya wahisani.

Aliongeza kuwa serikali itajadiliana na nchi hizo kuhusu msamaha wa kufutiwa deni hilo.

Alisema Serikali inatoa kipaumbele kwa miradi ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi ili kuiwezesha kuchangia maendeleo ya uchumi na kuipunguzia serikali mzigo wa madeni.

Alisema Septemba mwaka jana serikali kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa ilifanya thathmini kuangalia uhimilivu wa deni la taifa kwa kutumia vigezo vilivyowekwa na kutambuliwa kimataifa na kwamba ilionyesha deni ni himilivu kwa sababu viashiria vyote bado viko chini ya ukomo unaotakiwa.

MATUMIZI YA EFD
Akizungumzia matumizi ya mashine za kielektroniki EFD, alisema wataendelea kuyazitolea ufafanuzi na kuyasimamia vema kwa madhumuni ya kukusanya kodi kwa ufanisi zaidi ili kuongeza pato la taifa na kupunguza ukwepaji kodi.

Alisema serikali itaendelea kutoa elimu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa wafanyabiashara kwa kuwa huo ndiyo msimamo wa serikali. Alifafanua kuwa serikali iliwapa uhuru wafanyabiashara wanaolalamikia mashine hizo kuunda kamati na kwenda kutembelea nchi za China na Bulgaria zinapotengenezwa na kuangalia uhalisia wa bei, lakini walikataa.

Kuhusu ukuaji wa uchumi, Mkuya alisema umekua kwa kiwango kikubwa na unaendelea kuimarika kwa wastani na kwamba pato la taifa lilikuwa kwa asilimia saba kwa kipindi cha miezi tisa ya mwanzo wa mwaka 2013.

MFUMUKO WA BEI

Kwa upande wa mfumuko wa bei, alisema umeendelea kushuka hadi asilimia 5.6 Desemba mwaka jana kulinganisha na asilimia 19.8 mwaka 2012. Alisema kupungua kwake kulitokana na sera thabiti za fedha na kibajeti pamoja na kuimarika kwa uzalishaji na usambazaji wa chakula.

Alisema matumizi ya fedha za kigeni katika mzunguko wa uchumi Mtanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yoyote nchini kwa fedha hizo isipokuwa sehemu za utalii na ada za shule za kimataifa.

Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia vyema suala hilo ikiwamo kuwachukulia hatua wanaokiuka utaratibu huo.

SARAFU MOJA EAC
Akizungumzia matumizi ya sarafu moja kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mkuya alisema wanaendelea na mchakato na watalipeleka bungeni kwa majadiliano zaidi kabla ya maamuzi.

Akizungumzia Bunge la Bajeti, alisema licha ya kufanyika kwa Bunge la Katiba, wanatarajiwa kuwa bajeti itawasilishwa, kupitishwa na kuanza kutumika Julai Mosi, mwaka huu, lakini alisema kama kutakuwapo na viashiria, serikali itatoa taarifa.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya wanasiasa wanaohoji uwezo na uzoefu wake wa kusimamia wizara hiyo, alijibu kwa kifupi kuwa hataki maswali hayo kwani ni historia na kwamba Rais Jakaya Kikwete amekwisha kumteua na anaendelea kuchapa kazi.

Kuhusu madai ya baadhi ya watumishi wa serikali na watoa huduma serikalini, alisema tatizo liko katika halmashauri kwa kuwa fedha zinatumwa na kuwa kinachofanyika ni uzembe. Hata hivyo, Mkuya aliahidi kwamba serikali itafuatilia.
 
Katika kujadili ripoti mbalimbali bungeni leo, mbunge mmoja amesema kuwa kama deni la taifa ikigawanywa kwa kila mtu including watoto, kila mtu atakuwa anadaiwa milioni 350​


 
Leo bungeni:
Deni la trilion 14 zionyeshwe zimefanya nini kwa watanzania!
Deni linaongezeka kwa asilimia 39
Uchumi unadaiwa kukua kwa asilimia 6
Lakini serikali inatumbia tukaze mikanda
Wabunge leo wamechachamaa
 
Kukotona na deni la taifa kuendelea kuongezeka kwa speed kubwa, mahesabu yaliyofanywa na mbunge mmoja bungeni anadai kila Mtanzania, wakiwemo watoto, anadaiwa kiasi cha sh millioni 350. Wamegawanya deli hilo ambalo ni trilioni 14.4 kwa kila mtanzania takribani watanzania milioni 40.

Kwa hiyo, kila mtu aanze kulipa deni lake.
 
Tunaposikia usemi nchi imeuzwa pamoja na wananchi wake plus viongozi wenyewe sio utani.
Sasa wakitaka hela yao leo haturudi kwenye ukoloni?
 
EMT ipo siku nchi hii ikifika kutokukuposheka nadhani hali itakuwa mbaya sana, hasa kama serikali ya CCM itang'ang'ania madarakani.
 
Yaani najaribu kuangalia hili deni langu na kulinganisha na nilichonacho sipati picha. Sina mali ila nna deni la mil 350, duh kuwa uyaone wallah !
 
Kukotona na deni la taifa kuendelea kuongezeka kwa speed kubwa, mahesabu yaliyofanywa na mbunge mmoja bungeni anadai kila Mtanzania, wakiwemo watoto, anadaiwa kiasi cha sh millioni 350. Wamegawanya deli hilo ambalo ni trilioni 14.4 kwa kila mtanzania takribani watanzania milioni 40.

Kwa hiyo, kila mtu aanze kulipa deni lake.

EMT,
Mwambie huyo mbunge akajifunze kwanza hesabu za kuzidisha na kugawa.

Hilo deni linatakiwa kuwa karibu laki tatu na nusu kwa kichwa na wala sio milioni 350.

garbage in garbage OUT
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Issue siyo kulipa deni. Issue ni kwamba hiyo hela ilikopwa wapi na kwa madhumuni gani? Na je, imetumika kama ilivyotarajiwa? Tumesikia ubadhirifu mkubwa wa matumizi mabaya ya fedha ya wananchi.
 
Hivi waliokopa bank kwa madhumuni ya mtaji wa kibiashara wa million 50 tu in sawa kugawana Hilo Deni kwa watoto wako wakati mtaji huo unatumika kutunisha biashara zako? With politics we undermine our capacities to see the visible objects. God help us to be more objective for our lives and our world.
 
Kukotona na deni la taifa kuendelea kuongezeka kwa speed kubwa, mahesabu yaliyofanywa na mbunge mmoja bungeni anadai kila Mtanzania, wakiwemo watoto, anadaiwa kiasi cha sh millioni 350. Wamegawanya deli hilo ambalo ni trilioni 14.4 kwa kila mtanzania takribani watanzania milioni 40.

Kwa hiyo, kila mtu aanze kulipa deni lake.
sijui ndo athari za shule za kata...na wewe umechukua hiyo hesabu kama ilivyo?
 
Serikali yetu haina akili wala maarifa ya kutusaidia kufika tunakokwenda salama. Tunaposikia habari kama hizi, maumivu yanaingia rohoni kama nameza tindikali.
 
Sasa deni la Tanzania limefika Trilioni 22 sasa tunaambiwa tunadaiwa sasa kwani ile misaada Jk anayopitisha bakuli ndo madeni haya au kuna kwingine wanakokopa? Kwa matumizi ya nani?

Source: Star tv habari

============

Jan 2014:

Kila raia Tanzania anadaiwa 600,000/-. Deni la Taifa lafikia trillion 27.04
 
Back
Top Bottom