Magulumangu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 3,047
- 455
- Thread starter
- #61
Naona mwanisifia, tungo mwazifurahia
Mwasema ziko sawia, na tena mmeridhia
Vina mwaniambia, hakika vinatishia
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Kutunga nilitamani, toka zama za zamani
Labda sikujiamini, ningeanzaje jamani
Leo nipo furahani, najaribu hii fani
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Ni kweli sijakomaa, ningali ni mwanafunzi
sitokata na tamaa, nipate mwingi ujuzi
Mola nipe shufaa, ili niwe mkufunzi
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Msaada mnipatie, enyi mliobobea
Msiniache nikimbie, bahari kuogelea
Kweli mnisaidie, tungo zisije pelea
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
shuka mwana wewe shuka,tungo zako zi sawia,
kamwe hutoteremka,hapo ulipo kawia,
si wote tu mauruka,sifazo kukusifia,
mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,
muite klorokwini,aspirini na mangu,
mwanakijiji hayani,kamwe hao ndio mwangu,
lizi aso kibindoni,judi asiye kiwingu,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,
sijakutembo mkuu,nisje litia maji,
mweka we mpaka majuu,malenga wetu si maji,
lijua neno kajuu,malenga ndio mtaji,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu....