Dear mama....

Naona mwanisifia, tungo mwazifurahia
Mwasema ziko sawia, na tena mmeridhia
Vina mwaniambia, hakika vinatishia
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

Kutunga nilitamani, toka zama za zamani
Labda sikujiamini, ningeanzaje jamani
Leo nipo furahani, najaribu hii fani
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

Ni kweli sijakomaa, ningali ni mwanafunzi
sitokata na tamaa, nipate mwingi ujuzi
Mola nipe shufaa, ili niwe mkufunzi
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

Msaada mnipatie, enyi mliobobea
Msiniache nikimbie, bahari kuogelea
Kweli mnisaidie, tungo zisije pelea
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

shuka mwana wewe shuka,tungo zako zi sawia,
kamwe hutoteremka,hapo ulipo kawia,
si wote tu mauruka,sifazo kukusifia,
mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,

muite klorokwini,aspirini na mangu,
mwanakijiji hayani,kamwe hao ndio mwangu,
lizi aso kibindoni,judi asiye kiwingu,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,

sijakutembo mkuu,nisje litia maji,
mweka we mpaka majuu,malenga wetu si maji,
lijua neno kajuu,malenga ndio mtaji,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu....
 
Malenga bado mpo kumbe....

Ngoja nikakariri kamusi kwanza

Yakuonea ndo anaunguruma wengine kimya....wapi malenga wetu?mie nakesha nakula misamiati mkuu maana hapa usipoangalia utakuwa unarudia maneno tuu bila jipya lolote hahahha
 
Naona mwanisifia, tungo mwazifurahia
Mwasema ziko sawia, na tena mmeridhia
Vina mwaniambia, hakika vinatishia
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

Kutunga nilitamani, toka zama za zamani
Labda sikujiamini, ningeanzaje jamani
Leo nipo furahani, najaribu hii fani
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

Ni kweli sijakomaa, ningali ni mwanafunzi
sitokata na tamaa, nipate mwingi ujuzi
Mola nipe shufaa, ili niwe mkufunzi
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

Msaada mnipatie, enyi mliobobea
Msiniache nikimbie, bahari kuogelea
Kweli mnisaidie, tungo zisije pelea
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia

Karibu upite ndani, ewe ndungu wa fani
Sasa umo hesabuni, jiskie wa nyumbani
Tujumuike kundini , JF furahani
Wala sijione duni, huna hata mpinzani

Changamoto ninakupa, tena usiipuuze
Sredi moja ungetupa, nasi tuiendeleze
Hapa tuchape lapa , sifa za mama tutunze
Ombi usijelikwepa, twaomba utekeleze

Chagua mada yoyote, igusayo moyo wako
Wakijiji umchote , ajibu mapigo yako
Magulumangu atete, nitaweka kiitiko
Aspirin avue pete , tukuvike taji lako

Uzi tunausubiri , mimi na Judith pia
Lizzy nae ni mahiri, hakika atachangia
Shossi nae ni hatari, hii fani kabobea
Nawe wako ujasiri , kofia nakuvulia

hehehe Yakuonea sasa tunaomba sredi yako ya mistari
 
Magulu nimekupata, ujiko kunimwagia
Ila hapa ninasita, ukuu kunipatia
Fani ni sawa na vita, kifani sijatimia
Nduguyo yakuonea, kifani bado mchanga

Wakongwe nitawashika, niwe nanyi sambamba
Msije kukasirika, nitakuja hata shamba
Lengo likikamilika, ghani zangu zitatamba
Nduguyo yakuonea, kifani bado mchanga

shuka mwana wewe shuka,tungo zako zi sawia,
kamwe hutoteremka,hapo ulipo kawia,
si wote tu mauruka,sifazo kukusifia,
mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,

muite klorokwini,aspirini na mangu,
mwanakijiji hayani,kamwe hao ndio mwangu,
lizi aso kibindoni,judi asiye kiwingu,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,

sijakutembo mkuu,nisje litia maji,
mweka we mpaka majuu,malenga wetu si maji,
lijua neno kajuu,malenga ndio mtaji,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu....
 
Wakuu ninasimama, heshima kuwapatia
Napenda zenu hekima, lengo kunisaidia
Na kila nikitazama, siwezi kuwafikia
Changamoto nimepata

Mimi bado maamuma, kutembea sijaweza
Si kama narudi nyuma, Uzi kweli nitaweza?
Ndugu zangu sijagoma, ila sitaki jikweza
Changamoto nimepata

Ukaidi sijafanya, naomba mnielewe
Mwaweza hata nikanya, tusigombane wenyewe
Kifani sijachanganya, nitarusha vipi mawe
Changamoto nimepata

Muda ukifikia, uzi nitawatumia
Msije acha changia, mawazo yenu kutia
Kweli nimeweka nia, kloro fuatilia
Changamoto nimepata

Karibu upite ndani, ewe ndungu wa fani
Sasa umo hesabuni, jiskie wa nyumbani
Tujumuike kundini , JF furahani
Wala sijione duni, huna hata mpinzani

Changamoto ninakupa, tena usiipuuze
Sredi moja ungetupa, nasi tuiendeleze
Hapa tuchape lapa , sifa za mama tutunze
Ombi usijelikwepa, twaomba utekeleze

Chagua mada yoyote, igusayo moyo wako
Wakijiji umchote , ajibu mapigo yako
Magulumangu atete, nitaweka kiitiko
Aspirin avue pete , tukuvike taji lako

Uzi tunausubiri , mimi na Judith pia
Lizzy nae ni mahiri, hakika atachangia
Shossi nae ni hatari, hii fani kabobea
Nawe wako ujasiri , kofia nakuvulia

hehehe Yakuonea sasa tunaomba sredi yako ya mistari
 
Wakuu ninasimama, heshima kuwapatia
Napenda zenu hekima, lengo kunisaidia
Na kila nikitazama, siwezi kuwafikia
Changamoto nimepata

Mimi bado maamuma, kutembea sijaweza
Si kama narudi nyuma, Uzi kweli nitaweza?
Ndugu zangu sijagoma, ila sitaki jikweza
Changamoto nimepata

Ukaidi sijafanya, naomba mnielewe
Mwaweza hata nikanya, tusigombane wenyewe
Kifani sijachanganya, nitarusha vipi mawe
Changamoto nimepata

Muda ukifikia, uzi nitawatumia
Msije acha changia, mawazo yenu kutia
Kweli nimeweka nia, kloro fuatilia
Changamoto nimepata

Wala tena usihofu
Ombi sio msahafu
Muhimu usistaafu
Komaa na uzoefu

Ukitoa tutajibu
Ila hiyo si wajibu
Lakini ukijaribu
Utakifunga kitabu

Ukisubiri tuanze sisi
Wengi wetu ni waasi
Uzi kuanzisha si rahisi
Ni kaskazi hadi kusi

Lakini tupo pamoja
Japo tunajikongoja
Ipo siku itakuja
Tutaja kuvika koja
 
Thanx mkuu, elewa kwa kila beti unayoandika basi hiyo kwangu ni changamoto, na ninajifunza mengi kutoka kwenye beti zenu, i have some difficulties here and there but it is also good to see that i can at least add some value to this fani - much appreciation

Wala tena usihofu
Ombi sio msahafu
Muhimu usistaafu
Komaa na uzoefu

Ukitoa tutajibu
Ila hiyo si wajibu
Lakini ukijaribu
Utakifunga kitabu

Ukisubiri tuanze sisi
Wengi wetu ni waasi
Uzi kuanzisha si rahisi
Ni kaskazi hadi kusi

Lakini tupo pamoja
Japo tunajikongoja
Ipo siku itakuja
Tutaja kuvika koja
 
Nimeangalia watu wengi ambao wako kwenye fani ya ushairi nimeona wanamajina ya ushairi, mfano mzuri ni klorokwini na wengine wengi, hivyo na mimi kama mpenda mashairi nimeamua nitafute jina la kiushairi, na jina nitakalo tumia ni SINDANO YA GANZI, ninahisi labda klorokwini wewe ni mtu ambae uko kwenye fani ya madawa (sina uhakika na hili) na unaelewa vizuri umuhimu wa sindano ya ganzi,hivyo basi kwa wale wasio elewa undani wa sindano ya ganzi naweza kuandika mistari michache kuelezea umuhimu wake na kwa nini nimeamua kujipa jina hilo, labda siku za usoni naweza kuja kuandika kama kuna uhusiano wowote kati yangu na sindano ya ganzi kiuhalisia
 
Tunaisubiria mistari mkuu, jina limetulia kabisa. Magulumangu akiwapa dozi ya sindano ya ganzi, klorokwini na aspirin. kwisha habari yao! lol
 
JINA LA KISHAIRI

Mwenzenu nimefikiri, jina kujitafutia
Kwenye fani ushairi, niweze kulitumia
Pokeeni mistari, jina nawafunulia
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Sindano ile ya ganzi, sisi sote twaijua
Inafanya nyingi kazi, nani asiyetambua
Kupasua hauanzi, bila ganzi kupatiwa
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Ganzi itakufariji, pindi upasuliwapo
Utasikia baridi, tena hapo kwa papo
kutumima inabidi,hakuna njia mkato
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Maumivu utasikia, ganzi isipo tumika
Utaishia kulia, tena na kufadhaika
Ganzi yatusaidia, yabidi kuheshimika
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Sitaki tena fikiri, vipi isingekuwepo
Upasuaji nakiri, leo ungekuwa ndoto
Uliza madaktari, ganzi kweli kiboko
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Mshairi wenu
Sindano ya ganzi

Jina tumelipokea, na hati miliki yake
Limetulia!
Baraka twalimwagia, hii fani liiteke
Si nakwambia!

Maelezo umetowa, sababu ya kuchagua!
Imenoga!
Wa ganzi umekuwa, sindano isiyouwa
Umewakoga!

Sasa dozi wapatie, kutwa 2 mara tatu
Watapona!
Butwaa wakushangae, huyu ndie ganzi wetu?
Utawakuna!
 
Kloro ninashukuru, kwa jina kuliridhia
Wewe ni mwanga na nuru, mengi menisaidia
Tena hujui kufuru, na sasa tu ndugu pia
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi

Sijui ingekuwaje, jina ungelichukia
Jingine ningepataje, ganzi ningelililia
Ni furaha ilioje, kweli nalifurahia
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi

Kloro tukamatane, na mengi sasa tufanye
kwenye vita tupigane, ole wao mabwanyenye
Na tuwe kama mashine, ili tuwafinye finye
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi

Sindano ya Ganzi
 
Duu tusameheane ilikuwa kila nikijaribu kutuma post haiendi, kuja kuangalia post imejirudia rudia
 
Asprin yuko wapi, maana alipita hapa akaahidi kurudi sikumuona tena, mkuu magulumangu leo sijakusikia kabisaaa......lkn poa nipo klorokwini
 
Nimeangalia watu wengi ambao wako kwenye fani ya ushairi nimeona wanamajina ya ushairi, mfano mzuri ni klorokwini na wengine wengi, hivyo na mimi kama mpenda mashairi nimeamua nitafute jina la kiushairi, na jina nitakalo tumia ni SINDANO YA GANZI, ninahisi labda klorokwini wewe ni mtu ambae uko kwenye fani ya madawa (sina uhakika na hili) na unaelewa vizuri umuhimu wa sindano ya ganzi,hivyo basi kwa wale wasio elewa undani wa sindano ya ganzi naweza kuandika mistari michache kuelezea umuhimu wake na kwa nini nimeamua kujipa jina hilo, labda siku za usoni naweza kuja kuandika kama kuna uhusiano wowote kati yangu na sindano ya ganzi kiuhalisia

mkuu umeamua la maana, toka sasa jina lako Sindano ya ganzi...duhhh mkuu limetulia ile mbaya...
 
JINA LA KISHAIRI

Mwenzenu nimefikiri, jina kujitafutia
Kwenye fani ushairi, niweze kulitumia
Pokeeni mistari, jina nawafunulia
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Sindano ile ya ganzi, sisi sote twaijua
Inafanya nyingi kazi, nani asiyetambua
Kupasua hauanzi, bila ganzi kupatiwa
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Ganzi itakufariji, pindi upasuliwapo
Utasikia baridi, tena hapo kwa papo
kutumima inabidi,hakuna njia mkato
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Maumivu utasikia, ganzi isipo tumika
Utaishia kulia, tena na kufadhaika
Ganzi yatusaidia, yabidi kuheshimika
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Sitaki tena fikiri, vipi isingekuwepo
Upasuaji nakiri, leo ungekuwa ndoto
Uliza madaktari, ganzi kweli kiboko
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi

Mshairi wenu
Sindano ya ganzi

Sindano mwana wa ganzi,bila we chumba ki kimya,
nenda kule mi mbaazi,mhimbili kutofanya,
mwananyamara i hazi,sindano wataifanya,
Sindano hiyo na ipo,hata ya klorokwini,

umefunulia wengi,kwa jina la kishairi,
wasio na walo wengi,ganzi kote kushamiri,
hata ukubwa hujengi,ya ganzi kwa kutahiri,
Sindano hiyo na ipo,hata ya klorokwini,
 
Jina tumelipokea, na hati miliki yake
Limetulia!
Baraka twalimwagia, hii fani liiteke
Si nakwambia!

Maelezo umetowa, sababu ya kuchagua!
Imenoga!
Wa ganzi umekuwa, sindano isiyouwa
Umewakoga!

Sasa dozi wapatie, kutwa 2 mara tatu
Watapona!
Butwaa wakushangae, huyu ndie ganzi wetu?
Utawakuna!

sasa mkuu waja,
we noma,
kipindi kama mwaja,
si wakoma,
rusha mzee tu unguja,
si msoma,

Amejariwa yeye mwana,
kinoma,
jina le lina maana,
si kama,
Alianza kwa maana,
na tama,
 
Kloro ninashukuru, kwa jina kuliridhia
Wewe ni mwanga na nuru, mengi menisaidia
Tena hujui kufuru, na sasa tu ndugu pia
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi

Sijui ingekuwaje, jina ungelichukia
Jingine ningepataje, ganzi ningelililia
Ni furaha ilioje, kweli nalifurahia
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi

Kloro tukamatane, na mengi sasa tufanye
kwenye vita tupigane, ole wao mabwanyenye
Na tuwe kama mashine, ili tuwafinye finye
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi

Sindano ya Ganzi

duh mkuu unashine kama dhahabu...tutaandika kitabu chetu cha mistari mzee, ukiwa tayari nipo 24 saas.
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom