DCI Manumba: Kuna tishio la al-shabaab kushambulia Tanzania...

Status
Not open for further replies.

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Amewaomba watanzania wawe macho na tishio la kushambuliwa kwa nchi yetu...bila kusema tujihami vp tukae nyumbani tu au tufanyaje....
 
Alichokisema kinatokana na threat analysis waliyofanya,sasa tatizo ni kuwa tutashambuliwaje hilo si rahisi kufahamu mpk kuwa na reliable source of information.Katika lugha nyingine pilisi jamii inatumika hapa kwa kushirikisha umma endapo utaona jambo lolote lililo ndivyo sivyo basi utoe taarifa polisi (see something say something).kwa akili ya kawaida kabisa kama Nairobi wamepigwa mara mbili basi uwezekano wa sisi kupigwa pia upo.
 
Nairobi wamepigwa kwa sabau wameenda kuwachokoza wenyewe huko Somalia, sasa Manumba, Kova na wenzao watuambie kama na Tanzania imeenda kuwachokoza au ina mpango wa kuwachokoza, vinginevyo hakuna sababu ya kututisha ni kukukuza tu mambo bila sababu ya msingi
 
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini, DCI Manumba amesema kuwa Al-Shabaab hawawezi kuishambulia Tanzania kwa sababu ina jeshi imara na mfumo bora wa intelijensia. Lakini pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano pale wanapoona hali ya usalama inatishiwa na watu wasiofahamika.
Manumba amesema hayo kufuatia mashambulizi ya mfululizo ya wanamgambo wa Al-Shabaab yanayofanywa nchini Kenya.
Source:TBC News buletin,0800Pm

Je, kauli hii ya Manumba ina umakini wowote,na ni ya kuitumaini kwa kiasi gani?
 
Kuna kitu serikali yetu itakuwa imewafanyia hawa Al-shababy' kwani tangu jana wanazungumzia hiki! Watuambie wamewafanyia nini hao El-shababy!

Hakuna kitu chochote hapo wanatengeneza mazingira ya kuzuia maandamano ya amani kupinga ulipwaji Dowans
 
Upuuzi mtupu!!!!
Sasa Manumba kazi za kupeleka mafisadi mahakamani ameshindwa anaingilia swala la usalama wa mipaka!!
 
Tanzania Mungu anatulinda na atatuepushia na hili balaaaa.
 
Viongozi wa Tanzania nawashanga sana, Kova kakataza maandamano sababu ya Al-Shababu, Hivi uwezo wa jeshi la Wananchi JWTZ na Jeshi la Polisi upo wapi...? Kova na DC Manumba acheni kuonyesha Majeshi ya Nchi yanaudhaifu, ni Aibu
 
JWTZ ipo wapi mpaka polisi ndio itangazie uma kuhusu nchi kushambuliwa?
Polisi iache kutumika na CCM ishu hapo ni kupoteza watu malengo ili wasahau uozo unaoendelea kufanywa na serikali ya CCM.
 
Alichokisema kinatokana na threat analysis waliyofanya,sasa tatizo ni kuwa tutashambuliwaje hilo si rahisi kufahamu mpk kuwa na reliable source of information.Katika lugha nyingine pilisi jamii inatumika hapa kwa kushirikisha umma endapo utaona jambo lolote lililo ndivyo sivyo basi utoe taarifa polisi (see something say something).kwa akili ya kawaida kabisa kama Nairobi wamepigwa mara mbili basi uwezekano wa sisi kupigwa pia upo.

Kwani nairobi kupigwa ni lazima TZ tupigwe kivipi?
 
Hapa hakuna cha A-shabaab wala nini, ilikuwa inatafutwa sababu na kisingizio cha kuzuia maandamano ya kupinga malipo ya Dowans tu. Yote hii ni kwa sababu ccm ina mkono wake katika hayo malipo. Mwenye macho haambiwi tazama!!

Kweli mkuu umefikiria kwa kina, ccm wanataka kujifanya wajanja kumbe wanapokanyaga tushapita
 
Hakuna kitu chochote hapo wanatengeneza mazingira ya kuzuia maandamano ya amani kupinga ulipwaji Dowans

Nakubaliana nawe kama ulivyo andika hapo juu. Lakini kuna jambo jingine tena la msingi sana kwamba hawa magaidi na mashabiki wao wengi wapo hapa Tanzania. Na kichekesho utakuta akina Manumba hawajajiandaa,wamebakia kutupiga sounds kwamba nchi iko salama na vyombo vya usalama viko ktk high alert.
 
Tafadhali sahihisheni Manumba Robert ni DCI ( Director of criminal investigations) na sio DC ( yenye maana ya District Commissioner) wahusika rekebisheni title ilete maudhui sahihi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom