DCI Manumba: Kuna tishio la al-shabaab kushambulia Tanzania...

Status
Not open for further replies.
3.jpg

Waanze kumkamata huyu
 
yule wakala wao alishalipa ile laki
au ilikuwa ni danganya toto?
I hope vyombo vya ulinzi na usalama vinajipanga tutawasaidiaje jirani zetu wa Kenya. Kwa wale mnaodhani eti tusipo wachokoza hawatakuja kulipua Tanzania niwaulize sisi tulikua na ugomvi gani na Osama? Mbona watanzania wenzetu waliuliwa? Na Mtanzania mwenzetu amefungwa katika magereza ya Marekani kwa kuhusika katika tukio hilo. Hivi hamjuhi kwamba maharamia wa Kisomali kuna kipindi wanataka kuteka meli ktk bahari yetu? Mliwahi sikia majangili wa Kisomali waliokua wanateka watalii na wenyeji huko Ngorongoro? Tunapaswa kushirikiana na wenzetu wa Kenya kutafuta ufumbuzi wa kudumu. Tukikaa eti sisi hatuhusiki nawaambieni ndugu zangu haya tunayo sikia huko Kenya yatafanyika hapa.
 
Hapa hakuna cha A-shabaab wala nini, ilikuwa inatafutwa sababu na kisingizio cha kuzuia maandamano ya kupinga malipo ya Dowans tu. Yote hii ni kwa sababu ccm ina mkono wake katika hayo malipo. Mwenye macho haambiwi tazama!!

Message delivered to Manumba! Hamuwezi kudanganya watu wote, wakati wote!
 
Nijuavyo mimi hawa al shabab hawawezi kukushambulia bila ya wewe kuwafanyia jambo lolote, sasa serikali yetu ituambie wamewafanya nini hawa jamaa vinginevyo waache kututisha tuwe waoga ili tusahau shida zinazotukabiri ambazo serikali imeshindwa kututimizia
 
sio rahisi kama ufikiriavyo ndg
tuna cha kula cha kutosha na ile pesa ya rada na dowans tutazinunulia silaha...na watanganyika walivyo na mapenzi na nchi yao watatoa magari yao na mifugo na kujitolewa kuipigania nchi yao..hivyo usogope si uliona kule comoro alikufa mjeshi mmoja ingawa wengi wana vitambi
 
Hii kweli ni aibu ya karne kwa CCM,washadanganya mpaka wameishiwa. Uongo wa ghafla uliokuja mdomoni ni Al shabab nao wakabwabwaja. Au hii nayo ni moja ya maadhimisho ya miaka 50 ?
 
Hofu na mashaka ni kwenu mliolundikana DSM, sisi tuliopo mikoani hatuna hata wasiwasi na hao Al-Shabiby wenu. Acheni wawalipue tu ili mpate akili za kurudi kwenu mikoani. Watu wengine hamna hata ajira lakini mnajazana DSM tu, sasa mnategemea nini hapo? Ni kichapo tu kutoka kwa Al-Shabiby kudadadeki.
 
Naomba muwatangazie watalii waliotaka kuja Tz kuwa hali ni tete manake kuna tisho la Al Shabaab!

Au Al shabaab wanawalenga watanzania tu?
 
Tunashukuru kwa analizo lilotolewa na jeshi la polisi lililopelekea kukatazwa kwa maandamano kupingwa kwa malipo ya dowans lakini angalizo kwa selikali kisifanyike chochote kuhusu malipo ya dowans mpaka wanainchi tutimize adhma yetu hii ya kupinga huu uchakachuaji wa kodi zetu kama wanahitaji kufanya chochote basi nikufilisi na kuwafunga hawa magaidi wenye roho mbaya wanaotaka kutunyonya tulionyonywa na kuhamishia uchumi wa inchi yetu mifukoni mwao OLE WAO INCHI SIYO YA IONGOZI HII IFAHAMIKE HIVO.
 
anatuambia ili tufanyeje?????????
yeye ana intelegensia anayojisifia nayo sasa kazi kwake
 
Hili jambo hata mi sijamwelewa kabisa Manumba! Kenya imepeleka Jeshi lake Somalia kuwatafuta wale wahispania wa MSF ambao Kenya inadai wametekwa na Alshabab, na pia kuna matukio kadhaa nchini Kenya ambapo wametuhumiwa. Uganda na Rwanda zina majeshi yao kule Somalia. Sasa sisi hata siku moja hatujawahi kuwachokoza na hata wao hawajawahi kutuchokoza sasa watushambulie kisa nini! Alshabab sio machizi the have got missions to accomplish! Otherwise Serikali ituambie kwamba wana mpango wa kuwachokoza.
 
Amewaomba watanzania wawe macho na tishio la kushambuliwa kwa nchi yetu...bila kusema tujihami vp tukae nyumbani tu au tufanyaje....

Nadhani ni pamoja na kuwabaini watu ambao hawaeleweki katika maeneo yetu tunamoishi.
 
Hili jambo hata mi sijamwelewa kabisa Manumba! Kenya imepeleka Jeshi lake Somalia kuwatafuta wale wahispania wa MSF ambao Kenya inadai wametekwa na Alshabab, na pia kuna matukio kadhaa nchini Kenya ambapo wametuhumiwa. Uganda na Rwanda zina majeshi yao kule Somalia. Sasa sisi hata siku moja hatujawahi kuwachokoza na hata wao hawajawahi kutuchokoza sasa watushambulie kisa nini! Alshabab sio machizi the have got missions to accomplish! Otherwise Serikali ituambie kwamba wana mpango wa kuwachokoza.

Mkuu wamesema watawashambulia wakenya popote walipo, ina maana wakisikia Kuna wakenya Tanzania wanaweza kutushambulia, so mimi nadhani DCI hajakosea, ni suala la kuwa makini
 
Viongozi tuliobakinao nchi hii kwa sasa wana sifa Mbilli tu. 1. Kuropoka 2. Kulalamika a.k.a Kulialia. :doh::doh::doh:
 
Hofu na mashaka ni kwenu mliolundikana DSM, sisi tuliopo mikoani hatuna hata wasiwasi na hao Al-Shabiby wenu. Acheni wawalipue tu ili mpate akili za kurudi kwenu mikoani. Watu wengine hamna hata ajira lakini mnajazana DSM tu, sasa mnategemea nini hapo? Ni kichapo tu kutoka kwa Al-Shabiby kudadadeki.

aisee,bangi za usiku mbaya!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom