DC achakachua maoni ya wananchi juu ya Katiba Mpya

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Col. Issa Njiku, amechakachua maoni ya wananchi wa Missenyi kwa kuanzia na kata za Kyaka na Kilimililie ambako wananchi walipaswa kutoa maoni yao jana 16.7.2012.

Mkuu huyo kwa kushirikiana na makatibu wenezi wa CCM wa kata hizo, waliandaa karatasi maalumu zenye maoni ya kiserikali/CCM na kuzigawa kama njugu kwa wananchi na hayo ndiyo maoni yaliyowasilishwa kwa wajumbe wa katiba. Utaratibu wa kutoa maoni ulikuwa na mfumo wa aina mbili. 1. Kuwasilisha karatasi yenye maoni 2. kuzungumza moja kwa moja mbele ya hadhara.

Utaratibu wa 1, umetumika sana kwa maslahi ya CCM. Maoni hayo ya CCM/Serikali ya Njiku Missenyi yalisisitiza:
1. Uwepo wa serikali mbili- serikali ya Jamhuri na Serikali ya zanzibar
2. Rais aendelee kuwa na madaraka aliyonayo
3. wakuu wa wilaya na mikoa na watendaji wengine waendelee kuteuliwa na Rais
4.N.k.

Fomu yenyewe nitaiweka hapa baadaye.

Je, hali hii ni sawa? Huu utaratibu utawezesha tupate Katiba Mpya kweli?

Wajumbe wa Katiba wanahitaji kuchambua kwa makini na kuona kuwa fomu zaidi ya 2000 zina maoni yanayofanana, kitendo ambacho kinafanya zoezi zima kuwa hopeless.

Nawasilisha
 
ndio mana wabunge wa ccm wakiongozwa na ANNA KILANGO walikua wanang'ang'ania ma Dc wawepo kwenye mchakato wa kukusanya maoni, HILI HALIKUBALIKI HATA KIDOGO
 
Weka hiyo fomu tuisome ili tujue kuwa kumbe hii katiba mpya itakuwa ni changa la macho tu.
 
Duh! Tanzania, Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana,
Sitaweza kusahau mimi,
Mambo ya kipuuzi ya kwetu kabisa,
.............................
 
Kwa kweli hili halikubaliki na bila shaka kama kweli Tume ina wajumbe makini, wataona msululu wa maoni yenye kufanana maana kila fomu iliwasilishwa kwa Tume na chini yake jina la mtoa maoni liliandikwa kwa kalamu huku maandishi mengine yamechapwa kwa kompyuta.
 
Fomu yenyewe ndo hiyo kwenye attachment. Tazameni ni namna gani CCM na Serikali yake walivyoamua kwa gharama yoyote kubakiza Katiba hii yenye viraka.
 
hii taarifa haina ukweli.mimi nimeudhuria mikutano mingi sana nikiwa najitegemea,kuna kipindi nilikuwa narekodi nadhani hakuna jambo kama hilo.ebu weka hiyo form.kwa sababu karatasi zinagawiwa pale pale
 
tatizo kuna watu akilini mwao wameshakariri kabisa kuwa bila kutumia hila hawawezi kupewa nafasi walizo
nazo za kutawala na hawa ndo tunataka katiba mpya iwaondoe.Hakuna sababu ya kuwa na mkuu wa wilaya, mko pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom