DAWASA imenitumia bill ile ile miezi mitatu mtawalia, hii si sawa

Candela

JF-Expert Member
Aug 12, 2021
657
1,735
Kwa miezi 3 mfululizo sasa DAWASA wamekuwa wakinitumia bili ya maji yenye kiasi kile kile hakibadiliki, FEBRUARY wametuma bili, MARCH wakatuma kiasi kile kile mpaka senti, na hii ya APRIL wametuma ile ile, ni kama wametu forwardia tu meseji.

Nikiangalia matumizi kuna mda hatugusi bomba kabisa, tukijaza tanks tunaweza zitumia miezi 2 shughuli za jikoni bomba inabaki kuoga tu.

Sasa kama tumejaza February (baada ya bili ya January) wakaleta bili yake kawaida itakuwa kubwa. Lakini February mpaka March maji yote ya kutumia jikoni yanatoka kwa Tanks na mifumo yake iko tofauti, yaani ili maji yafike jikoni na bomba la nje lazima yakae kwa tank.

Dawasa ina flow moja kwa moja Bafuni pekee kwa ajili ya kuoga tu, hatujafill tanks Tangu Hiyo January mwishoni mpaka leo. Kufua tunapeleka kwa Dobi.

Cha ajabu bili ya kujaza matenki 3 ya 10,000 Litres each imekuwa sawa na bili ya kuoga kila siku kwenye bomba la mvua. Hata kama tunaoga na kuosha Zambi zetu hii sio sawa, kuna mahali DAWASA mnatutapeli.
 
Kwani hata wewe si unaweza kurekodi matumizi ya maji kupitia mita yako...

Tazama mita yako tarehe fulani kuona inasoma kiasi gani, subiri baada ya mwezi tazama tena...

Fanya hivyo kwa miezi kadhaa ili uone matumizi yako yakoje...

Back
Top Bottom