Mimi ni Polisi: Hadi Lindi

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Mimi ni Polisi: Hadi Lindi?


2001

Ndio kwanza nilikuwa nimetoka depo na kupangiwa mkoani Lindi. Maisha kwa kweli yalikuwa magumu. Mkoa ule umekaa kushoto sana. Kitu pekee nilichoona nafuu ni bei za nyumba za kupanga.

Nilibahatika kupata nyumba ya kupanga yenye chumba kimoja cha kulala, sebule, kajiko na bafu/choo kwa shilingi 70,000/- tu. Ilikuwa imeungana na nyumba nyingine hivyo tulikuwa wapangaji wawili tu kwenye eneo lile. Maji ya bomba tulishare bomba lililopo nje ya nyumba. Jirani zangu walikuwa baba na mama Sharifa. Ni kisa cha baba Sharifa kilichonifanya nijiulize kama hadi Lindi kuna mambo haya kumbe.

Ilianza kama utani...

2001, March

"Pole na kazi afande" Nilisikia sauti nyororo ikisema. Nilikuwa nimetoka zamu lindo la benki ya CRDB mjini. Ilikuwa ni sauti ya jirani yangu, Mama sharifa.

Imeandikwa usimtamani mke wa jirani yako ila ngoja tu nimpe sifa zake. Mama Sharifa! Mweupe wa wastani, nywele ndefu nyeusi zinazoshuka mpaka chini kidogo ya mabega (hizi niliziona siku nyingine) na midomo iliyojaa vyema. Ana umbo linaloelezeka kiasi kwamba pamoja na kuvaa hijab lakini unaweza kuliona na likakuvutia..aaah mama sharifa umeniponza!!!

"asante ma Sharifa, mmeshindaje?" Niliitikia

"sie kama unavyojua afande," alijibu.

Tangu nimehamia pale mara nyingi nilikuwa nasikia akigombana sana na baba Sharifa usiku. Sikuwa nikijua nini hasa sababu na kwa kuwa hakuwa akilalamika asubuhi, nikaona niwaache na mapenzi yao. Ila akili yangu ya upolisi ilitaka tu kujua kama yote yalikuwa sawa.

"Yupo?" (nilimuuliza kama mumewe yupo kwa sauti ya chini)

"Ayupo kenda vuna chumvi," alijibu.

Nilisogea hadi alipokuwa mama Sharifa akipembua mchele nikaketi kwenye jiwe tukaanza kuongea.

Mentor: "Salama lakini mama Sharifa?"

Mama sharifa: "Mh! Afande acha tu maisha ni magumu ila ndo hivyo tunavumilia."

Mama Sharifa aliniambia kuwa yeye ni Mdigo wa mkoani Tanga na alikutana na baba Sharifa kipindi hicho baba Sharifa, ni baba Sharifa kweli. Alikuwa akifanya biashara ya kusafirisha chumvi kutoka Lindi kwenda mikoani. Kipindi hicho alikuwa amepita Tanga kununua chumvi akauze sehemu nyingine alipokutana na mama Sharifa.

Alitania kuwa game alilompa baba Sharifa lilimdatisha akaahidi hatorudi Lindi bila mama Sharifa. "Kipindi hicho nilikuwa naita kweli sio sasa hivi unavoniona afande wangu," aliongeza mama Sharifa. Iliwachukua wiki tatu tu kuhakikisha yote yamekuwa sawa na mama Sharifa alikuwa ndani ya basi wakielekea mkoani Lindi. Pesa iliongea.

Kumbe baba Sharifa alikuwa akifanya biashara bila daftari. Yeye akisafiri akarudi na lundo la hela hajui kuwekeza au kuhifadhi. Alitumia hadi ziishe zote. Alijaribu kumwelekeza mumewe huyo bila mafanikio na baada ya muda alifilisika. Baba Sharifa akaishia kuwa mchimba chumvi.

Chanzo hasa cha ugomvi wao kilikuwa baba Sharifa kutotimiza wajibu wake kama mume. Alianza kwa kutimiza mara moja kwa wiki kisha mwezi na sasa wana miezi tisa baba Sharifa akirudi ni kulala tu tena siku nyingine bila hata kuoga, "ananata nata jasho la chumvi. Hata umwambie akaoge hataki, mimi nahisi anafanya hivyo ili nisimguse ila ndo hivyo afande ninapata shida sana." Aliniambia pia kutokana na kufilisika huko amekuwa mtu wa kununa na kuanzisha ugomvi alimradi tu, hadi chumvi kidogo kwenye chakula kitu ambacho anaweza kuongeza mwenyewe tu.

Nilimfariji mama Sharifa na kumtia moyo avumilie kwani katika ndoa kuna mazuri na mabaya na huu ni wakati wa mpito tu.

Tuliendelea kuongea na mama Sharifa kila mara nilipokuwa nikirudi kazini mchana maana mumewe anakuwa ameenda baharini. Na kwa wakati ule mama Sharifa alinifaa sana kwani alikuwa ananipikia kuanzia staftahi hadi chakula cha usiku. Sitosahau mfungo wa mwaka ule wa Ramadhani. Nahisi niliongeza japo kilo mbili tatu. Mdigo yule yuajua kukarangiza maakuli. Na mimi kuonesha ushirikiano nilikuwa nikimwachia pesa kidogo za kusaidia kubadilisha mboga nisijewafilisi na mumewe.

2002 January, Kosa la kwanza

"Afande, ngoja nikusaidie," alitamka mama Sharifa. Nilikuwa nikifanya usafi ndani kwangu. Nilikuwa nimetoka nje nisafishe dekio niendelee kudeki chumbani kwangu.

"Ah! Asante ma Sharifa ndo adha ya kutokuoa hii," alicheka akaninyang'anya dekio akamalizia kudeki kile kisehemu kilichokuwa kimebakia. Hapo nilikuwa nimesimama nje ya mlango namwangalia alivyoinama, basi nisimalizie!!!

"Wala usijali bana afande, siku ingine uwe unaacha funguo tu nitafanya usafi."

Na ndiyo ikawa tabia yangu, nikitoka asubuhi naacha funguo juu ya mlango naenda kazini. Nikirudi nakuta ndani pamefanyiwa usafi na chakula kipo mezani. Ah! Mama Sharifa alidhamiria kuniweka matatizoni.

2002 January 28

Nilitoka lindo la mchana nimechoka sana kwani hiyo siku nilikuwa nimepangwa lindo la usiku hadi asubuhi ila waliopangwa kuja kutupokea asubuhi hawakufika hadi mchana. Kwa nidhamu tuliyofundishwa hatukuweza kuacha lindo, hivyo ilitubidi kukaa lindo masaa 18. Nilirudi na kukuta mlango wazi. Niliingia kwa kunyata ndipo nikamuona mama Sharifa, akiwa anapangusa paja na kitambaa. Mh! majaribu haya. Alikuwa akitoka damu kiasi. Nilimsalimia ndipo alipojistukia na kujifunika.

"Umefanyaje mama Sharifa?"

Aliniambia alijikwaruza bahati mbaya wakati anafuta kabati. Nilimwomba kupaona naye bila hiyana akapandisha baibui nipaone. Tulishtuka nusu saa baadaye bila kujua yaliyoendelea. Mama Sharifa aliomba msamaha sana na kuondoka haraka. Kwa dakika chache za mwanzo nilipatwa hofu na kujutia upuuzi niliofanya na mke wa mtu. Kwa kweli kama sumu huwa tamu hivi naelewa kwa nini watu wengi hawaogopi #sina-maana-hiyooo

Kosa la siku moja likawa tabia. Nilikuwa kila nikitoka lindo mchana namkuta mama Sharifa ndani kwangu. Muda huo tulikuwa na uhakika Baba Sharifa hayupo. Siku moja mama Sharifa aliniambia mumewe amemtishia usiku. Alimwambia, "Mama Sharifa, ujue nilipotoka kijijini kuja hapa niliaga lakini? Chunga nyendo zako." Nilijifanya mjuaji wa miji ya watu nikamwambia asitishike Polisi halogeki. Tuliendeleza libeneke hadi wiki tatu baadaye.

Hali hii ilinianza usiku nikiwa lindo. Nilihisi maumivu wakati wa kujisaidia. Maumivu hayo yaliendelea kwa muda wa siku tatu mfululizo. Nilijiambia itakuwa UTI tu hivyo nikameza anti-biotics na kwa muda wa kama wiki mbili maumivu yaliisha kabisa. Ghafla baada ya hapo kukaanza kuota nyama nyingine mbele ya kichwa cha uume wangu. Nyama hii iliambatana na maumivu sana. Nilienda hospitali ambapo madaktari hawakujua sababu ya uoto huo. Nilipima magonjwa yote ya zinaa na kukutwa safi. Madaktari waliamua kunifanyia upasuaji na kuondoa nyama hiyo. Baada ya muda nilipona na kuendelea na maisha kama kawaida.

Lakini kama lilivyo sikio la kufa, sikusikia dawa. Baada ya kupona tu nikarudi kwa mama Sharifa. Baada ya miezi minne hali ile ilijirudia tena na mimi nikajipa moyo kuwa labda hawakuitoa vyema hivyo nikarudi hospitali. Mchezo huu uliendelea hadi siku nilipoitwa hospitali na daktari.

Lindi Regional Hospital, 2003

Baada ya kusikia jina langu likitajwa nilinyanyuka na kumfuata nesi hadi ndani ya chumba cha daktari ambapo aliweka faili langu juu ya meza ya daktari na kutoka nje. Daktari alinikaribisha huku akinionesha kiti cha kukaa.

Daktari: "Karibu kijana, karibu uketi."

"Asante dokta, shikamoo," nilimsalimu.

Dokta akaendelea, "Unajisikiaje tangu upasuaji wa mwisho?"

Mentor: "Vizuri tu dokta sijasikia tatizo lolote tena."

Dokta: "Vizuri. Kuna taarifa zisizo nzuri sana ningependa kukuambia, ila usishtuke sana bado haijathibitishwa."

Nikajiweka vizuri kwenye kiti kusikiliza taarifa hizi. Dokta akaendelea, "Upasuaji wa mwisho uliofanyiwa ulituhitaji kukuongezea damu. Kwa bahati mbaya damu ile haikuwa imepimwa vya kutosha kutokana na uharaka wa hitaji lako la damu hivyo uliwekewa damu inayosadikiwa kuwa na virusi vya UKIMWI. Nimekuita hapa ili tufanye vipimo zaidi kuthibitsha hili."

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

 
NB: Baada ya vipimo na dawa nilibahatika kukutwa sijaathirika na virusi hivyo. Nilijihisi mshitakiwa aliyepewa adhabu mara mbili kwa kosa moja. KWamba ule ugonjwa usioelezeka haukutosha, baba Sharifa akaamua kunitumia na virusi vya UKIMWI kwa njia alizozojua mwenyewe.

Kwa kweli mke wa mtu sumu, tena sumu iuayo!

Jenga kisima chako kijana mwenzangu, unywe maji ya kisima chako mwenyewe. BE WARNED..nilipona mimi, hatuna uhakika kuhusu wewe.
 
Mentor nawe uliposave kuambukizwa UKIMWI kule Tanga ukaenda tena kwa mama Sharifa Lindi?
Eti uliomba uone alipoumia ulitaka kumpima nini wewe Daktari ama? tehetehe na Yule mchuba mliyekutana bar vipi naye?
 
Mmmh! Kumbe ubazazi umeuanza zamani ha ha ha eti sina maana hiyo !! He hee chezeya baba shaa wee!! Polee! Kastory kazuri !!
 
Kitu hikooo nimekiotea ngoja nikisome
mwekundu upo ndugu yangu? #longTYM

kwa hiyo una ukimwi

Hapana masai dada, niliponea kwenye tundu la sindano...vipimo vilionesha damu niliyowekewa haikuwa hiyo walioihisi kuwa na virusi hivyo. Hata hivyo adhabu nilikuwa nimeshaipata mwanzo (psychological torture) nadhani ilitosha, don't you think?

Yeah...."Baki Njia Kuu, Michepuko Hailipi"!

Sisi tusiooa bado huwa tunajiambia hatuna njia kuu...ni sawa na mtembea kwa miguu, popote njia! Nilikosea nikaenda kutembea katikati ya barabara.

Mentor nawe uliposave kuambukizwa UKIMWI kule Tanga ukaenda tena kwa mama Sharifa Lindi?
Eti uliomba uone alipoumia ulitaka kumpima nini wewe Daktari ama? tehetehe na Yule mchuba mliyekutana bar vipi naye?

Nyani niliyekoswa na mishale mingi mkuu, niko hapa kuwaonya!

Teh teh nice story kwa #teamRafiki wajifundishe Tatizo lako Mentor ugonjwa wako unaitwa #Bazazi you are addicted kwenye wake za watu
Muulize Nicas Mtei au Excel mwenzio ana handle vipi

Mnajuana wenyewe...endelea kuwaita na wenzako wa #teamBAzazi .

Aha aha aha! Acha uoga soja!! Askari mzuri anatakiwa awe na tripple W yaani war, women and whisky. Kwa maana ya mpenda mapambano, mtu wa totoz, na pia mlevi.

Endelea kusimamia show at ur own risk soja!!

Ahahah mkuu, seriously??!
Hunitakii mema wewe...

Pole afande.

Asante raia!

Du!natabaki na mali yng aisee...kama hali ni hii.

Hapana mkuu, OA tu...! Hawa kina mama Sharifa na Mentor ni wachache...wasikunyime raha ya ndoa mkuu!

Duuh...nice story bro!

Thanks mkuu, jifunze! Usiwe kama mimi...

Mmmh! Kumbe ubazazi umeuanza zamani ha ha ha eti sina maana hiyo !! He hee chezeya baba shaa wee!! Polee! Kastory kazuri !!

Nimeacha lakini! Halafu mbona meseji yangu bado iko pending...
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom