dawa ya unene

noella

Senior Member
Mar 21, 2011
101
46
Salamu wote wanaJF,

Mimi ni mama wa mtoto mmoja, nina tatizo la umbile langu yani ni mwembamba ninavaa size 8. Kwa kweli huwa nikijiangalia hata sipendezewi na umbo langu, nimekuwa nikila ovyo ili ninenepe lakini wapi. Nimekula mpaka cerelac na uji vya mtoto lakini wapi.

Sasa nimesikia kuna dawa za kuongeza unene. Nahitaji ushauri wenu kwa hili tafadhali. Kuna yeyote aliyewahi kunywa hizo dawa? Na je, zina side effects gani? Au kama kuna njia mbadala naomba ushauri, maana hata nikivaa nguo sipendezi.
 
Dada Noella,

Yaani umbile kama lako watu wengi wanahangaika kulipata hata wanalazimika kutokula wakati wana kila kitu. Ningekushauri uridhike na ulivyo, kwani baadaye kama wewe ni mweusi utataka uwe mweupe na kama ni mweupe utataka uwe mweusi, kitu ambacho baadaye utaonekana kituko.
 
Dada Noella,

Yaani umbile kama lako watu wengi wanahangaika kulipata hata wanalazimika kutokula wakati wana kila kitu. Ningekushauri uridhike na ulivyo kwani baadaye kama wewe ni mweusi utataka uwe mweupe na kama ni mweupe utataka uwe mweusi kitu ambocho baadaye utaonekana kituko.

Asante my dear kwa ushauri.

Huwa najisikia vibaya pale napokutana na watu halafu wananambia kuwa unazidi kuwa mdogo tu au hukui..yani mwili wangu ukiniona huwezi kujua nina mtoto, ndiyo maana sipendi nataka ninenepe japo kidogo tu
 
haaa haaaa haaaa pole lakini me nadhani we ni mtu mwenye bahati sana,ni leo tu asubuhi wakati nkwenda kazini nilikutana na kijana kama ana miaka 14 au 15 lakini ukimuona nadhani suruali ya size 40 cjui kama inamtosha kwa unene!

Uwe jasiri wa kuisimamia nafsi yako ijikubali ulivyo. Au unasemwa huna usafirii na pistol? huo huo na hizohizo mbona poa tu? Kula tu vizuri na dawa ya kuongezeka ni kuridhika tu.

MUNGU SI FUNDI MUASHI, YEYE HAKOSEI.
 
Hongera sana kwa kuwa na umbo dogo kwani wengi wanatamani kupungua na hawawezi.
Ridhika na Kazi ya Mungu kwani haina makosa.
 
Kinachofanya ukonde sana ni hayo mawazo ya kutaka unene, relax kubali ulivyo then the body will come. Yaan km vle una hamu ya kushika mimba ukiiwaza sana haiji ng'oooooo... ukiwa uitaki au ukijiachia na wala hauna shauku nayo ndo inakuja, so u just relax ma dear.

Wenzako tunashinda gym kutafuta kuvaaa size 8, we watafuta dawa ya kufmuka? dahh! Kupendeza kitu gan? Kuwa na akili na roho nzuri then ukiongea mbele za watu utaonekana umependeza tu na utapewa kiti cha mbele, lakini kupendeza kimavazi/ outfit, mmh, huko si kupendeza.

Takatisha na pendezesha ubongo wako na roho yako, huo ndo urembo kamili.
 
kusema ukweli sikuwa na tatizo hapo mwanzo..ila baada ya kupata mtoto nikajua nitanenepa ila ikawa vice versa mtoto aliacha kunyonya ana miezi tano..nikarudi kwenye kilo zangu na size ile ile ya mwanzo tena naona nimekuwa mdogo zaidi..maneno ya watu ndo yananikosesha raha..eti hukuii,unazidi kuwa mdogoo..aa sasa mi nakosa raha mnoo. Mume wangu naye asubuhi hii ananambia loo nawe mdogo sana..ndo kisa cha mimi kutaka kunenepa
 
Asante my dear kwa ushauri.

huwa najisikia vibaya pale napokutana na watu halafu wananambia kuwa unazidi kuwa mdogo tu au hukui..yani mwili wangu ukiniona huwezi kujua nina mtoto, ndiyo maana sipendi nataka ninenepe japo kidogo tu

mimi natafuta mke wa kumuoa awe na vigezo kama vyako, sema utakuwa hujui watu kama nyinyi mlivyo na thamani

kusema ukweli sikuwa na tatizo hapo mwanzo..ila baada ya kupata mtoto nikajua nitanenepa ila ikawa vice versa mtoto aliacha kunyonya ana miezi tano..nikarudi kwenye kilo zangu na size ile ile ya mwanzo tena naona nimekuwa mdogo zaidi..maneno ya watu ndo yananikosesha raha..eti hukuii,unazidi kuwa mdogoo..aa sasa mi nakosa raha mnoo. Mume wangu nae asubuhi hii ananambia, loo nawe mdogo sana..ndo kisa cha mimi kutaka kunenepa
nikipata mtu kama wewe naoa hapo hapo na ndoa kabisa
 
Asanteni wapendwa kwa kunipa moyo nahisi confidence ilinitoka pale partner wangu alivyonambia hivyo
ila kwa kupata maoni na ushauri wenu nimejisikia mwenye furaha na amani kabisa

@Ivuga..asante, nadhani niliyenae kwa asubuhi ya leo tu hajanipenda gafla jinsi nilivyo ila naona umenena ukweli mtupu
nashukuruni sana
 
Salamu wote wanaJF

Mimi ni mama wa mtoto mmoja,nina tatizo la umbile langu yani ni mwembamba ninavaa size 8.kwa kweli huwa nikijiangalia hata sipendezewi na umbo langu,nimekuwa nikila ovyo ili ninenepe lakini wapi..nimekula mpaka cerelac na uji vya mtoto lakini wapi.

sasa nimesikia kuna dawa za kuongeza unene.nahitaji ushauri wenu kwa hili tafadhali.
kuna yeyote aliyewahi kunywa hizo dawa,je zina side effects gani?
au kama kuna njia mbadala naomba ushauri.hata nikivaa nguo sipendezi.

Tafuta mchagga uzae naye atakupa uzazi ukitoka umefura kama kiboko
 
Asanteni wapendwa kwa kunipa moyo nahisi confidence ilinitoka pale partner wangu alivyonambia hivyo
ila kwa kupata maoni na ushauri wenu nimejisikia mwenye furaha na amani kabisa

@Ivuga..asante, nadhani niliyenae kwa asubuhi ya leo tu hajanipenda gafla jinsi nilivyo ila naona umenena ukweli mtupu
nashukuruni sana
ni kweli dada yangu yaani wenzako wengi wanatafuta miili kama yako,hawali kutwa nzima , sema basi tu umeshaolewa ila nisingekuacha . hauna hata mdogo wako huko/?
 
Unene ni uzembe, usipende unene. Jipende vile ulivyo.
Kwenye suala la kuvaa angalia nguo ndogo ndogo zinazoendana na mwili wako.
Ukivaa minguo mikubwa mikubwa lazma uchekeshe.
Jiamini mdada. Kuna vibonge vinatamani vikonde.
 
ni kweli dada yangu yaani wenzake wengi wanatafuta miili kama yako,hawali kutwa nzima , sema basi tu umeshaolewa ila nisingekuacha . hauna hata mdogo wake huko/?

hahaha..pole Ivuga nilizaliwa msichana peke yangu sina mdogo wa kike.lol
 
Lo, wewe dada una nini, angalia usijaribu dawa utakuja kujuta hata kuzaliwa, mbona wenzio wanahaha kuwa kama wewe wanashindwa, kama ni huyu mumeo anakuambia anapenda unene anakudanganya na si zaidi hata yeye anakuonea wivu na kafugure kako.
 
mimi nimemwambia nataka nimuoe huyu.watu tunatafuta vipotabo yeye anatafuta midawa ili awe kibonge!!
 
Kula mara tano kwa siku, yaani msosi hevi.. utaona matokeo yake. Asubuhi chai na vitumbua au chapati 2, saa tano tano pata uji wa ulezi, mchana pata ugali/wali na nyama au samaki tena ule sahani imejaa. Saa 10 piga chai maandazi, na saa 2 usiku ule wali wa kushiba. Fanya hivyo kwa miezi 3 tu utapata matokeo.
 
Kwa nini usiridhike na ulivyoumbwa? Ukitaka kujua faida ya hicho unachokiwaza nenda duka la muziki, nunua CD ya marehem Marijan Rajab yenye wimbo unaoitwa Mayasa
 
Kinachofanya ukonde sana ni hayo mawazo ya kutaka unene, relax kubali ulivyo then the body will come. Yaan km vle una hamu ya kushika mimba ukiiwaza sana haiji ng'oooooo... ukiwa uitaki au ukijiachia na wala hauna shauku nayo ndo inakuja, so u just relax ma dear.

Wenzako tunashinda gym kutafuta kuvaaa size 8, we watafuta dawa ya kufmuka? dahh! Kupendeza kitu gan? Kuwa na akili na roho nzuri then ukiongea mbele za watu utaonekana umependeza tu na utapewa kiti cha mbele, lakini kupendeza kimavazi/ outfit, mmh, huko si kupendeza.

Takatisha na pendezesha ubongo wako na roho yako, huo ndo urembo kamili.

big ups!
 
Back
Top Bottom