Dawa ya hasira

mkuu inshort nagombana na mtu yule atakaye nihusisha kwa njia 1 au nyingine kwenye mazungumzo.
Mfan nikuwa kwenye daladala kalibia watu wote waliokuwa wanaongea na redio pia ilikuwa imefunguliwa iliniboa sana nilishikwa na hasira na kama ningekuwa na uwezo ningeamuru redio izimwe na watu wote wawe kimya balaa na hasira zote zilimdondokea konda wakati akidai nauli mzigo wote wa hasira ulimwishia yeye.

Tatizo hasira sijajua zinatoka wapi maana nimekuwa na hasira pasipo sababu wala sijagombana na mtu.
Ila nikikaa na mtu ndani ya dk 1 lazima tutakwaruzana huwa najisonya pasipo hata sababu naweza nikaa nikawa nimeduwaa kama kunakitu nawaza/fikiria na ugomvi huanza mtu yoyote atokee na kunisemesha au kunidistable kwa namna moja au nyingine balaa huanzia hapo.
Hakuna kitu kama hasira bila sababu. Sababu ipo mkuu, ila huijui. Na vitu vitakavyo kusaidia kujua sababu ni hivyo hapo in bold. ukisha jua hasira inapanda wakati gani itakua rahisi kupunguza exposure na vitu hivyo, au kujifunza namna gani unaweza kuziwia hasira kupanda ikiwa unakutana na mazingira hayo.
Kuna councelor mzuri sana humu JF, anaweza kukusaidia free of charge. Ukiwa interested nitakupa ID yake via PM.
 
mkuu jongoo linapanda mtungi kama kawaida
ila semaga nikitambo kimepita sija DO na sinaga mpango wa wanawake naona kama wananitibua brain yangu.

hii inaweza kuwa sababu kuu ya wewe kukasirika mara kwa mara. most likely kuna jambo linakusumbua akili ndo maana umewaweka pending warembo, hence stress..
 
Kwa kawaida hasira husababushwa na kuwa na mawazo mengi. mkuu tiba ya hasira, hakikisha unakula ndizi za kutosha kila siku, ndizi ina kemiko iitwayo serotonin ambayo inafanya regulation ya mood na kumfanya mtu kuwa na furaha, kujisikia vizuri, pia na kupata usingizi wakutosha,na kuondoa hasira. PIA MKUU UNAWEZA KWENDA PHARMACY ULIZIA DAWA INAYOITWA PROZAC mg 20 mara moja kwa siku mpaka dose itakapoisha
 
Nahisi utakuwa umetendwa tu,possibly na demu... Hapa ni kumtafuta mtaalamu wa psychology haraka kabla hujaharibikiwa zaidi.
 
unaweza ngumi au ndo boya sasa angalia wengine wapiga ngumi za chembe au unamadeni nini ndo maana hasira haziishi
Conquest-ukiwa na hasira jiharishie then walk around the street
 
Stress hizo za ukosefu wa kuDu, tafuta dem utoe wadudu hao wamejaa wanaleta tension zisizokua na msingi.
 
labda una matatizo ya kifedha
Labda mambo yako hayajaka a vile unavyotaka
Na labda wanawake imekuwa ndio tatizo lako kubwa linalokuchanganya ubongo
 
Wakuu naomba kuuliza kama kuna dawa yoyote ya hasira.
Kwani sasa hivi nimekuwa na hasira ambazo nashindwa hata kujua chanzo chake ni nin?
Kwani nimekuwa sitaki au kusikia mtu yeyote akiongea mbele yangu au kunisemesha.Mpaka niandikapo post hii nishagombana na watu zaidi ya 7 kwenye simu na wa usoso kwa uso hawahesabiki.

Naomba msaada wenu wataalam hali hii huweza sababishwa na nin na tiba yake ni nin??
hao unaopenda kugombana nao ni wanawake au wanaume?
Wewe una pschological problem.ni maradhi ambayo yanasababishwa na kitu kibaya chochote ambayo kinastick mind yako.ushauri wangu ni huu:nenda kwa daktari wa wagonjwa wa akili na umueleze tatizo lako halafu yeye atkupa tiba sahihi.
 
Ndugu yangu hilo linaweza kuwa ni pepo, unajua shetani yupo kazini anakutia hasira kuna siku utakasirika utafanya kitu kibaya kitakuingiza kwenye matatizo makubwa. Kwa imani yako fanya maombi sana muombe Mungu akuondolee hasira na ulikemee hilo pepo la hasira na uanze kufanya mazoezi ya kuwa mtu wa kawaida kujichanganya na watu uone kama tiba imefanya kazi.
 
Back
Top Bottom