Tatizo la Typhoid na UTI zinayojirudia mara kwa mara. Je upi ni mdadala wa dawa za Hospitali au nini kufanyike ili kuondokana na tatizo?

SIRE

Member
Feb 20, 2022
83
119
Wakuu naanza kwa salamu zangu za dhati kwenu pia poleni na mihangaiko ya siku nzima ya leo.

Kabla sijaenda kwenye maada. Naanza kwa kusema kuwa najiona kuwa na bahati sana kuwa katika jamii ya siri kama hii ambapo kila mmoja ana uhuru wa kutoa mawazo yake bila kuhofia kutambulika katika jamii husika kitu ambacho kimafanya watu wawe huru sana kutoa mawazo na maoni yao ya siri juu ya maada mbalimbali.

Paso na kupoteza wakati wenu naomba nianze na kuelezea hili swala ambalo naliona kama kero kwangu.

Nimekuwa nikisumbuliwa na Typhoid na UTI ambazo zinarudi tena muda mfupi ( makadirio ya mwezi mmoja au miwili) baada ya kutumia dawa za hospitalini. Hii shida sikuwahi kuwa nayo nilipokuwa mtoto lakini ni haki ambayo imejitokeza nikiwa mkubwa. Nakumbuka nilipokuwa mtoto nilikuwa nakunywa hata maji ya bombani bila shida yeyote, lakini hali ilibadilika nilipojiunga na advance. Hali hii imekuwa endelevu mpaka imekuwa kero kwangu.

Nimetumia dawa karibia zote zinazohusiana na Typhoid na UTI. Baada ya kutumia kidogo napona lakini baadae naanza kupata dalili tena.

Nafikia kipindi naogopa pengine matumizi yaliyozidi ya dawa za hospitalini yataleta athari kwenye ini au figo.

Naomba kwa aneyejua dawa za asili Ili nipate kuwa natumia pengine zikanitatulia hili tatizo langu.

Natanguliza Shukrani zangu kwenu kwa usaidizi mtakaonipatia.
 
Kwani Dr. Janabi anasemaje?

-1251504935.jpg
 
Nimetumia dawa karibia zote zinazohusiana na Typhoid na UTI. Baada ya kutumia kidogo napona lakini baadae naanza kupata dalili tena...
Nimetumia dawa karibia zote zinazohusiana na Typhoid na UTI. Baada ya kutumia kidogo napona lakini baadae naanza kupata dalili tena

🤔🤔
 
Tatizo ni kitu unachokula na Usafi
Pengine mkazi wa maeneo kama ya DAR au Moro na unakunywa maji ya visima,Bomba haya Maji yana bacteria wengi sana sasa Unakunywa unapata Typhoid unameza dawa inatulia kisha unaendelea kunywa maji yaleyale lazima irudi..

Au Unakula Migahawani/Chipsi hasa kachumbali au mayonaizi za Viepe mara nyingi wanaandaa kwenye Mazingira sio masafi kwahiyo nawewe ukila lazima uumwe tumbo..Mikono michafu lazima uumwe

Kifupu hakuna mchawi zaidi ya VITU UNAVYOINGIZA MDOMONI...
 
Nilikuaga na shida ya typhoid ya kujirudia ila nikapataga dawa za wahaya, kuna kipindi nilikua pande za Nkwenda kuna mwenyeji akaniagizia dawa toka kwa jamaa wapo boda ya mutukula, tokea kipindi hiko kama 2017 hivi sijawahi kupata typhoid tena hadi leo
 
Nimetumia dawa karibia zote zinazohusiana na Typhoid na UTI. Baada ya kutumia kidogo napona lakini baadae naanza kupata dalili tena

Asante kwa kuelewa hapa nilihisi ingeleta utata. Nilitaka kumaanisha kuwa, nikitumia dawa na kupona muda mfupi (approx 2 months) baada ya kumaliza dawa napata shida hiyohiyo.
 
Nilikuaga na shida ya typhoid ya kujirudia ila nikapataga dawa za wahaya, kuna kipindi nilikua pande za Nkwenda kuna mwenyeji akaniagizia dawa toka kwa jamaa wapo boda ya mutukula, tokea kipindi hiko kama 2017 hivi sijawahi kupata typhoid tena hadi leo
Asante mkuu, Vipi shida yako iliisha jumla?
 
Nilikuaga na shida ya typhoid ya kujirudia ila nikapataga dawa za wahaya, kuna kipindi nilikua pande za Nkwenda kuna mwenyeji akaniagizia dawa toka kwa jamaa wapo boda ya mutukula, tokea kipindi hiko kama 2017 hivi sijawahi kupata typhoid tena hadi leo
Asante mkuu, nitaifuatilia hii dawa. Maana nipo hukuhuku kwa wahaya. Naamini watanisaidia.
 
Wakuu naanza kwa salamu zangu za dhati kwenu pia poleni na mihangaiko ya siku nzima ya leo.

Kabla sijaenda kwenye maada. Naanza kwa kusema kuwa najiona kuwa na bahati sana kuwa katika jamii ya siri kama hii ambapo kila mmoja ana uhuru...
Unapoenda kupima U.T.I. hospitali, ni muda gani unapata majibu ya kipimo?
 
Back
Top Bottom