David Mwaibula, aliyebuni mistari ya daladala Dar es salaam yupo wapi?

sijui nini kilitokea mpaka mwaibula akazimwa? gafla tu ikaja sumatra isiyo na meno toka mwaibula amekuja na innovation ya kuchora magari mstari ili yasikatishe ruti na akaja na ruti mpya kibao na akaondolewa ikaundwa sumatra mpaka leo hakuna ubunifu wowote uliofanyika kusaidi kero za usafiri ingawa challenge zimekua zikiongezeka?? kwa nn huyu jamaa hakupewa nafasi huko sumatra is beyond me!!
 
Kila shujaa na wakati/vita yake. Ndio maana wengine wanaendelea kumuwaza Mwalimu Nyerere huku wakisahau kuwa yeye aliishi maisha yake na akafanya aliyostahili kufanya hivyo hivyo kwa Mzee Mwaibula.
Tunachojifunza hapa ni kuwa wanaozaliwa sasa hivi tu watu tusiotumia akili, wanyonge na dhaifu na ndio maana tunayaona yote haya. Swali la kujiuliza ni: huu ujasiri wa kukatiza ruti watu wa daldala wanaupata wapi na wewe unyonge wa kutowakatalia au kudai chako umeurithi kwa nani!?
 
mwaibula alikuwa mbunifu na hakuwa mbabaishaji,sumatra ni wa kujilipa mishahara mikubwa tu..
 
Kila shujaa na wakati/vita yake. Ndio maana wengine wanaendelea kumuwaza Mwalimu Nyerere huku wakisahau kuwa yeye aliishi maisha yake na akafanya aliyostahili kufanya hivyo hivyo kwa Mzee Mwaibula.
Tunachojifunza hapa ni kuwa wanaozaliwa sasa hivi tu watu tusiotumia akili, wanyonge na dhaifu na ndio maana tunayaona yote haya. Swali la kujiuliza ni: huu ujasiri wa kukatiza ruti watu wa daldala wanaupata wapi na wewe unyonge wa kutowakatalia au kudai chako umeurithi kwa nani!?

Kila vita lazima iwe na majeruhi.
 
Nilikuwa nashuhudia madenti wakijua mzee huyu katega barabara ya route fulani,wanakomaa kwenye seat ole wako konda uzingue,yuko wapi sasahivi?
 
Kipindi cha mwaibula watumiaji wa usafiri wauma (daladala)tulipata nafuu/uhakika wa usafiri wa daladala kwani daladala zilikuwa hazikatishi ruti gari ilivyo andikwa ndo inapoenda kuanzia mwanzo wa kituo hadi mwisho kama ni Gongolamboto-mwenge inakuwa hivyo hivyo nowdays daladala zinakatisha ruti kwa makusudi bila kuchukuliwa hatua yoyote.Mfano jana mapema kabisa saa 7 nimepanda daladala ya bugurun mbezi nimepanda wametucharge bugurun ubungo sh400 kufika ubungo 2kashushwa hapo hapo wakatangaza mbez 2kapanda ruti ya mia 500 tukatozwa sh800.jamani mwaibula na vijana wako tunaomba mrudi maskini Dar 2nanyanyaswa/tunabanwa kila kona.
Mkuu,
Kwanza pole kwa usumbufu uliokutana nao.
Tulishawahi kujadili suala Kama hili hapa Jamvini. Kukatisha Ruti ni kosa la kisheria. Na Kama ulitozwa Tsh 400 kutoka Buguruni mpaka Ubungo..halafu ukachajiwa Tsh 800 kutoka Ubungo mpaka Mbezi, kwa hiyo Ina maana Safari nzima ya Buguruni mpaka Mbezi ilikugharimu Tsh 1200/-. Huu ni UJANGIRI ambao hautofautiani na majangiri ya kuua Tembo.

Lakini wewe na Abiria wa hilo basi ni moja au kwa njia moja au nyingine mmechangia tatizo kwa kukubali na kufuata huo mfumo walioupanga Huyo Dereva na Utingo wa hilo daladala. Siku nyingine ikitokea tatizo Kama hilo Chukua tiketi ya hilo daladala...namba ya gari na Ruti iliyopangiwa halafu toa taarifa kwenye vyombo vya Dola. Pia Ulete hizo taarifa humu JF zikiwa na vielelezo nilivyoorodesha hapo juu ili haya Majangiri ya Ruti yaweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Haya matatizo yanatokea na ni wajibu wetu Kama Watanzania kupambana na Uhujumu na Ujangiri wa kila aina katika kila kona ya nchi yetu. Mungu Ibariki TANZANIA.
 
Mchango wa huyu Ndugu ni mkubwa kweli hasa kwa abiria tunaotumia usafiri wa daladala kwenda hapa na pale.

Utaratibu ulioanzishwa chini yake wa daladala kuandikwa njia unatusaidia sana hivi sasa na kutupunguzia gharama. Sipati picha ningekuwa natumia kiasi gani kwa siku kutoka na kurudi Kimara ninapojibanza. Sasa hivi hata konda akiitia mwisho Ubungo napanda tu ili mradi ni Kimara

Sijui yuko wapi, lakini mchango wake binafsi ninauthamini sana. Mwenyezi amjalie popote alipo Mheshimiwa sana David Mwaibula
 
Na zile barabara zake mpya alizobuni mpaka leo zipo vilevile hawajabuni nyingine yaani huyu mzee alikuwa jembe.
 
Du na alivyokw anagoma wamiliki wa daladala kupandsha nauli hovyo! nakumbka alishawahi kuwaambia kama wanataka wapandshe mauli basi wahakikshe wanakwenda na level!
 
Mzee mwaibula yupo, nilionana nae mwezi uliopita kwenye kitafrija flani. ....yupo sinza, ukifika uwanja wa tp kuna kanisa la wasabato, ukiuliza hata mtoto naenda kwa mwaibula basi unapelekwa
 
Mzee mwaibula yupo, nilionana nae mwezi uliopita kwenye kitafrija flani. ....yupo sinza, ukifika uwanja wa tp kuna kanisa la wasabato, ukiuliza hata mtoto naenda kwa mwaibula basi unapelekwa

kweli hazina kama hii inapotea kirahisi namna hii!.Big up mzee Mwaibula!
 
mzee namkubali sana, mara nyingi huwa anakuja dukan kwangu, Coz lipo karibu na garage yake, mzee ana stori nying sanaaa.
 
Back
Top Bottom