David Mwaibula, aliyebuni mistari ya daladala Dar es salaam yupo wapi?

Kwa sasa ruti zimekuwa nyingi, ubora umepungua, mabasi hayaeleweki mf mabasi ya msasani ni mabovu, yakifuatia ya Makumbusho Kkoo mstari Mwekundu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mwaibula alitakiwa apewe nishani ya Taifa kwa mambo mengi mazuri kwa daladala za Dar alitumia ubunifu wa hali ya juu
 
Daladala zinaenda Makongo zinasababisha abilia kupata Tetenasi sababu ya uchakavu, inshort zile ni Skrepa
 
Hawa makondakta wasikuhizi ni wachafu mnoo sijui hawaogi wananuka makwapa, meno ya njano kama wana kula ugoro yaani unakuta kavaa suruali juu ya suruali shati juu ya shati shati imechanika hovyo suruali Haina zipu miguuni ana malapa jamani wamekaa kama vibaka, wanapenda ugomvi na abiria hasa wakike.
 
Jana nimetoka kumtimua dereva wangu kazi kwa makosa ya kusababisha hasara kwenye gari ,kwa kifupi dereva wanting Ni mvivu ,muongo na hajali kitu Yuko ilimradi aishi

Naomba namba zake anipe mbinu ya kusurvivu kwenye hii biashara
 
Nadhani huyu jamaa ndio alikuwa anaendesha benzi fulani ya kizamani (chakavu) halafu ameiandika hivi "baba yako anayo?"
 
Back
Top Bottom