Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Mkuu Maranya siyo mimi ninayekuambia kwamba ni makampuni 13 angalia mtoa uzi mesema mangapi na ndio rejea yangu.
Mkuu naijua vizuri sekta ya ujenzi. Wakandarasi wetu wengi huwa hawako serious. japo na wachina siyo wazuri kihivyo lakini wa kwetu huwa wanajikosesha fursa nyingi sana sababu ya ubabaishaji. Pamoja na hayo huo ni mwanzo mzuri na kama watautekeleza huo mradi kwa ufanisi sioni ni kwa nini wasipewe miradi mingine. wazalendo wana advantage nyingi mno katika kushindana na wageni.
Kimbunga,
Nimekusoma ''kamanda'' ni kweli sio wewe unayeniambia, unamrejea mtoa hoja.
Kweli makandarasi hawa wazawa waonyeshe mfano na wajitengenezee cv ili waendelee kuaminika na hivyo kuwafungulia mlango na wazawa wengine kwani nchi yetu itafaidika sana kuliko kuwapa wachina ambao kazi zao siku hizi nyingi ni sub-standard!