Dar: Yaliyojiri katika mjadala wa wazi juu ya muswada wa vyama vya siasa katika ukumbi wa Kisenga Hall, LAPF Tower

Oct 15, 2018
17
153
Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) kimeandaa mjadala wa wazi juu ya muswada wa vyama vya siasa katika ukumbi wa Kisenga Hall, LAPF tower.

Lengo kuu ni kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Mswada na kuyapeleka kwenye mamlaka husika.

Tutawaletea update juu ya kinachojiri!

=====

UPDATES:





1547278397662.png

mdahalo2.jpg

DSC01128.JPG

Baadhi ya wananchi wakisikiliza ufafanuzi wa muswada huo kabla ya kuanza mjadala.

Baada ya kuchambua kiundani muswada huu TLS imetoa pia analysis au mtazamo wake juu ya mswada huo.

=====

Wakili Wilbard Msechu:
Mdahalo huu umehudhuriwa na wawakilishi toka serikalini, viongozi wa dini, wawakilishi wa mabalozi na mashirika ya kimataifa, vyama vya siasa, viongozi wa asasi za kiraia

1547281748524.png


Makatibu watatu wa bunge wamehudhuria katika mdahalo huu, hivyo nitumie fursa hii kuwakaribisha.

Lengo letu ni kuwafundisha wananchi kwa ujumla, ili wananchi waweze kujielewa. Nafungua mdahalo huu rasmi. Mdomo haujaumbwa kula tu, umeumbwa pia kutoa mawazo.

Lengo letu ni kuwafundisha wananchi kwa ujumla, ili wananchi waweze kujielewa. Nafungua mdahalo huu rasmi, toeni maoni yenu bila woga, Mdomo haujaumbwa kula tu, umeumbwa pia kutoa mawazo.


Wakili Harold Sungusia:
Kwanini Muswada Wa Vyama Vya Siasa umeletwa sasa? Ni nani atafaidika na sheria hii na nani watakuwa waathirika wa muswada. Je hakuna sheria nyingine zinazoweza tatua tatizo kama lipo? Kuna maswali mengi ya kichunguzi, je ni nani analalamika kuhusu muswada?

Tusome ibara ya 3 Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na kijamaa yenye kufuata mfumo wa vyama vingi

Ibara ya nane ya Katiba yetu inasema Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki za kijamii, hivyo wananchi wana mamlaka yote na serikali itapata mamalaka kutoka kwa wananchi

Nchi nyingine mbalimbali wamefanya analysis zinazohusiana na vyama vya siasa na kuna kitabu kingine nitajaribu kuwasambazia muone wenzetu wamefanyaje.

Ibara ya nane ya JMT ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki za kijamii, hivyo wananchi wana mamlaka yote na serikali itapata mamalaka kutoka kwa wananchi.

Haki za kisiasa ni miongoni mwa haki za binadamu, siasa sio uhalifu/uhaini ni haki za binadamu, siasa isifanywe kuwa uhalifu.

Nani atakayefaidikika ikiwa muswada huu utapitishwa na kwa kiwango gani? Nani ataathirika na kwa kiwango gani? Ni maeneo gani yenye utata na yanatakiwa kuondolewa au kurekebishwa?

Umeme unapokatika, ukiona baba analalamika jua alikuwa anaangalia kitu kizuri, na ukiona mtoto analalamika jua alikuwa anaangalia katuni. Kama wananchi lazima tuangalie 'what do we want'.

1962 Tanganyika kulikuwa na chaguzi, mwaka 1965 tulipata Katiba Mpya ikapiga marufuku vyama vya siasa ikaruhusu vyama viwili tu, TANU Tanganyika na ASP Zanzibar

Mwaka 1977 tulipata katiba yenye kava la rangi ya kijani. Marehemu Mchungaji Mtikila akasema tuna vyama vingi vya siasa, kwanini katiba iwe yenye kava la rangi mojawapo ya chama cha siasa? Katiba ikabadilishwa kava

Kumekuwa na kuminywa kwa #UhuruWaKujieleza , haki ya kufanya siasa, Ethiopia ni moja ya nchi ambazo zilirudi nyuma sana kwenye #UhuruWaKujieleza na haki nyingine za binadamu lakini sasa wamebadilika natumaini tutafuata mfano

Mwaka juzi tulitaka kuzindua kitabu tu cha Alphonce Lusako kinachoelezea suala la elimu. Polisi wakaja wakasema tumefanya mkutano usio halali. Mnaona tunavyovunja katiba kwa kukiuka uhuru wa kukutana?

Kuna wakati unaweza kwenda kwa fundi na baiskeli yako, akaharibu kabisa. Ninachotaka kusema ni kuwa si kila amendment (marekebisho ya sheria) ina jambo zuri

Msajili ana nguvu ya kufuta mwanachama yoyote ya chama cha siasa. Hivi ikitokea amemfuta uanachama mtu ambaye ni Rais wa nchi itakuwaje? Maana kwa Muswada Wa Vyama Vya Siasa huu msajili ana nguvu kuliko Rais

Nguvu na madaraka aliyonayo msajili wa vyama vya siasa, Msajili amepewa mamlaka makubwa sana. Kukufuta kuwa mwanachama, kuamua nani wa kutoa elimu ya kiraia, kuamua nani wa kugombea urais kwenye chama chako cha siasa

Huu muswada unahitaji nguvu ya kiungu kuuelewa, nimecheka sana nilivyokuwa naupitia...Umempa kinga msajili kutoshtakiwa, hata kama akifanya kwa uzembe, kumbuka ana mamlaka ya kufuta uanachama... Rais akifutwa uanachama itakuwaje??

1547281774246.png


Siku hizi ukitaka kuangalia taarifa ya muhimu lazima uangalie TBC kama una kingamuzi cha DSTV. TV zingine zimezimwa.Tunaamua kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii, ukienda huko nako unakutana na sheria, hata WhatsApp

Twende kwenye nguvu na madaraka ya msajili wa vyama vya siasa. Msajili amepewa mamlaka makubwa sana. Kukufuta kuwa mwanachama, kuamua nani wa kutoa elimu ya kiraia, kuamua nani atagombea urais kwenye chama cha siasa.

Siku hizi ukitaka kuangalia taarifa ya muhimu lazima uangalie TBC kama una kingamuzi cha DSTV.... Tv zingine zimezimwa, tunaamua kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii, ukienda huko nako unakutana na sheria.

Nimecheka sana nilivyokuwa naupitia muswada huu. Umempa kinga msajili kutoshtakiwa, hata kama akifanya kwa uzembe. Kumbuka ana mamlaka ya kufuta uanachama. Rais akifutwa uanachama itakuwaje?

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda, anasema:
Nawapongeza TLS kwa sababu ya dhamira zao nzuri na kuwa majasiri wa kushughulikia masuala ya kitaifa. Huu muswada wa siasa umekuwa ukisomwa hasa kwenye mitandao na sisi viongozi wa kijamii, tumekuwa tukiona mijadala inayoendelea katika jamii.

IMG-20190112-WA0000.jpg


Watu wanahisi kwamba sheria hii ni nzito na inaweza ikaleta mabadiliko katika sura ya nchi. Haya ni maneno katika vikao visivyo rasmi mfano kwenye misiba mabasi etc. Watu wanaona inaenda kuwanyima haki. Mfano katika uchambuzi inaonesha msajili anayo mamlaka ya kumzuia mtu yoyote asichague au asishiriki kwa namna yoyote, Mfano Mimi au Kakobe, Gwajima Kilaini na watu wanaofanana na hawa. Mamlaka ya Msajili anaweza akawazuia wasishiriki.

Na hawa watu niliotolea mfano wanaweza wasikubali na hawa watu wanawanaowaunga mkono. Mfano kule Congo, Viongozi wa Katoliki wamepinga sasa hivi hata wananchi wanapinga.. Utaona yamayoendelea..

Nawashauri Wabunge wasikubali. Mwaka 2012 uliletwa muswada wa Ugaidi. Jambo kubwa kwenye ule mswada wa sheria ilikuwa na kuondoa haki za mtuhumiwa. Wabunge wa CCM na upinzani wote waliupinga.

Ukienda kwenye hansadi za Bunge utaona. Wabunge wa chama tawala walitwa wakashinikizwa wakapitisha. Sasa hivi kila mtu anaona, watu wanatekwa, maiti zinaokotwa.

Naomba wabunge wasirudie makosa isipokuwa wajirekebishe kwa maslahi ya taifa sio binafsi.

Makundi yote ya kijamii yamewekeza kwenye siasa, unapogusa siasa umegusa nguvu ya umma. Pale pote unaposikia vurugu ni sehemu ambapo Watawala walichukulia siasa kama mali zao binafsi.


Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Karagwe, Askofu Benson Bagonza, anasema :
Nachukua nafasi hii kushukuru kwa nafasi niliyoipata kushiriki mjadala huu.

Mimi nina mambo manne napenda kujazia na kugusia. Nafanya hivyo kutokea kwenye kona ya kiongozi wa dini.

1. Mimi naona huu si Muswada wa vyama vya siasa bali ni Muswada wa msajili wa vyama vya siasa kwani unampa thamani msajili na kuviondolea thamani vyama vya siasa.

2. Muswada huu una ujasili mkubwa sana wa kuingilia haki za wengine na kuna hatari muswada huu kujenga mazoea ya vyombo vingine kuingilia haki nyingine.. Hii nahofia vyombo vingine vinaweza ingilia uhuru wangu wa kuabudu. Na wengine wataingiliwa uhuru wa kuandika na kuchapicha nakadhalika

IMG-20190112-WA0004.jpg


3. Ninaona muswada huu unaingilia uhuru wa dhamili. Sababu unataja wajibu wa waziri kuvitungia vyama vya siasa kanuni. Waziri ili awe waziri inabidi awe waziri wa chama fulani. Unampa mzigo wa kutunga kanuni wa vyama vingine.. Hatujawa na Waziri wa kutoka vyama vyote. Huyu ndo mnamtwisha waziri mkubwa katika dhamili yake.

Na kwa kuwa waziri huyu anateuliwa na mtu mwingine ambaye ni mwenyekiti wa vyama vingine maana yake mwenyekiti huyu ataviongoza vyama vingine kupitia waziri na msajili. Huo ndo uhuru wa dhamili.

Hata mihimili mingine ya dola Bunge na Mahakama na wao dhamili zao zinaweza kuingiliwa kupitia muswada huu.

4. Muswada huu unamlazimisha msajili asiwe binadamu awe Malaika. Muswada unampa uhuru wa kukaa katikati ya Mungu na binadamu. Amepewa kinga kubwa.

Kuwapa watu wengi kinga ni sawa kumpa uhuru wa kimungu si binadamu na hamfikii Mungu. Anaelea katikati

View attachment 992307

1547281695144.png



Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Vicensia Shule, anasema:
Huu muswada umetunyima nafasi sisi Wanawake kushiriki katika siasa. Tulitegemea uwekwe msingi wa kuamrisha vyama vya siasa kuingiza Wanawake kwenye siasa.

Haujawekwa msingi kwenye rushwa inayowasumbua Wanawake ndani ya vyama.

Tunaendeleza taifa linaloendeleza utata. Hatuweki mipaka.

IMG-20190112-WA0003.jpg


Hawajaweka ufafanuzi wa elimu ya uraia.. Tuna utawala usioturuhusu kufikiri kwa niaba yetu Wananchi.

Wameongelea uraia.. Hapa wote tunajua kwenye siasa ni watu gani wanaambiwa sio raia.. Hii inategemeana na msajili kakupenda

Huu muswada unawapa haki sana, hatuwezi kwenda bila msuguano hii ni fizikia, ili twende zaidi lazima tusuguane zaidi


Professa Azavaeli Lwaitama, anasema;
Muongozo wa TANU ilikuwa ni chama kinakaa ilikuwa sio zidumu fikra za Mkuu... Hapana haikuwa hivyo.

Kuna watu wanapenda sana kutawala, ndio maana tuna wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na sasa msajili naye anataka kutawala vyama vya siasa ? hawa ni watu huru lazima watengenezewe sheria za kuongeza uhuru wao ?

IMG-20190112-WA0005.jpg


Eti kama unataka kufanya elimu ya uraia eti lazima uende kwa Msajili.... Wewe vipi?

Nina mambo matano;
1. Mamlaka ya Msajili. Hii ni dhana ya dola. Je, dola la kinyampala au dola la kiratibu? Huyu alitakiwa asimamie Katiba za vyama kuliko kuwatungia.. Hui ndo uratibu. Kuna wanaojita chama tawala.. Unawalaje watu walio huru? Na msajili anataka kuwa mtawala.

Muongozo wa TANU haukutungwa na Mwenyekiti bali mkutano mkuu. Msajili asiwe msajili awe kama refa.

2. Zana ya siasa. Eti mtu anataka kutoa elimu kuhusu chama chao hadi wamuendee msajili kuomba ruhusa. Mimi natamani tuwe na chama kiwe Afrika nzima. Sasa tunajirudisha nyuma. Watu walio huru, watengeneze sheria zilizo huru. Itikadi sio mwenge au kuvaa nguo za CCM

3. Udhibiti wa hisia. Siku hizi watu wanavaa sana mashati ya rangi ya kijani kuliko wakati wa Mwl Nyerere, lakini watu hawa awajitoi katika kufanyakazi za kujitolea kusaidia jamii? tunaangaika sana na nembo. Mimi nlikuwa najitolea kuchimba mitaro huko dodoma sio kuvaa shati. Shati linaficha mengi.

4. Dhana ya ulinzi. Ulinzi ni wa watu wote. Makampuni ya ulinzi binafsi yanaruhusiwa. Lakini watu wa chama vijana kuamua kumlinda kiongozi wao ni kosa. Akakodi walinzi wakati wao wapo?

Lengo la chama si kushika dola bali ni kishawishi watu wakuunge mkono katika mambo fulani. Dola haishikwi tunayo. Dhamana ya maendeleo ni hatari. Ni dhana ya kuabudu, kuhusudu.

Tulipigania uhuru kuwa huru, na sio kuwa na madaraja au kuabudu vitu, watu wanashinda airport wanashangaa ndege, maendeleo hata wakoloni walifanya lakini wengi tulikuwa na furaha wakati wa Mwl Nyerere ila madaraja machache yalijengwa

Kama mnataka kuweka mambo ya msingi kwenye muswada wekeni yaliyomo kwenye katiba kama ujamaa na demokrasia. Itikadi sio mwenge au kuvaa kijani


Awadhi Ally Said, anasema:
Huu ndo ulikuwa muafaka wa kufanya tathimini kama taifa kuagalia kama taifa tulifanya kosa kuleta vyama vingi au hatukifanya kosa. Mfumo wa vyama vingi unakaribia miaka 30

Tanzania mlango wa Mgombea huru umefungwa. Vimebakia vyama vya siasa. Vyama vya siasa vinakuwa regulated kama TCRA, TCU nk. Sasa siasa ndo inakuwa regulated.

IMG-20190112-WA0002.jpg


Huyu msajili sio anaregulate tu bali anaweza kuthibiti na kuingilia chama cha siasa. Upi ulikuwa ni umuhimu wa kuweka vyama vya siasa? Malengo yalikuwa ni yapi?

Je, malengo yetu ilikuwa kuunda vyama vingi vya wananchi kuchagua mgombea wanayemtaka? Au tunatumia mfumo wa vyama vingi kuidhinisha chama cha kutawala milele? Tunajenga usultan wa kichama.

Unaweza ukawa na chama kimoja halafu kukawa na harakati za kisiasa na ukawa na vyama vingi kusiwe na harakati za kisiasa. Walisema chama kushika hatamu iliondoka, je kweli imeondoka?

Yanga umwambie Simba amchagulie refa hatokubali hao ni wanamichezo tu. Sasa wanataka chama kimoja ndo kisimamie siasa halafu tutegemee kuwe na matokeo ya haki. Haki inatendeka lakini inatakiwa haki ionekane imetendeka.

Tufike wakati hivi vyombo viwe huru ili watu waheshimu maamuzi yao. Tujiulize katika mika 30, huu mfumo wa vyama vingi unasonga mbele.

Dawa ya demokrasi ni moja tu, ni kuongeza demokrasi. Demokrasi haidhibitiwi. Mika ya 80 kulikuwa na gazeti la fahari. Watu walikuwa wanashitakiwa sababu ya hili gazeti.. Watu wanatoa fotocopy lile gazeti walikuwa wanakamatwa.

Mzee Mwinyi akaja akasema magazeti ruksa, ndo mambo ya kukamatwa yakaisha. Dawa ya demokrasi ni kuongeza demokrasia.. Haizuiliki


Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia CHADEMA, John Mnyika, anasema:
Uchambuzi ambao TLS wameufanya tutautumia kuhakikisha nia mbaya ya muswada huu haifanikiwi. Kwa muundo wa Bunge jinsi ulivyo dhaifu na tukataka Bunge liendelee tukidhani haya mambo yaliyomo yanabadilika tutakuwa tunajidanganya.

IMG-20190112-WA0006.jpg


Ni vyema wadau mbalimbali mkashirikisha taasisi nyingine ziende kwa wingi kwenye Kamati ya Bunge kusema huu muswada uondolewe.

Tumezungumiza sana juu ya huu muswada. Mwaka 2017 ulitolewa muswada pendelekezwa baadae ukakanwa. Walichofanya wameondoa baadhi ya mambo kwenye huo muswada wa 2017.

Na ndani ya Bunge mtaona yameingizwa mambo ya ajabu

Msajili alishawahi kuiandikia barua mara nyingi CHADEMA akitisha kukifuta sababu ya ulinzi. Tukawa tunamjibu hana mamlaka hayo basi amarudi nyuma. Sasa wanataka kumpa hayo mamlaka


Mwenyekiti Chama cha Chaumma, Hashim Rungwe anasema:
Huu muswada una mapungufu mengi sana hata viraka havitoshi. Kwa ujumla wetu sisi tunaona huu muswada haufai sababu una mammbo ya jela, faini.

Vyama vya siasa vimeonekana ni kama wahalifu ndio maana wametengenezea sheria. Usipelekwe Bungeni sababu itatokea kichaa akataka kuutetea atazomewa.

Wakina mama wasogee kwenye vyama vya siasa sio kila kitu kubembelezwa tutabembelezana chumbani


Mbunge wa Kigoma mjini na Kiongozi wa chama cha ACT, Zitto Kabwe, anasema:
Kuna watu wanasema vyama vinapinga huu muswada sababu ya ruzuku. Mimi ndo nlipeleka Bungeni mabadiliko ya mdhibiti kukagua vyama vya siasa lakini CCM waligoma.

1547285363098.png


Tulisema 2005 CCM walishindwa sababu ya fedha za EPA na BoT. Baadae Warema akajenga hoja hoja ikapitishwa. Hatukatai mdhibiti kukagua vyama vya siasa. Muswada unasema mtu akipata hati chafu msajili anafuta. Inaonesha aliyeandika muswada hajui mkaguzi mkuu anafanyaje kazi.

Huu muswada sio wa vyama tu. Vyama vya siasa ndio wasemaji wa Wananchi. Mfano kikotoo, vyama vya siasa ndo walikuwa wanapinga


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, anasema:
CCM ni sehemu ya vyama vya siasa vya Tanzania. CCM tusipofuata mambo fulani nasi pia tutakumbana nayo. Ni nini malengo na. Madhumuni ya muswada huu?

1547285380130.png


1. Huu muswada upo katika hatua ya mwanzo ua kutoa maoni. Na wengine wafanye kama TLS. Tusianze kutishwa katikati ya mchakato. Watu wanatisha watu kwamba ondoa kabisa hii, isifike huko Bungeni. Ushwahi kufika?

2. Tunataka sheria ambayo itaimarisha taasisi ya vyama vya siasa. Muswada unakuja kituwekea utaratibu na nidhamu kwenye vyama vya siasa.

Tunataka sheria ambayo itasaidia demokrasia ndani ya chama inaheshimika. Kuna vyama huwa havifanyi uchaguzi tunawajua sema msajili alikuwa hana mamlaka. Vipo vyama Ubunge wa viti maalum kama sio mkewe huwezi kupata. Hata jaji mkuu amechaguliwa na rais, hao hao majaji waliochaguliwa na Magufuli juzi wameenda kwako.

Mimi naona tunatengeneza hofu ya kujitengenezea na tunayaka tuipeleke kwingine. Msajili alikuwa na kinga.

Chama cha siasa kina majukumu yake. NGO isifanye kazi ya siasa.


Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini na Katibu Mkuu chama cha Ada Tadea, John Shibuda, anasema:
Nitakayoyaongea ni maoni yangu. Nimewahi kuwa mjumbe CCM, Mbunge CHADEMA na sasa ni Kiongozi wa vyama visivyo na Wabunge.

Tupo hapa kuzungumzia swala la utaifa sio uCCM na upinzani. Ujana ni maji ya moto. Wakina Polepole, Zitto na Mnyika kuongea kwa munkari ni haki zao za ujana. Acha waongee kwenye ombwe pawe na ujazo. Isiyo kongwe haivushi.

IMG-20190112-WA0007.jpg


Sio penye mifarakano ndo tunaanza kukumbuka mambo ya baba wa taifa.

Hii sheria ni kwa vyama leo vipo kesho havipo.

Tuna kamati za maadili za vyama, kwanini hatuzitumii badala yake tunatunga muswada. Why do we create our empire?

Muswada unasema ukiahama chama ukae mwaka bila kugombea. Sheria hii inadhalilisha CCM. Itafika kipindi utaambiwa kuhama dini moja kwenda nyingine lazima ukae mwaka mmoja ndio uoe. Hebu tuuenzi wosia wa Mwl. Nyerere

Je sheria hii ina changisho la historia ya Tanzania.

Nakuombeni mnaenda huko muichambue. Kwanini msajili umejitengenezea madaraka lakini baraza la vyama vya siasa umevitenga. Maana ya Siasa ni rufaa ya sauti ya jamii. Vijana mlio kwenye maamuzi msiwe na mihemko ya kukomoana. Ukoloni mamboleo tunaunda. Huwezi kuwa mwanasiasa bila kupigwa unyago wa elimu ya uraia.

Tuna tatizo la miaka 30 kufunda vijana kuwa viongozi, Rais Mkapa , Mwinyi na Kikwete hakuandaa. Vijana tuliopo tuliandaliwa na Mwl Nyerere tu. Mtoto wako akiwa chokoraa uwezi lalamika ujamlea, tujenge vijana kuwa viongozi

Sijwahi kuona Askofu anawatengenezea sheria za waislamu, na kamwe sijawahi kuona waislamu wakiitengenezea sheria wakristo.... Tunakwenda wapi?

Huu muswada ni haramu huwezi kuondoa uwe halali. Shame upon us! Nyama ya nguruwe uitie viungo gani iwe halali?

Tanzania bara tunaelekea Zanzibar. Tunaelekea Zanzibar walipotoka wakauana.

Maagano ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni vijana wawe na amsha amsha kama Zitto na Polepole na Mnyika.

Tushindanishe busara na hekima zetu. Kila shilingi ina pande mbili. Dhamira ya huu muswada ni nini?

Nguvu ya chama cha siasa ni hisia za umma. Chama cha siasa sio chama cha kutegemea Polisi na msajili.

Kasoro na kufanya ni kujadili ni vipi tuwe na maendeleo, maendeleo sio chama cha kauli za chuki.

Vyama vinatangatanga sababu vimekosa sikio sikivu.
 
Kwani wakati huo muswada unapitishwa hamkushirikishwa? Je maoni yenu yalikuwa yapi kipindi hicho? Ok nawatakieni mjadala mwema.. zaidi sana mtujuze..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taasisi pekee iliyobaki yenye uwezo wa kutetea HAKI, USAWA na UTU.
Haya maneno nikiyaona naumia sana roho. Taasisi iliyokua nguzo,iliyopaswa kutahwa kwenye hiyo posti yako sasahivi wamekuwa logisticians kule kusini wanafanya shughuli za Metl
 
Yaani hao woote Kiongozi wao ndo huyu Fatuma wa instagram?
Kuna mambo yanawezekana Tanzania tu. Mtu serious Ukimwambia Fatuma ni Rais anaongoza wasomi anaweza hoji wasomi kwa darasa la ngapi?Maana hawezi fikiria kabisa kuhusu Wanasheria wenye masters na PhD zao.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Namuona Mzee Wangu Hashim Rungwe Spunda ile hadisi ya kuwa Vyama vya Uchaguzi tu, watu wameona ni Ungese!
 
Kuna mambo yanawezekana Tanzania tu. Mtu serious Ukimwambia Fatuma ni Rais anaongoza wasomi anaweza hoji wasomi kwa darasa la ngapi?Maana hawezi fikiria kabisa kuhusu Wanasheria wenye masters na PhD zao.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu

Hana tofauti sana na rais wetu.
 
Back
Top Bottom