Dar; Mwanaume ajiua kwa kujirusha kutoka gorofani

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,748
Habari za weekend.

Mwanaume wa Dar amejiua baada ya Kujirusha Kutoka gorofa ya 3 Hadi chini na hivyo kupoteza maisha, Polisi wa DSM wamethibitisha.

----

MWANAMUME ambaye jina lake halijafahamika, amefariki dunia baada ya kudaiwa kujirusha kutoka ghorofa ya tatu kwenye jengo la Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli iliyoko Mbezi Louis mkoani Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea jana asubuhi na kusababisha taharuki kwa watumiaji wa kituo hicho ambacho husafirisha abiria wa ndani na nje ya nchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mtatiro Kitinkwi aliithibitishia Nipashe jana kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema lilitokea majira ya saa mbili asubuhi kituoni huko.

"Ni kweli tukio limetokea majira ya saa 2:30 asubuhi kwenye Stendi ya Magufuli na mtu huyu ambaye ni mwanamume, hajatambulika kwa jina. Anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 42 na 45.

"Amejirusha kutoka ghorofa ya tatu na kufikia kichwa. Mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Tawi la Mloganzila," alifafanua.

Kamanda Mtatiro alisema uchunguzi wa kifo hicho unaendelea ikiwa ni pamoja na kubaini jina lake.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, alidai mtu huyo alionekana akizunguka kwenye eneo la stendi na baadaye alipanda ghorofani.

"Alipanda juu ambako mamalishe hupatumia kwa kupika na kisha akachungulia na kujirusha, akapasuka," alidai shuhuda huyo.

Bingwa Mwandamizi wa Afya na Magonjwa ya Akili MNH na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Afya ya Akili Tanzania (MEHATA), Dk. Saidi Kuganda alisema sababu kuu ya matukio ya mtu kutenda hivyo huwa ni magonjwa ya akili na msongo wa mawazo.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom