Ajifungua na kutupa kichanga maeneo ya Shule

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
MWANAMKE ambaye hajafahamika jina lake na anayedaiwa kuwa ana ulemavu wa akili, amejifungua mtoto mchanga kisha kumtupa kwenye eneo la shule ya msingi Msali "A" iliyopo kijiji cha Ngararambe kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo mkoani Kagera, huku baba wa mtoto huyo akiwa hajulikani.

Akizungumza na Nipashe Digital shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni Diwani wa viti maalumu kata ya Nyakahura, Ziyuni Hussein, amesema kuwa alipokea taarifa za tukio hilo kwa njia ya simu kutoka kwa baadhi ya walimu wa shule hiyo na kwamba alipofika eneo la tukio alishuhudia kichanga hicho kikiwa kimetupwa kwenye mchanga na kulazimika kukichukua kwaajili ya kukihudumia ili kunusuru maisha yake.

Chanzo: Nipashe
 
Kwanini baadhi ya wanaume wanapenda kudinya wanawake wenye matatizo ya akili?
Au ni madomo zege au hawana pesa za kuhonga??
Wanaleta vichanga visivyo na baba.
 
Kuna wanaume ni useless kabisa.

Unampaje mimba kichaa, na ukimpa si uhudumie mtoto sasa.
 
Back
Top Bottom