Ajaribu kujiua baada ya kulazimishwa kuolewa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
JESHI la Polisi Mkoa wa Mtwara, linaendelea kufanya upelelezi juu ya jaribio la kutaka kujiua lililofanywa na binti Zamira Hashimu (20), mkazi wa Kijiji cha Makote wilayani Newala baada ya kudaiwa kunywa sumu ya kuulia panya na kujikata na wembe mguuni baada ya kulazimishwa kuolewa na mwanamke asiyemtaka.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP- Mtaki Kurwijila amesema tukio hilo limetokea Februari 12, 2024, majira ya saa moja usiku.

Amesema binti huyo alikunywa sumu aina ya Ratox, na kisha kujikatakata na wembe kwenye mguu wa kulia kwa lengo la kutaka kujidhuru.

Kamanda Kurwijila amesema Zamira alichukua uamuzi huo baada ya kushinikizwa na dada yake aolewa na mwanamume ambaye alikuwa hamtaki, kwani alihitaji kuendelea na uhusiano na aliyekuwa mpenzi wake ambaye tayari amezaa naye mtoto mmoja.

Source - Nipashe
 
Mambo yakulazimishana ni ya kishamba, Hapo dada mtu alitaka kuuza furaha ya mdogo wake kwa vizawadi vya hapa na pale
 
Back
Top Bottom