Dar es Salaam - Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014
Wakuu,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka jiji la Dar es Salaam. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mkoa wa Dar Es Salaam una jumla ya majimbo ya uchaguzi 10. Wagombea Walioshinda kwenye hayo majimbo ambayo ni;

Ukonga: Waitara Mwita(CHADEMA)

Ilala: Mussa Azzan Zungu (CCM)

Segerea:
Bonna Mosse Kaluwa (CCM)

Temeke: Abdallah Mtolea (CUF) 103,231

Kigamboni: Faustine Ndugulile (CCM)

Mbagala: Issa Mangungu (CCM)

Kawe: Halima Mdee (CHADEMA)

Ubungo: Saed Kubenea (CHADEMA)

Kibamba: John John Mnyika (CHADEMA)

Kinondoni: Maulid Mtulia (CUF)


ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Hapa Kibangu-Ubungo nimeamka saa 10 Usiku, nimekutana watu kama hamsini. Mpaka sasa tupo kama 500 tunasubiri kupiga kura. Wasimamizi wote wapo japo wakala hata mmoja hajafika. Watu ni wastaraab
 
Kwa uelewa wetu Watz huenda tusijue sana kuweka posts kwenye mikoa husika. Napendekeza kuwe na uzi wa general alafu Mods muwe mnaelekeza posts kwenye nyuzi za mikoa husika
 
Sisi wengine tusio na micheche tunawaachia kwanza wenye micheche kujipanga misusuru mikubwa ili kuwahi kupiga kura.

Hii itakuwa ni mara yangu ya 5 kupiga kura, hivyo kwa uzoefu, asubuhi kunakuwa na foleni ndefu, mchana kuko free, hakuna misusuru wala foleni!. Hivyo around milango ya saa 7 mchana ndipo mimi nitajisogeza kituoni sio kwenda kupiga kura tuu, bali kwenda kwenda kupiga kura kwa kukitumia kichinjio changu kuchinjia tuu!.

Nawatakia uchaguzi mwema!.

Pasco
 
Back
Top Bottom