Dalaly Kafumu amekalia kuti kavu Igunga

Bundewe

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
400
141
Mbunge wa Igunga aliyeingia kwa uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka jana Dr. Dalaly Kafumu imeelezwa kuwa amekalia kuti kavu baada ya makamanda kadhaa wa Chadema kufungua kesi ya kupinga ushindi wake. Imeelezwa kwamba kilichopelekea kufungua kesi hiyo ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za uchaguzi ikiwemo waziri wa ujenzi (Magufuli) kutumia ofisi ya serikali kisiasa kwa kuahidi kujenga barabara na daraja kushawishi achaguliwe Dalaly, Kada wa ccm (Rage) kutishia kwa bastola na polisi kutochukua hatua zozote, Daftari la wapiga kura kuchakachuliwa na kuonesha kwamba zaidi ya makada 2000 wa cdm kuonekana wamefariki huku wakiwa hai na wenye afya njema (baadhi yao ndo hao waliofungua kesi).

Source: High Court Registry Tabora.
 
CCM ni wezi professional na wizi wao sasa umeoitiliza ni wa macho kabisa hivi hivi mtu unaona.

Na huyi mke wake tume ngoja awe fair awe anagawa kwa wote na si kwa magamba pekeyao ni hapo timbwiki litakapotokea.
 
wasiwasi wangu mahakama itawalinda ila haki hupiganiwa makamanda msichoke tutawaombea.
 
Huyu mb huwa namuona mlandizi akinunua mahindi ya kuchoma na kuelekea kwenye mashamba yake huko vikuruti. Wana igunga hapa wamelamba galasa.
 
Igunga nilikuwepo kwenye uchaguzi mdogo na nilishuhudia mengi ya uvunjwaji wa kanuni za uchaguzi kwa vigogo wa ccm but my take ni kwamba mahakam haitaweza kutengua ushindi ule kwani ipo kutumika kisiasa so cha kufanya ni kuelekeza nguvu zaidi ktk kusambaza elimu ya uraia kwa wananchi kwani am sure CDM itachukua jimbo hilo 2015,
MUNGU IBARIKI CHADEMA.
 
Huyu mb huwa namuona mlandizi akinunua mahindi ya kuchoma na kuelekea kwenye mashamba yake huko vikuruti. Wana igunga hapa wamelamba galasa.
Sio wamelamba bali wamelambishwa, lakin hata hivo hayo walishayazowea tangu enzi za LA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom