Kwa bahati mbaya mimi sikuona hayo majadiliano na Mh. Ndugai.
Swali kubwa ninalojiuliza ni kwa nini mambo ya posho na maslahi ya wafanyakazi wa serikali yamewekwa siri? Miaka ya zamani, enzi za JKN niliwahi kufanya kazi serikalini. Mishahara na marupurupu yote ya wafanyakazi serikalini yalikuwa bayana. Leo ni siri kubwa. Nadhani usiri huu umeandamana pamoja na wizi/uporaji. Nchi nyingi duniani zinaweka wazi mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa serikali, na sisi lazima tulazimishe iwe hivyo. Tuone madudu yanayofanyika huko.
Matumizi ya serikali ya Tanzania ni ya kifahari sana. Posho zao za safari za nje za USD600 kwa siku ni kubwa kupita nchi nyingi duniani, na nadhani ni kupita hata wafanyakazi wa UN. Wakati mawaziri wa nchi kadhaa duniani wanapanda ndege daraja la tatu (tourist) ikiwa safari ni chini ya masaa fulani wafanyakazi wengi wa serikali ya Tanzania wanasafiri daraja la kwanza au business. Hivi kweli tuna akili?
Serikali inabidi ituondolee uchafu huu.