Dakika 45 ITV: Jobu Ndugai apasua siri jinsi nchi inavyofilisiwa na serikali iliyoko madarakani

Tanzania yetu kweli imeisha, but its true fikiria posho wanazolipwa watumishi wa umma wa foreign affairs na idara zingine inapotokea wamesafiri na mh rais nje ya nchi. na kama mjuavyo safari za mkuu wa nchi

SHILINGI NGAPI KWANI? LAKINI SI INABIDI IENDANE NA MATUMIZI YA FEDHA ZA HUKO AENDAKO? CHA MSIngi ni kudhibiti safari zisizo na tija
 
Akili yangu inasita kukubaliana na hilo jambo, manake nikiona flow ya watu hata kama ni mabosi kwenye mashirika mengine bado wanaacha huko wakikimbilia bungeni. Sijawahi kuona mtu aliyeacha UBUNGE kisa kapata kazi ya ukurugenzi NSSF, TANAPA au hata TRA alizozisema. Hii inamaanisha nini? ni kuwa bungeni ni mahali BEST kuliko pote?
 
Nilikuwa nasikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania MAT Jana akihojiwa Redio Clouds, Kipindi cha Jahazi, Huwezi amini Daktari analipwa Posho ya sh za kitanzania less than 500 Kwa saa. Na anafanya kazi 24 hours ana ambulia 10,000 na kesho yake anaunganisha kazi. Ama kweli ngonja nijiandae kukamata jimbo, Bingo iko kwenye siasa sio kwenye professional.
Mbunge std 7 or form.... Failure anakamata 200,000. Dr Darasani more than 20 years 10,000. Hakuna kabisa uwiano
 
Job Ndugai kanisikitisha.
Nae anaingia kwenye orodha ya magamba yasiyofaa kuwa viongozi wa uma.
How the hell did he become a deputy speaker?
OTIS
Ajabu OTIS kuwageuka mabwana zake, ama kweli nyota imechomoza!
 
Haya ni matunda ya serikali corrupt. Kuhonga killa anayekuwa tishio ili ibaki madarakani.

Majaji wanalipwa posho kubwa sana lakini ni nani anayewapangia na kuwalipa?

Serikali hii ni janga la kitaifa. Badala ya kuwaendeleza watu wake, na kujilinda kazi yake ni kuhonga kwa kwenda mbele.
 
Naibu Spika Jobu Ndugai amedai kuwa watanzania inabidi wasilaumu sana wabunge kuongezewa posho, Ndugai kasema kuwa kuna muhimili mitatu ya nchi ambayo niBUNGE, SERIKALI NAMAHAKAMA, Ndugai kasema kama watanzania wangejua ni kiasi cha posho kubwa wanacholipwa viongozi wa seikali na mahakama basi watanzania wangejinyonga kabisa badala ya kulaumu hizi wabunge ambacho ambacho kadai kuwa ni kidogo kuliko wananchi wanavyofikilia,

Hii kauli ya Ndugai ilimshitua hadi mtangazaji baada ya kusikia kuwa nchi hii kuna zaiudi ya maefu ya wafanyakazi wanapokea posho za kutisha kuliko hata wabunge, Ndugai kadai wabunge ni wafanyakazi wasiozidi hata 350 lakini ndoo wamenyooshewa kidole na waandishi wa habari bila kufahamu kuwa kuna posho zinalipwa mara 10 zaidi ya hizo zao kwa siku na kudai kuwa ni maelfu ya wafanyakazi wa mihimili ya serikali na mahakama na hii ndoo imefanya hadi wabunge waamue kujiongezea.

Mimi nadhani hii inaonesha ni kwa jinsi gani, angalau kwa kumwangalia Ndugai, viongozi wetu, ama kwa kujua au kutokujua, wasivyojua kazi na majukumu yao ya msingi. Hivi hapo kwenye red ndio kaongea nini? Kumbe yeye, au niseme Bunge, wanayajua hayo yote ila badala ya kuchukua hatua wamekaa kimya tu? Kwao suluhusho ni kutaka nao waongezewe? Eti wako wachache - 350!

Mwenye mamlaka ya kuzuia hujuma "hujuma" hizo za serikali na mahakama (eti mihimili) kulihujumu taifa kwa gharama ya wanyonge ni Bunge ambacho ndicho chombo cha uwakilishi wa wananchi! Kama chombo hiki (Bunge) nacho kimeamua ku-practice unyang'au ndipo wananchi tunapopiga kelele angalaui kupitia taasisi chache adilifu zilizobaki iwe vyama vya siasa, asasi za kiraia, n.k. Watu wakitaka kuandamana kulaani wizi kama huu ni hao hao akina Ndugai wanakuwa wa kwanza kuleta vitisho, wakinyamaza ndio hivyo tena hao hao akina Ndugai wanawaibia wananchi! Sijui hapa wananchi wafanye nini?

Kwa ufupi haya yote yanayotekea hapa nchini ni matokeo ya mhimili mmoja kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo na mhimili huo ni Bunge. Leo hii Bunge likiamua kufuta ufisadi na ubadhirifu wote ulioko Serikalini au Mahakamani kama anavyodai Ndugai, linaweza tena lina mamlaka kamili ya kufanya hivyo. Bunge likiamua kuitimua serikali lina mamlaka ya kufanya hivyo. Bunge lina mamlaka yote kwa NIABA YA WANANCHI.

Ndugai, timizeni wajibu wenu acheni kubwabwaja, mmepewa mamlaka yote. Simameni upande wa wananchi mtaheshimiwa badala ya kutamani kula haramu kama wenzenu.
Lakini sitegemei lolote la maana kutoka kwa Bunge hili ambalo wakati mwingine hujigeuza kuwa KAMATI YA CHAMA.
 
Napingana na Job kujustify wizi kwa sababu wengine wanaiba pia. hebu tuwe na huruma kwa watanzania itafika mahala tutagoma kulipa kodi sijui mtajisikiaje. Nalaumu wengi wa sisi watanganyika tuna nidhamu ya uoga. Kwa upande wa posho ktk mihimili mingine atuambie ni kiwango gani cha posho wanazopata mwenye dondoo atuwekee kidogo. Mimi huwa naona kuna kitu hii inaitwa per DM if am not wrong kwa mfanyakazi wa kawaida aendae nje ya nchi ni zaidi ya dola 600 kwa siku x 1600 =960000 Kwa JK na timu yake? Inawezekana wabunge wengi hawapati hii kwa sababu vikao vyafanyika dodoma ambayo ni ndani ya nchi. Halafu tunadanganywa kwamba sisi ni waajiri wao thubutu? Mwajili gani hajui mfanyakazi wake anajilipa ngapi?

Du ! ,Kumbe hadi Ikulu wanalipana ina Dollars ?
Nadhani ni muda muafaka wa kuweka hadharani mishahara na posho za kila mtumishi wa umma ,
Na za kufutwa zifutwe mapema kabisa,
Zito ,uko wapi kakaangu , ebu koroma tena , wembe ni ule ule......
 
Hii kauli ya Ndugai ilimshitua hadi mtangazaji baada ya kusikia kuwa nchi hii kuna zaiudi ya maefu ya wafanyakazi wanapokea posho za kutisha kuliko hata wabunge, Ndugai kadai wabunge ni wafanyakazi wasiozidi hata 350 lakini ndoo wamenyooshewa kidole na waandishi wa habari bila kufahamu kuwa kuna posho zinalipwa mara 10 zaidi ya hizo zao kwa siku na kudai kuwa ni maelfu ya wafanyakazi wa mihimili ya serikali na mahakama na hii ndoo imefanya hadi wabunge waamue kujiongezea.

Kwa hiyo Ndugai anachotaka kusema hapa ni kwamba Serikali yetu anaithamini mihili miwili tu na muhili wa tatu umesahaulika? Fine, hata Ngugai ambaye ni mwakilishi wa wananchi hajaona umhimu wa kuwafikilia hata watu wa kima cha chini? Je, wakulima na mazao yao yanayonunuliwa kwa bei isiyoendana na gharama za usharishaji? Mfuko wa mbolea inayoitwa ya RUZUKU ya kupandia mahindi (DAP) inauzwa zaidi ya 70,000/= ilihali gunia moja la mahindi haliuzwi hata nusu ya bei ya mfuko wa mbole? Huo ni ubifasi wa hali ya juu!!!
 
Ndugai asifananishe majaji na wabunge, majaji ni proffesional wakati wabunge ni siasa tu mdomoni. kweli ccm imekuwa kila kiongozi ni kambale, mtoto ana ndevu, mama ana mdevu na baba ana ndevu. hakuna kuheshimiana.

Mkuu kwahiyo unamanisha wafanyakazi wa mahakama ndo wanastaili posho kubwa kwasababu ya merit je walimu na manesi?
 
Akili yangu inasita kukubaliana na hilo jambo, manake nikiona flow ya watu hata kama ni mabosi kwenye mashirika mengine bado wanaacha huko wakikimbilia bungeni. Sijawahi kuona mtu aliyeacha UBUNGE kisa kapata kazi ya ukurugenzi NSSF, TANAPA au hata TRA alizozisema. Hii inamaanisha nini? ni kuwa bungeni ni mahali BEST kuliko pote?
Unajua ni kwa nini? Bungeni ni sehemu pekee unapoweza kuchapa usingizi kutwa nzima na bado ukalipwa malipo makubwa bila wasiwasi wowote. Ndani ya Bunge letu nakuhakikishia wabunge hasa na watimiza wajibu hawazidi 70.
 
Nilkuwa sijui kama wabunge ni wafanyakazi. Kumbe ukipigiwa kura unapata ajira? Huyu jamaa nadhani uwezo wake wa kuelewa ni mdogo sana unless amenukuliwa vibaya......kazi za kuchaguliwa mara nyingi zinapaswa kuwa za kujitolea

kujitolea?kama unataka kujitolea kuna haja ya kutoa HONGO?
 
Hata mimi nimemsikiliza ila nilikerwa na pale anapolaumu wananchi kwa kuwanyooshea wao vidole, nikajiuliza kama wao wameamua kufanya siri baadhi ya mambo serikalini sisi tutafahamu vipi?? Aweke wazi ili kama kuna wengine wenye posho za ajabu tuweze kuzitathmini na kufanya maamuzi...

Hii ishu ya usiri..usiri itaimaliza Tanzania...

Nikaona pia anaingilia hadi secta binafsi kwamba nao wazibitiwe..nikachoka kabisa. Hivi leo hii nikiamua kumlipa house girl wangu laki tano ni kosa?? Sijatumia fedha ya walipa kodi bali nimetumia fedha yangu binafsi. Mbona tunarudishana enzi za Mwalimu???

Sisi tunahoji kodi yetu inayotumika vibaya...
 
Na mimi pia nimeangalia hicho kipindi.
Nimekuwa nikisikia watu wanasema eti huyo bwana ni bora zaidi ya bosi wake Mama Makinda, sasa kwa maelezo yake ukichukulia na aina ya mwandishi aliyekuwa anamuhoji (fakiria angelikuwa akipokea simu kutoka wa watazamaji) ndio unagundua kuwa either nchi imeishiwa vipaji au tumeamua kutawaliwa na watu wasio na uwezo au wenye malengo tofauti na viapo vyao!
Anasema kuwa Watanzania tunalalamika lakini na yeye kaishia kulalamika vilevile na juu ya yote kumsifia JK kana kwamba nchi inatawaliwa na CUF/cdm
Job Ndugai kanisikitisha.
Nae anaingia kwenye orodha ya magamba yasiyofaa kuwa viongozi wa uma.
How the hell did he become a deputy speaker?
OTIS
Huyo Ndugai hana jipya, yeye na Makinda walipaswa kuliongoza Bunge kukataa posho na baadae wangeweza kuisimamia uondoaji wa baadhi ya posho kwenye Serikali na Mahakama. Anachothibitisha sasa ni ulafi wa Wabunge kwa kisingizio cha "mihimili mingine pia kufanya jambo hilo."
 
Na kwa taarifa yenu msiojua...huyu ndio miongoni mwa wale wabunge waliopita bila kupingwa 2010....!Nawaonea huruma sana wananchi wa jimbo la Kongwa
 
Tatizo lingine ni hawa waandishi wetu...... Hapa alitakiwa kumhoji zaidi ili kumvua nguo huyu Job Ndugai.
Swali kama 'Je nyie kama bunge si mnaweza kusimamia masuala ya posho hata ya mihimili mingine maana inapata ruksa yenu,, je yeye Ndugai kafanya nini kwa niaba ya wale ambao anasema wakijua watalia machozi? maana wao wabunge wapo kwa niaba ya hawa walia machozi!'
Au
'Je kwa nini baada ya Chadema kulizungumzia suala la kufuta posho msingeanzia hapo kuangalia posho zote katika mihimili yote zinafutwa badala yake wewe na wabunge wa chama chako mkiongozwa na waziri mkuu mkawa wakali mkitetea uwepo wa posho hizi? huoni kwa kuwepo posho hizo kwenu wabunge inawafanya kukosa ujasili wa kuhoji mihimili mingine?'
Waandishi wetu katika media mara nyingi wametuangusha sana. Au hawajui nini cha kuuliza au ni waoga kwa wanaohojiwa,
 
Ndugai kama mbunge aliye kwenye muhimili mkuu wa serikali ambao kazi yake kubwa ni kuinyooshea serikali vidole na yeye kama Naibu speaker huu siujinga inamaana hajui hata kazi ya Bunge .............

Hata hivyo hawa tunaowachagua hawajitambui ndio maana anaamua kusema haya .....ni mwezi uliopita Waziri alijitosa kwenye vyombo vya habari na kusemaangekuwa na uwezi angewafunga wauza mafuta wakati yeye ndio waziri wa wizara husika....
 
Hapa naamini Ndugai alikuwa akitetea posho zao ili watu wahamie kwenye posho za mihimili mingine ili wasahau posho walizoongezeana bungeni, hiii ndoo nchi ya TZ duuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!
 
Siamini kama Ndugai anaweza kuongea ushenzi wa hivi... Hafai tena hafai hata kidogo... Na kama yupo humu JF basi ajue AMELAANIWA si bure..
 
Back
Top Bottom