Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

Nilichokisema ni hakuna mtoto wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye kwa sasa yuko kwenye vyama vya upinzani na siyo mtoto wa familia ya Nyerere.
Mheshimiwa Letcia Nyerere,
MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

Mwenyekiti huyo wa CCM na Madaraka ni watoto wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.

Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba.

Kampeni hizo zilizinduliwa katika mji mdogo wa Hungumalwa, wilayani Kwimba.

Katika uzinduzi huo, Makongoro alielezea kushangazwa kwake juu ya hatua ya viongozi wa Chadema na Leticia, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika kujinadi kwa wapiga kura.

Alisema hata hivyo kitendo hicho kinacholenga katika kumwezesha mgombea huyo wa Chadema kuchaguliwa, hakitasaidia hata kidogo kushinda katika uchaguzi huo.

Alisisitiza kuwa ni makosa kwa mgombea huyo kutumia jina la ukoo wa Nyerere kujinadi, hasa ikizingatiwa kuwa ndoa baina yake na mdogo wake (Madaraka) haipo tena.

Kwa mujibu wa Makongoro, wanandoa hao walitengana miaka 12 iliyopita baada ya kutofautiana.

"Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.

Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.

Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.

"Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.

Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu.
 
Unajua nashangazwaga na kitu kimoja. Mtu akihama chama kwanini harudishi kadi kwa wenyewe anaipeleka huko anakohamia? Hii ni sawa kweli? Hiyo kadi ni ya nani hasa, sio ya chama husika anachokihama?
Wakati Mwenyekiti wa taifa CHADEMA mh Freeman Mbowe na baadhi ya Wabunge wakihojiwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kwa kile kinachodaiwa na jeshi hilo ni kupitiliza muda wa kuhutubia ktk mkutano uliofanyika siku ya jumamosi, Dada yake na Mbowe GRESI MBOWE,ameamua kuikacha CHADEMA na hatimae kujiunga na CCM!!

SOURCE; Gazeti la Uhuru (Radio Free Afrika)
 
Mbowe ni ukoo mkubwa sana.....Lete habari kamili ni Mbowe yupi...?

Haya ndiyo maneno ya Dada mtu wakati anakabidhi kadi ya CDM:
“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia Chadema. Nadhani utakuwa umepata jibu la swali lako mkuu.
 
kimsingi chadema ni chama cha kifamilia hilo lipo wazi wala haliitaji phd kulitambua.

Mmiliki wa chadema ni mtei, na mwenyikiti wa chadema ni mbowe, ambaye ni mkwe wa mtei,

kuna uwezekano mkubwa wa kimaslahi ndani ya familia ndiyo maana grace mbowe, kuamua kuondoka chadema na kwenda ccm.

Tutasikia mengi pindi grace mbowe, atakapofunguka zaidi.

pole! Kwa hiyo wote tuje ccm? Et mke wa mtoto wa rais ana mkopo 100% hilo tu linatosha kuniua, wala usinitafute mi ninayesoma kwa kuuza ubuyu huku jk akiahid mikopo kwa walalahoi, leo mke wa mtu mlalahoi? Achen waje ila kamwe usitarajie mtu anayejitambua kuja ccm, huko wote hamjitambui, mnajua kuiba na kunyonya kama unavyowanyonya wakaz wa dodoma kwa kununua maeneo yao kwa kigezo cha umaskin. Kama mwakyembe alivyosema, usinitafute kuniua nilishakufa zaman.
 
5380448_orig.jpg
9892981_orig.jpg
Bi Grace Mbowe, ambaye ni dada yake Freeman Mbowe, akikabidhi kadi ya chadema na kukabidhiwa ya ccm na katibu wa ccm wilaya ya Hai ndugu Hassan Mtenga. c.c. ritz, hamy - d, tumaini makene na ben saanane
 
Watoto wa wasira walivo hamia chadema naona hapa pali waka moto, kila mada wasira..... hapo jeeee!
 
Wakati Mwenyekiti wa taifa
CHADEMA mh Freeman Mbowe na baadhi ya Wabunge wakihojiwa na jeshi la
polisi mkoani Iringa kwa kile kinachodaiwa na jeshi hilo ni kupitiliza
muda wa kuhutubia ktk mkutano uliofanyika siku ya jumamosi, Dada yake
na Mbowe GRESI MBOWE,ameamua kuikacha CHADEMA na hatimae kujiunga na
CCM!!

SOURCE; Gazeti la Uhuru (Radio Free Afrika)

Nilikuwa nabwia unga kidogo hapo kwa Yahya unaishi wapi aka Idd Azan. Dah huyo Grace kimwili Ccm,roho na nafsi CDM damu.
 
Ni mchovu wala kuondoka kwake hakuna impact. Siasa za upinzani zahitaji moyo na uthubutu. Puya hutokea utakapoloweka mchele. Halafu angepiga hatua aende panakoendeka, yeye karudi mahabusu badala ya uraiani. Kichagga "HENDESHIKA NDETIKO"
 
Kama ccm sio ukoo wa kikwete na magfisadi wengine nawewe hamia chama kingine kuonyesha uzalendo. Unatafutwa na wachina kwa tuthuma za madawa ya kulevya.
 
mletauzi akiliyako haina akili hebu jiulize na ujijibu hiliswali dogo sana mbona mtoto wa nyerere yuko upinzani,ilihali babayake alikua mwenyekiti na mwasisi wa ccm ?

Aende tu kwa hao magamba alidhani akiwa chadema mbowe atampacheo kwasababu ni dadayake kama wanavyofanya magamba?
Mbowe ni GT,uyo mdada alidhani kaka mwenyekiti yeye atakuwa katibu akasahau chadema sio mali ya Mbowe niyawatanzania,amebugi bora aondoke kwa sababu tutampa kazi ya kufunga na kufungua mageti...
Viva chadema..
 
Du waafrica cku zote wanafiki tu yani haoni jipya akiwa CDM na CCM ni ileile sidhani kama wewe ni kijana wa enzi za Mwalimu.unaeona CCM ya Nyerere ni kama hii ya leo? kweli Dada uko seliously? Hizi pesa tutaziacha jamani hii c kama kutaka kuwambia watu kuwa Rangi ya damu ni nyeupe?
Kaja chadema akifikiri atalipa madeni,huoni alivyochoka hahahaaaaa,chadema sio chawachumia matumbo,nenda tu bi mkubwa Nape na Mwigulu watakufadhili na utauza Unga kwa kwenda mbele..
 
Napenda kuwaeleza kama hamjui, Kila mtu na nafsi yake. CCM mmechemsha kama hiyo ndo mbinu. Unajua kabisa jinsi wanawake wanavyodanganyika na mambo madogo: hiyo kofia na kitambaa tuuuuu!! Hiyo mbinu ni ndogo. Labda pia kaahidiwa udiwani wa maneno na ameona CHADEMA hawana mpango naye, kuhama hama kunaonesha udhaifu wa mtu. Kwani alikuja CHADEMA akitoka wapi? Mbowe songa mbele. Baba na Mama waweza Kukuacha lakini usikate tama na unachifanya as long as huna hila ndani yako.
 
Kwani huyo Grace Mbowe alikuwa na wadhifa gani ndani ya Chadema? Mbona sijawahi kumsikia?
Huyu anamzidi Freeman umri, na anadai tangu ameifahamu CCM iko vilevile haijabadilika. Atakuwa na matatizo huyu. Ni sahihi kwake kutokuwa na wadhifa wowote ndani ya CDM, na kuondokewa na wanachama wa aina yake ni faraja.
 
Mimi nina imani kuwa kuhamia kwake CCM kuna mahusiano na jinsia yake kama mwanamke na sio nafsi ukizingatia kuwa akiwa Chadema wanaume wengi licha ya kumheshimu, pia walimwogopa kwa sababu ya kuwa ndugu wa Mwenyekiti wao Bwana Mbowe. Jinsia yake ilipata wakati mgumu lakini kwa sasa iko huru ingawa nafsi itaendelea kumsuta kwani haijahama wala haitahama Chadema. jibu litakuwa wazi pindi Chadema ikiingia ikulu na kaka yake akashika nafasi ya waziri mkuu. Isitoshe kaka yake anawindwa sana na mafisadi kwa mabomu na risasi ili auwawe, hivyo uwepo wa dada huyo CCM unaweza kuzima harakati hizo ... si atakuwa shemeji. Kwa hilo nampongeza huyo dada kwa kuhamia CCM maana amecheza kama messi na CCM kwa kutokujua wanashangilia bila kujua hilo ni bao la kisigino.
 
Back
Top Bottom