CWT yasisitiza mgomo upo palepale Jumatatu tar 30/07/2012

Ina maana hujui kufanya analysis ya nilichokiandika hapo au nini tatizo? usiwe na hasira ndugu ukiangalia hapa utaona ni jinsi gani CWT wanatumbua mipesa sasa hivi na kuandikia hizi Millions zimetumika katika kipindi cha kuhamasisha mgomo wakati wanajua ...kuwa hakuna lolote litakalofanikiwa....CWT ni wahuni kama hujui hilo shauri yako.
shauri yako ww na familia yako kwa taarifa yako mgomo huu haujahamasishwa hakuna mwalimu asiye fahamu kama ananyanyaswa na serikali hii dhalimu. wala haihitaji kampeni kuhusu madai ya walimu hata mtoto mdogo anafahamu kuwa mwalimu anaonewa. ww umetumwa tuu hata kama cwt wanamatatizo huu sio wakati wake sasa tupo kwenye mapambano hainahaja ya kulaumiana. funga domo lako
 
ukiamua inawezekana walimu maanishe kwenye hili komaeni maana naona kama hakuna umoja hii nchi bila kukomaa lazima wakupunje onyesheni solidarity ya hali juu wote mkiamua kwa pamoja lazima watatoa maamuzi pesa ipo ila wachache wanaitafuna.
 
Kesho mwache ujinga,unafiki,ukigeugeu wenu nyote shikamaneni ili mboreshewe hali zenu kimaisha ili nanyi muishi kama watumishi wengine ktk nchi hii.Msiendelee kuwa ombaomba,kuvaa ngouo zenye viraka viraka,kugeuzwa wake wa Maafisa Elimu.Fursa ya kuleta mabadiliko ni sasa itumieni usaliti usiwepo.
 
Ni kweli ukombozi wa mtu uko mikononi mwake hivyo ukombozi wetu uko mikononi mwetu, Naomba hata Mkoba utuelewe hata hiyo mahakama ikileta zuio la mgomo naomba tukatae tunachotaka madai yetu yatatuliwe, walimu tusikubali kutishiwa na akina majaliwa na akina mlugo wanajifanya wao ni miungu watu.

Ikibidi kufukuzwa bora watufukuze wote na mahakama ndo zikafundishe. Tangu watu wa afya walipooungana kudai nyongeza za mishahra leo wanalipwa zaidi ya sisi walimu japo mwanzoni tulikuwa sawa. Basi walimu tukomae ili kuwadhihirishia kuwa tumechoka kuonewa, kudharauliwa, kupuuzwa, kutishwa, kudhurumiwa, kutukanwa na kunyanyasika.

Nia ya mgomo tunayo, sababu za kugoma tunazo na uwezo wa kugoma tunao kwa pamoja tuseme hapana kuonewa, kwani wao wana nini waifaidi nchi peke yao na sisi tuna nini tushindwe kufaidi matunda ya nchi yetu!!!!!!!!
 
Akitangaza kupitia kituo cha itv naibu katibu wa chama cha walimu cwt mwl. Ezekiel amesema mgomo unaanza rasmi tar.30/07/2012 kwa kuwataka walimu wote kubaki nyumbani hadi hapo watakapopata maelekezo mengine kutoka kwa rais wa chama hicho mwl. Gration mukoba. Haya na tusubiri kuona nao kama watafukuzwa kama madaktari.
 
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimesisitiza kuwa, mgomo wake uliopangwa kuanza leo upo palepale.
Hatua hiyo ya CWT imekuja siku moja baada ya Serikali kutangaza kuwa mgomo huo ni batili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba ameitaka Serikali kuacha vitisho dhidi ya walimu.
Alisema kuwa Serikali imekuwa ikiwalazimisha walimu kujaza fomu zinazowataka kuorodhesha majina yao na shule wanazofundisha na kueleza kama wanaunga mkono mgomo huo au la.CWT imesema walimu wanatakiwa kushiriki mgomo huo kwa kuwa ni halali na umeitishwa na chama hicho kwa kufuata taratibu zinazotakiwa.
Mukoba alisema, Baraza la CWT lilitoa notisi ya saa 48 kuanzia jana (juzi) saa 8 mchana, ambayo inamalizika leo saa 8 mchana, kisha kutangaza rasmi kuwa utekelezaji wa azma yao ya kugoma unaanza kesho.
“Walimu wataanza mgomo rasmi Jumatatu (kesho), kwa kubaki nyumbani bila ya kwenda kazini hadi watakapotaarifiwa vinginevyo na Rais wa CWT,” alisema Mukoba.
Alisema kuwa, wanachama waliopiga kura kuamua kuwepo kwa mgomo walikuwa 183,000 ambapo kati yao 153,000 waliunga mkono azimio hilo wakiwa sawa na asilimia 95.7 ya wanachama, hivyo kuhalalisha mgomo huo.
Hata hivyo, Mkoba alisema kuwa mgomo huo hautahusiana na zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 26, mwaka huu ambapo aliwataka walimu kushiriki kikamilifu.

“Walimu wanahakikishiwa kuwa mgomo hautaathiri utumishi wao kwa kuwa umezingatia sheria, ingawa tunategemea kuwapo kwa vitisho na propaganda nyingi kutoka kwa waajiri wetu,” alisema Mukoba.Mukoba alieleza kuwa mgogoro uliotangazwa na walimu kupitia CWT ulishindikana kusuluhishwa na msuluhishi aliyeteuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
"Nawataka walimu wote nchini kuungana na kuhakikisha kuwa mnashiriki zoezi hili lenye lengo la kumshinikiza mwajiri wetu (Serikali) kusikiliza madai yetu," alisema.
Alhamisi wiki hii CWT ilitangaza mgomo wa walimu nchi nzima kupinga Serikali kushindwa kuwatimizia madai yao ya siku nyingi ikiwamo ongezeko la mishahara.
Madai ya walimu
Madai ambayo walimu wamekuwa wakiitaka Serikali kuyatafutia ufumbuzi ni pamoja na ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa Sayansi asilimia 55, asilimia 50 kwa walimu wa masomo ya sanaa na posho kwa walimu wanaoishi katika mazingira magumu.Mgogoro kati ya CWT na Serikali umedumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa, ambapo licha ya ahadi ya kulipwa madai hayo, fedha zimekuwa hazikidhi ukubwa wa tatizo na kusababisha madeni kurundikana.
 
Fisadi moja tu likijiachia walimu wote watacheka na mgomo tena basi. Gomeni walimu, sijui kama mnapata chalk dust allowance? Kama sivyo na hili daini.
 
Hadi hivi sasa Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba anaeleza mgomo upo pale plae na hawatorudi nyuma kwa lolote lile naliwe au liwatoke ,lakini inasemekana kama lisa moja hivi amepokea Ujumbe unaosema kushuhulikiwa kwake kutafanyika wakati wowote pale mgomo utakapo fanyika na kumalizika.
 
safi sana ..wamezoea kusahau wanyonge na kukumbatia mafisadi...sijui watasema na kwa hili CDM iko nyuma ya pazia..
 
Halafu walisema hawatagomea sensa, maana wanajua washavuta fungu. kweli mwalimu ni mwalimu tu na atabali kuwa mwalimu.
 
CWT imefuata taratibu zote za mgomo.Hivyo kesho mgomo kama kawaida.Ngoma inogile.
Source itv.
 
huu mgomo na hizi nyuzi humu jf zinaweza kuwa ni za 20 na kitu huko halafu kesho utasikia no mgomo :msela:
 
Nipo sehemu moja kijijini huku maeneo ya Serengeti nimekaa na walimu s/m wanasema mgomo uko palepale. Ni mara yangu ya kwanza kuona kuna muamko mkubwa wa walimu sasahivi.

Huko Serengeti nyumbani kwetu ndugu na baba yangu ni mwalimu pia huko
 
Ushauri Walimu msigome chonde chonde! Madaktari hawafanani na watu wa aina yeyote Tanzania kwa hali yoyote, wanawadanganya hao wakubwa zenu wanatafuta UMAARUFU. Mwisho wa siku mtayatoa yaliyo sirini mkawe Mbuzi wa KAFARA.
 
Akitangaza kupitia kituo cha itv naibu katibu wa chama cha walimu cwt mwl. Ezekiel amesema mgomo unaanza rasmi tar.30/07/2012 kwa kuwataka walimu wote kubaki nyumbani hadi hapo watakapopata maelekezo mengine kutoka kwa rais wa chama hicho mwl. Gration mukoba. Haya na tusubiri kuona nao kama watafukuzwa kama madaktari.

Mmewaelimisha wanafunzi wa boarding wasije wakakosa uji wa asubuhi na kupiga kiberiti shule.
 
Back
Top Bottom