CWT yasisitiza mgomo upo palepale Jumatatu tar 30/07/2012

haya gomeni tuone serikali itakavyowatumia wanajeshi kufundisha..!!! shaka hakuna itabidi wawashirikishe police, magereza na wafungwa ili waweze ku cover nafasi za walimu... sina shaka kuwa kesho walimu mtaanza mgomo ila nna wasiwasi na muda mtakaogoma.. nna mashaka j4 mtarudi clas kama kawa, ndio zenu.. tushawazoea..
 
madaktari vipi? wao wamenywea? au ndio wanaendesha mgomo baridi unaendelea kunyofoa roho za watanganyika bila huruma? ingekuwa busara mkaungana na walimu!

Kuna mgomo mkali wa madaktari unaendelea chini kwa chini aisee.
Walim wao walishagoma kitambo sana hadi kesho bado wamegoma tu.Hakuna mgomo mpya wa walim bali ni mwendelezo tuuu...
 
Walimu lazima tugome,mimi mmoja wapo! Nasisitiza nitagoma mpaka kieleweke! Shule yangu ina f1 - f4,nafundisha physics and maths madarasa yote,mikondo ipo 10,kwa mwezi 273,000/= mbunge kwa siku zaidi ya 200,000 kutukanana tu . . Analipwa! Mm napauka na chaki,tuwe wazalendo! Usipondee ualimu wakati hujui chochote
 
Baada ya madokta kufanikiwa kuvuka mstari wa vitisho uliokuwa ukichorwa na Dhaifu na Liwalo na Liwe sasa walimu njia Nyeupe. Usalama wa taifa hawatakuwa tayari kudharirishwa kama ambavyo imetokea walipojaribu kumuua Bila mafanikio Dr. STEVEN Ulimboka, ni wazi kwamba hawatakuwa tayari kwa sasa kutumiwa na Dhaifu kumteka Rais wa CWT Ndg Mkoba, kwa hiyo Walimu wanapaswa kuitumia vizuri damu iliyokwishamwagika ya Dr. ULIMBOKA kudai maslahi yao. Njia Nyeupee washndwe wao wenyewe tu.
 
walimu tukomae jwtz walikuwa wanalipwa posho ya nyumba then wakadai ya umeme na maji bajeti mpya wanaanza kulipwa
 
Unajidanganya na kauli zako za kichawi dhidi ya cwt sasa wambie serikali haturudi nyuma mgomo forever no teach ing and hardship allowance never kufundisha mgo mo wa madaktar muhmbili walipel eka jeshi tell the m wawalete na huku ktk shule za sekondari za kata na za msing huku vijijini kalag abaho.mshikama no daima.
 
Madaktari wanajeuri hiyo ya kugoma lakini si walimu,mtaniambia wadau serikali ikitisha kidogo tu wataufyata mkia maana miongoni mwao wamo ambao walipata kazi ya ualimu kwa kutotimiza vigezo ikiwemo na kufoji vyeti!Hawa jamaa hawajiamini hata kidogo siamini kama watashikilia msimamo wao.
 
Dah,nchi na serikali inapita kwenye kipindi KIGUMU SANA,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
USISHANGAE USIKU WA LEO AU KESHO MAHAKAMA IKASITISHA MGOMO
Hicho ndicho kitakachjotokea... isichokijua serikali ni kuwa huku kukimbilia mahakamani ni kuahirisha tatizo. Ilitakiwa itafute suluhisho la madai ya walimu. Imeahirisha tatizo la madaktari, sasa itaahirisha tatizo la walimu, siku nyingine itaahirisha tatizo la kada nyingine... siku yakija kulipuka hayop matatizo serikali isishangae kujiku ikiwa nje ya madaraka
 
Jaribuni kugoma muone moto wa serikali. Na vyeti vyenu vya kubumba bumba mtaenda wapi?

Nilikuwa sijui sababu ya wana JF kuficha majina yao halisi. Kwa mfano huyu beast ametukana NECTA eti inatoa vyeti vya kubumba, ametukana serikali eti inaajiri watu wa kubumba, ametukana walimu eti hawana elimu, amejitukana mwenyewe eti ana elimu ya kubumba aliyopokea kutoka kwa walimu wa kubumba. Sijui kama KUBUMBA ni kiswahili kweli?
 
Back
Top Bottom