CUF yameguka vipande vipande

Unadhani bila sijida Angepewa ile posti? Hahaaa!(cjasema)

Jina "Mtatiro" asili yake ni mkoa wa Mara (jina la Wakurya). Iwapo jina la "Mtatitro" alilipata baadae (according to you), ktk mihangaiko ya maisha, ina maana kwamba yeye julius sio mzaliwa wa mkoa wa Mara ? ..... I just wish to know.
 
Jina "Mtatiro" asili yake ni mkoa wa Mara (jina la Wakurya). Iwapo jina la "Mtatitro" alilipata baadae (according to you), ktk mihangaiko ya maisha, ina maana kwamba yeye julius sio mzaliwa wa mkoa wa Mara ? ..... I just wish to know.
(Tetesi).......Ni wa hukohuko, ila alilichukua baada ya kudunda std7....akiwa hukohuko mkoani (mara). Usininukuu tafazali. Lol
 
Cuf Ni taasisi kwny makaratasi na ndio mana ikapata usajili kisheria, lakini katika hali halisi hakuna taasisi pale, iko kwa ajili ya wachache kwa personal interest baaasi.Maisha yatasonga mbele hata siku cuf ikifa pia, huwezi kufananisha mazingira aliyotoka Nyerere katika uongozi na huu uozo unaoendelea ndani ya cuf sasa, kwa taarifa yako Kama unavyofahamu 2015 haitokuwepo hiyo cuf unayoizungumza. Huwezi kufukuza viongozi waandamizi wa chama na tizama hili la mtatiro, from no where anaropoka tu ooh! Hata hao waliojitoa mlishapanga kuwatimua kwny kikao kijacho..madudu gani haya?

Hahahaha naona we mfuasi wa kibwetere (HR) limekuganda...! Kwa kukuongezea mashaka na presha nakuhakikishia CUF itabaki imara siku zote! Hao wanaoondoka na watakaondoka (baada ya huku ya HR) hawakustahili kuwemo! CUF ni kama bahari, kamwe haikai na uchafu, lakini pia haikauki!

CUF si chama cha msimu, ndo mwanzilishi wa vyama vingi, ni chama dume, ni mzoefu wa siasa! Ni imara! Hili ni wimbi tu linapita, halafu litatulia, hakuna bahari isiyo na mawimbi!
 
Mkuu wangu udini ni dhambi mbaya sana.Tuweke itikadi zetu pembeni tutetee taifa letu kwanza.Kitendo alichofanya Jussa kinafaa kulaaniwa na watanzania wote hata wewe ukiwemo.Mkuu wangu kwangu mimi Taifa ni bora kuliko vyama vyetu hivi.
Kama huo ndio mtizamo wa CUF na wazanzibari wote unadhani atalaaniwa?
 
Lipumba1(23).jpg

Profesa Ibrahim Lipumba


Jinamizi la kufukuzwa uanachama Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed, na wenzake 10, limezidi kukitafuna Chama cha Wananchi (CUF), baada ya viongozi watatu waandamizi Taifa, kutangaza kujitoa katika chama hicho, huku wakimshauri pia Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, kufuata nyayo zao ili kulinda heshima na hadhi aliyonayo kitaifa na kimataifa.
Waliotangaza uamuzi huo ni Abubakar Rakesh ambaye ni mtu wa karibu na swahiba mkubwa wa Profesa Lipumba; aliyewahi kuwania ubunge kwa tiketi ya CUF Jimbo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Juma Kilaghai. Wote ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa; na Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Vijana wa Chama hicho Taifa, Omar Constantine.
Walitangaza uamuzi wao huo jana walipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwezi mmoja tangu Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa, litangaze kuwavua uanachama wa chama hicho Hamad na wenzake, uamuzi ambao wameupinga Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Akitangaza uamuzi huo kwa niaba ya wenzake jana, Rakesh alisema pamoja na mambo mengine, umetokana na kuchoshwa na kile alichokiita Umungu-mtu aliojipachika Katibu Mkuu wa CUF, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, katika chama hicho.
Rakesh alimshauri Profesa Lipumba kutoendelea kuwapo ndani ya CUF akisema kufanya hivyo kunaweza kusababisha apoteze heshima na hadhi aliyonayo kitaifa na kimataifa.
"Simshauri Profesa Lipumba kuendelea kwenye CUF. Namshauri kwamba ndani ya CUF atapoteza heshima yake. Hivyo, akija (kutoka Marekani) awaite waandishi wa habari kama hivi, kisha atangaze kujitoa CUF," alisema Rakesh.
Alisema Maalim Seif amekuwa Mungu-mtu ndani ya CUF katika maamuzi ndani ya chama hicho hata kama ya kukinyonga chama na kwamba, hataki kuona maendeleo ya chama hicho yakipatikana, hasa upande wa Tanzania Bara.
Rakesh alisema zaidi ya hivyo, anao ushahidi madhubuti kwamba, ndani ya CUF kuna mtu aliyepandikizwa ili kufanya kazi mahsusi ya kukiua chama hicho kwa maslahi binafsi.
Alisema mtu huyo amepewa maelekezo kufanya kila liwezekanalo, ikiwamo kutengeneza migogoro ili ifikapo Juni, mwaka huu, awe amehakikisha CUF inakufa, hasa upande wa Tanzania Bara.
"Na mkimtafuta huyo mtu mtampata. Ni bingwa sana wa migogoro," alisema Rakesh.
Alisema mtu huyo ambaye ni katika viongozi wakuu wa CUF amekuwa akichochea na kuendekeza migogoro tangu alipokuwa akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Rakesh alisema kutokana na CUF kuwa katika hali mbaya kutokana na fitina za baadhi ya viongozi wake wakuu, hivi sasa wilaya zaidi ya 250 Tanzania Bara zimetelekezwa kwa kukosa uongozi.
"Hivyo, tumeona tutoke mapema (katika CUF)…Tunajivua nyadhifa zetu na kukihama chama," alisema Rakesh na kuongeza kuwa baada ya kutangaza uamuzi huo hatua inayofuata itakuwa ni kumuandikia barua Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Lipumba, kumuarifu kuhusu uamuzi wao huo.
Alisema sababu nyingine iliyowafanya kufikia uamuzi huo, ni kesi iliyofunguliwa na Hamad na wenzake kupinga kuvuliwa uanachama.
Rakesh alisema kesi hiyo ni mbaya, hivyo wanaogopa kufungwa jela.
Katika kesi hiyo, Hamad na wenzake walifungua maombi madogo mahakamani wakiiomba mahakama pamoja na mambo mengine iwaite wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF, akiwamo Maalim Seif, wajieleza kwanini wasifungwe jela.

Hamad na wenzake wanataka wajumbe wa baraza hilo wajieleze hivyo, kwa madai ya kukiuka amri halali ya mahakama iliyowazuia kuendelea na mkutano wa Baraza hilo, ambao ulitumiwa kuwavua uanachama katika chama hicho.

Rakesh alisema uamuzi wa kujitoa CUF hauna ushawishi wowote wa Hamad, bali wanachokifanya ni kusimama katika haki na ukweli.
Alisema sababu zote walizozitaja zilizowafanya wafikie uamuzi huo, aliwahi kuzizungumza pia katika vikao vya chama.
Pia alisema hana tabia ya kupindisha ukweli, hivyo wakati wowote akiitwa mahakamani katika kesi ya Hamad na wenzake kwenda kuueleza anachokijua kuhusu mvutano uliopo unaohusu amri ya mahakama iliyozuia mkutano ule wa Baraza Kuu kufanyika, kama CUF waliipata amri hiyo mapema au hawakuipata kabisa, atakuwa tayari kwenda kutoa ushahidi alionao.
Kwa upande wake, Constantine alisema miongoni mwa mambo yaliyomfanya afikie uamuzi wa kujitoa CUF, ni kauli ya ubaguzi wenye misingi ya dini, Ubara na Uzanzibar aliyodai kuwa ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Tanzania Bara, Ismail Jussa Ladhu.
Alidai kauli hiyo ilitolewa na Jussa kufuatia matokeo mabaya iliyoyapata CUF katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika Jimbo la Uzini, hivi karibuni.
Constantine alisema baada ya CUF kushika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo, Jussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mjimkongwe, alikaririwa akisema kilichosababisha matokeo hayo kwa CUF, ni wingi wa wananchi wa Tanzania Bara na Wakristo, waliopo katika jimbo hilo.
Alisema kauli hiyo ya Jussa inapingana dhahiri na madhumuni ya CUF namba moja yanayopinga kauli na matendo ya ubaguzi kufanywa na mwanachama yoyote wa CUF kwa misingi yoyote nchini.
"Kauli hiyo ya Jussa inathibitisha kwamba, mahali ambako kuna wananchi kutoka Tanzania Bara na Wakristo hakuna CUF. Huu ni ubaguzi mkubwa usioweza kuvumilika," alisema Constantine.
Naye Kilaghai alisema wanaCUF hawana sababu ya kumtafuta mchawi kwingine, bali wajue kwamba, anayeibomoa CUF ni Maalim Seif na Kamati Tendaji ya Chama hicho Taifa.

Alisema matokeo iliyoyavuna CUF kwenye uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la Uzini, ni uthibitisho tosha kwamba, Wazanzibari wameanza kuona ubaya wanaofanyiwa na Maalim Seif na kamati hiyo ambayo ni chombo cha juu cha maamuzi katika chama hicho.

Kilaghai alisema CUF imepoteza mwelekeo na kwamba, ushahidi wa hilo ni kauli za kukinzana ambazo katika siku za hivi karibuni zimekuwa zikitolewa hadharani na viongozi wake wakuu.
Kutokana na hilo, aliwataka wanaCUF waliobaki kuhakikisha wanakiokoa chama chao kutoka katika makucha ya wote waliobainika kuwa na njama za kukiua chama hicho.

CHANZO: NIPASHE
 
CUF ndo inazidi kupotea na mwaka 2015 CDM tunaingia visiwani tukiwa full
 
Naye Kilaghai alisema wanaCUF hawana sababu ya kumtafuta mchawi kwingine, bali wajue kwamba, anayeibomoa CUF ni Maalim Seif na Kamati Tendaji ya Chama hicho Taifa. Alisema matokeo iliyoyavuna CUF kwenye uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la Uzini, ni uthibitisho tosha kwamba, Wazanzibari wameanza kuona ubaya wanaofanyiwa na Maalim Seif na kamati hiyo ambayo ni chombo cha juu cha maamuzi katika chama hicho. Kilaghai alisema CUF imepoteza mwelekeo na kwamba, ushahidi wa hilo ni kauli za kukinzana ambazo katika siku za hivi karibuni zimekuwa zikitolewa hadharani na viongozi wake wakuu. Kutokana na hilo, aliwataka wanaCUF waliobaki kuhakikisha wanakiokoa chama chao kutoka katika makucha ya wote waliobainika kuwa na njama za kukiua chama hicho.QuoteHuyu Kilaghai vipi tena?Yaani anawashauri wakiokoe chama wakati yeye kashindwa kwa nini asiwashauri wakihame kama yeye?
 
NASIKITISHWA KWA KUONA MWANACHAMA MKONGWE MWINGINE KUTOKA CUF AKIJITANGAZA KUJITOA KUTOKA KATIKA CHAMA CHAKE, ABOUBAKARI RAKESH NA WAFUASI WAKE WAZIDI KUNYONG'ONYESHA CHAMA. NA KUMSHUTUMU MTATILO KUDHOOFISHA CHAMA KWA UPANDE WA BARA.
........KWA MTINDO HUU CUF NI SAWA BAISKELI YA UDONGO KIPINDI CHA MASIKA HAIWEZI KUMALIZA SAFARI...........:shock:
 
Mbona hao viongozi wa kafu kutwa kwenye tv wanasema hakuna mwanachama wa kafu aliyerudisha kadi?

1.Mamushii nakuona na kapuu la matunda mie zani dondoka njoo nkupe buku.

2.Hv hayo mambo tunayozungumza watayasikia au nsije nkawa napoteza muda tu? Hali ya micheweni tangia asubuhi tuu duunii.
 
Awali ya yote napenda kuwapongeza na kuwapapole kwa ujenzi wa taifa letu tulijengalo kwa hisia tukitumai kwa ndoto kwamba litaendelea kwa midomo tu ya wanasiasa walioishiwa mbinu na kubaki na mbinu za kundelea kutuibia na kujipangia madalaka kwamba baada yautawala wangu kuisha utafuata wewe bila kujali na kujiuliza kwamba aliye maliza kuiongoza nchi ameisaidiaje? na atakaye fuatia afanyenini ili taifa letu lilete tija na kuendelezwa?

Kwa awali, sasa na kueendelea imeonekana zaidi watu ama viongozi wapo kwa maslai binafsi ambayo yameanza leta migawanyiko ya wenyewe kwa wenyewe.

CUF kimemeguka na kinaendelea na mgawanyiko huo hii yote ni kutokana na sababu ya wao kuachana na umoja wao waliokuwanao kama CUF na kuamua kuungana na CCM kwa upande wa zanzibar tena kwa siri bila yawananchi wao ambao kwa mantiki ndio wanao wapa nafasi za ushindi na kuwawakilisha wao kama wanchi.

Sababu hiyo ndiyo imewafanyawanaCUF wabunge kushindwa kuwa na hoja nzito kama ambavyotuliwazoea apo awali. Ndiyo maana hadi kila tuamukapo hakuishi kujitoa na wengine kutakakuanzisha chama chao kimya.

Fanyeni hivyo mkiweza lakini mtuambie watanzania na wanaCUF mwafanya hivyo kwamanufaa ya nani yaani NYIE AMA WANACUF NA WATANZANIA WOTE kama hivyo ni ipi mikakati mnayoendakujanayo.
 
Hhahahah munaota ndoto ya Alinachu. Eti, CUF inameguka. Mbona munachekesha. CUF wana "base" ya kutegemea. Nyinyi walalahoi muna nini?. Hawa wasaliti wamejondoa sabaubu wanajua wazi kuwa kifimbo cheza kitafanya kazi yake. Kwa hivo, kabla kuadhirishwa ni kheri wakae upande. Sasa hivi tumo katika uzinduzi mpya wa kukiendeleza chama bar na tunawahakikishia Watanzania kuwa CUF itakuwa chama kikuu cha kutisha CCM kuliko vyama vengine na tuna harakati kabambe ya kuchukua mwaka wa 2015. Usimuone simba kanyeshewa na mvua ukadhani ni mpaka. Utaliwa mzima mzima.
 
Hahahaha naona we mfuasi wa kibwetere (HR) limekuganda...! Kwa kukuongezea mashaka na presha nakuhakikishia CUF itabaki imara siku zote! Hao wanaoondoka na watakaondoka (baada ya huku ya HR) hawakustahili kuwemo! CUF ni kama bahari, kamwe haikai na uchafu, lakini pia haikauki!

CUF si chama cha msimu, ndo mwanzilishi wa vyama vingi, ni chama dume, ni mzoefu wa siasa! Ni imara! Hili ni wimbi tu linapita, halafu litatulia, hakuna bahari isiyo na mawimbi!

Mimi ninavyojua NCCR Mageuzi walikuwa ndio wa kwanza, vipi wewe useme CuF ndio waanzilishi wa vyama vingi?
Ufafanuzi tafadhali, au?
 
Hahahaha naona we mfuasi wa kibwetere (HR) limekuganda...! Kwa kukuongezea mashaka na presha nakuhakikishia CUF itabaki imara siku zote! Hao wanaoondoka na watakaondoka (baada ya huku ya HR) hawakustahili kuwemo! CUF ni kama bahari, kamwe haikai na uchafu, lakini pia haikauki! CUF si chama cha msimu, ndo mwanzilishi wa vyama vingi, ni chama dume, ni mzoefu wa siasa! Ni imara! Hili ni wimbi tu linapita, halafu litatulia, hakuna bahari isiyo na mawimbi!
Kibwetere?!! Haya SULTANI maalim! HAKIIII (kwa wachache!)Inasikitisha kuona Zanzibar sio Tanganyika kuna watu wengi sana bado mmelala....kwa komenti hii ww Ni lazima wa Huko visiwani tu Sikulaumu, lakini elewa kwamba yeyote mwenye upeo sahihi hawezi kuzungumza ulichoandika, udume huo wa Cuf umeujulia wapi? Je, unafahamu kwamba huyo Bwana wako Maalim alikaribishwa kwny chama na huyo kibwetere unayemtaja? Nani anayeweza kuzungumza CUF hapo! Uwepo wa cuf upo tu na utaendelea kuwepo lakini lakini Ni dormant! Ni sawa na mfu tu AMA jiwe....kaa ukielewa 2015 kura hazitotosha, hakutokuwa na Viti maalum, na Huko Pemba mtagawana Viti na kibwetere ilhali atakuwa na Viti vya kutosha bara....imekaaje hiyo hapo?!
 
Hahahaha naona we mfuasi wa kibwetere (HR) limekuganda...! Kwa kukuongezea mashaka na presha nakuhakikishia CUF itabaki imara siku zote! Hao wanaoondoka na watakaondoka (baada ya huku ya HR) hawakustahili kuwemo! CUF ni kama bahari, kamwe haikai na uchafu, lakini pia haikauki! CUF si chama cha msimu, ndo mwanzilishi wa vyama vingi, ni chama dume, ni mzoefu wa siasa! Ni imara! Hili ni wimbi tu linapita, halafu litatulia, hakuna bahari isiyo na mawimbi!
Kibwetere?!! Haya SULTANI maalim! HAKIIII (kwa wachache!)Inasikitisha kuona Zanzibar sio Tanganyika kuna watu wengi sana bado mmelala....kwa komenti hii ww Ni lazima wa Huko visiwani tu Sikulaumu, lakini elewa kwamba yeyote mwenye upeo sahihi hawezi kuzungumza ulichoandika, udume huo wa Cuf umeujulia wapi? Je, unafahamu kwamba huyo Bwana wako Maalim alikaribishwa kwny chama na huyo kibwetere unayemtaja? Nani anayeweza kuzungumza CUF hapo! Uwepo wa cuf upo tu na utaendelea kuwepo lakini lakini Ni dormant! Ni sawa na mfu tu AMA jiwe....kaa ukielewa 2015 kura hazitotosha, hakutokuwa na Viti maalum, na Huko Pemba mtagawana Viti na kibwetere ilhali atakuwa na Viti vya kutosha bara....imekaaje hiyo hapo?!WIMBI HILI HALIPITI BURE BURE LINAONDOKA NA CHOMBO.
 
Back
Top Bottom